Usalama wa Rais ni muhimu kuliko usalama wowote ule katika Nchi

Africa tishio kubwa la usalama wa viongozi sio raia makapuku wanaopigwa na jua barabarani bali ni watu wa ndani ya mfumo wenyewe, Africa ni nadra sana kusikia mwananchi wa kawaida amemdhuru au amekusudia kumdhuru kiongozi.

Nchi kama Marekani na za Ulaya ambapo tishio kubwa la usalama ni raia wa kawaida wa mitaani wanaomiliki sila za kivita kirahisi bado viongozi wao hawalindwi na misururu ya magari, jammers, helikopta na vifaru. Africa pia runaweza kutumia akili nyingi zaidi kuliko nguvu kuokoa mabilioni ya pesa tunayotapanya kwa vitu visivyo na msingi.
Man this is africa
 
Man this is africa
Abeid Karume, Thomas Sankara, Laurent Kabila, Juvenal Habyarimana-Burundi , Samuel Doe- Liberia, Dadis Camara, Murtala Mohammed-Nigeria na wengine wengi walidhuriwa na watu waliokuwa karibu nao kabisa(inner circle), sio walalahoi wa huko mtaani wanaokingwa na kuta za magari, mabunduki na vifaru.
 
Mungu ndiye mwenye dhamana ya uhai wa mtu Nani alitegemea Magufuri kuondoka kwa ulinzi aliojiwekea? Inabidi wajue "Adui wa mtu ni wale wa nyumbani mwake"
Wakidhani adui atatoka nje ya wanaomzunguka subiri muda utajibu
 
Hakuna mlinzi hapo, wote hao ni wasaka tonge tu. Wanajaribu kujikwamua na hali ngumu ya maisha inayomkabili karibu kila mmoja wetu.

Kuna marais wamewahi kuwa na ulinzi hata sisimizi alikuwa hawezi kutambaa walipokuwa lakini waliuliwa tena kirahisi kabisa, historia ni shahidi mzuri.

Ni kweli hizo ni mbinu tu za watu kujiingizia kipato zaidi kwani mishahara si chochote. Hata Alpha Conde alikuwa na ulinzi vile vile.
 
Hii ni aibu kubwa sana. Mantiki ya aina hii ya ulinzi ni ya ajabu sana. Okay hata kama sasa kweli kuna tishio watazuiaje na wanayemlinda yuko juu ya gari? au hata wakimuona mhalifu, si wataua watu wengi tu including wao wenyewe? Hii approach sijui wameitoa wapi badala ya kuendeleza passive approach ambayo viongozi wote hupewa? Wajameni, mnamharibu sana taswira ya mama na nchi yetu.
Nilishangazwa hata Rais wa Zanzibar alipoenda kufunga maonyesho huko Arusha alikuwa anasindikizwa na mabunduki na makombati kama vile pale kuna Boko Haram wakujitoa muhanga. Ni shida kweli wajameni.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Hii ni aibu kubwa sana. Mantiki ya aina hii ya ulinzi ni ya ajabu sana. Okay hata kama sasa kweli kuna tishio watazuiaje na wanayemlinda yuko juu ya gari? au hata wakimuona mhalifu, si wataua watu wengi tu including wao wenyewe? Hii approach sijui wameitoa wapi badala ya kuendeleza passive approach ambayo viongozi wote hupewa? Wajameni, mnamharibu sana taswira ya mama na nchi yetu.
Nilishangazwa hata Rais wa Zanzibar alipoenda kufunga maonyesho huko Arusha alikuwa anasindikizwa na mabunduki na makombati kama vile pale kuna Boko Haram wakujitoa muhanga. Ni shida kweli wajameni.
Nadhani ulinzi wa aina hii wame focus zaidi mikoa ya Kaskazini.
 
kwani kaskazini kuna tishio gani dhidi ya mama? Kama ni show of force sawa, lakini dhidi ya nani?
Wamekariri kwasababu ya historia na matendo ya mwendazake kwa watu wa kule.
 
Black Belts kasema eti "Rais lazima alindwe kwa 'ghalama' zote" wakati akimjibu Lord Osagyefo aliyesema usalama wa rais hautegemei wingi wa magari na helikopta... duh! Fuso alihesabu magari 39 ya walinzi katika msafara wa rais na Bak katupia ka-foto kakionyesha walinzi wakiizingira gari ya rais... yaani, kwa macho ya wengi, ni full ulinzi. Na kuna watu wanaamini kuwa hapo mama kalindwa! Mi naona wanajidanganya.
Historia ina viongozi wengi sana waliouawa wakiwa katika misafara na/au wakihutubia wananchi... tena wakilindwa vilivyo. Hao walinzi waliolizingira hilo gari alipo rais wanaonekana kulilinda gari zaidi kuliko kumlinda rais.
Katika dunia ambapo haya mavitu yaitwayo "ma-drone" yanayo jiendesha yenyewe yanapatikana kama bidhaa yoyote ile, na masilaha ya aina kadha wa kadha yapo, ulinzi wa staili zetu za kiafrika ni kuwabebesha walipa kodi gharama zisizo za lazima. Ni kweli rais lazima alindwe, lakini isionekane kama vile ni maonyesho fulani yenye madoido makali kwa gharama kwa mwananchi - Magari 39-petroli. Walinzi (?), madereva(?), Wasaidizi(?)-posho aka kodi za wanyonge!! Kwa nchi ombaomba ya Tz!! ...dah! Tutakoma
 
Ndiyoo SSH alindwee ...Kwa maombi na dua... Ikulu kama taasisi itoe elimu ya uraia has a Kwa wanasiasa /vijana wetu ... Kama Rais na baraza lake wanaapa kutotoa siri za baraza - iweje mwanasiasa/harakati/mfurukutwa / nk anaenda payuka hizo siri majukwaani - SIRI ZA NCHI !!.?? ...ukibanizwa na Menyewe unaanza kulaumu Raising .. - Hapa elimu bado haijafika ...wahusika waelimishe watu ...Vijana ; ukishambulia kwa maneno yasiyo staha hio taasisi ya nchi siyo Hekima na in htr pia
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Katika Mambo ambayo sijawai kuyakataa katika taifa letu ni juu ya ulinzi wa Rais.

Mwalimu Nyerere alinusulika kupinduliwa zaidi ya Mara tatu kwa sababu ya misimamo yake na uzalendo wake kwa nchi.

Ukitaka ulinzi wako uwe wa kawaida kuwa shamba la Bibi.

Magufuli watu walimlalamikia Sana juu ya ulinzi wake kuwa mkubwa lakini Mimi niseme kabisa Magufuli hakuwa na ulinzi mkubwa kivile Kama watu wanavyosema maana jamaa alikuwa anajiamini Sana.

Ulinzi aliokuwa nao ni vile idara ilimlazimisha kwamba upo kisheria na kulingana na jinsi alivyokuwa anaishi na watu alitakiwa kuwa na ulinzi mkubwa zaidi labda yasingetokea hata yaliyotokea mwezi 3 ingawa tunasema mipango ya Mungu haina makosa.

Rias Samia alindwe na ikiwezekana aongezewe ulinzi swala la ulinzi wa Rais wetu lisifanywe kisiasa kwa sababu sio swala la kisaisa ni la mstakabali wa Nchi kwa ujumla.

Wote Ni mashaidi kilichomtokea Rais Samia akiwa ziarani Morogoro Yule traffic aliyekatiza mbele ya Gari lake bila kuonekana kwani alitakiwa kukamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi ila akaachwa.

Angalia kilichomkuta Rais wa Ufaransa baada ya kupokea kibano kutoka kwa raia baada ya kujifanya mtu wa watu unaweza kuwa mtu wa watu kweli lakini not to the extent!!

Rais wa Nchi anakuwa na Marafiki wengi na Maadui wengi kulingana na anayoyafanya yeye sio maraika.

Kuna watu wanahoji juu ya ulinzi wake kwa Sasa kuimalishwa na Mimi nawakumbusha ulinzi wa Rais ni kwa mjibu wa katiba na sheria za Nchi Wala sio matakwa yake binafsi.

Hivyo ulinzi wake usiusishwe na siasa zetu maana Hata Rais akiwa mzuri vipi anawindwa Kuna makundi ambayo hayakubaliani naye but hata Kama makundi hayo hakuna Rais anatakiwa kulindwa anapokuwa salama na taifa linakuwa salama atafanya maamuzi kwa Uhuru na Hali bila kumhofia mtu yeyote.

Naomba usalama wa Rais ubakie kuwa chini sheria na katiba na watu waliopangwa kumlinda sisi wengine hakuna tunachojua.
Sisi tubishane kwa hoja zetu za kisiasa kuchumi na Mambo ya kutafuta katiba mpya.

Tukumbuke rais akiwa salama na sisi tunakuwa salama Kama Nchi.

Mngejua taharuki iliyotokea Hayati Magufuli alipokufa akiwa madarakani Mngeomba kabisa ulinzi wa Rais Samia uongezwe maradufu.

Rais wetu alindwe asiwe na presa na mtu yeyote na kikundi chochote juu ya maamuzi yake Rais Ni wa Nchi sio wa ccm Wala kikundi chochote akipata tatizo tatizo ni la Nchi naomba Rais aongezewe ulinzi kila Mara pale inapobidi.
Fact...Rais amebeba dhamana ya nchi na itakuwa ujuha kutokumlinda Rais wetu. Hatari yeyote kwa Rais ni hatari kwa nchi na amani ya watu. Mungu mlinde Rais wangu, ilinde nchi yangu na utulinde raia wake. Maana bila amani na usalama hakuna alitakayekuwa salama
 
Back
Top Bottom