Usalama wa Rais apandapo Helkopta wakati wa kampeni

From Sir With Love

JF-Expert Member
Sep 13, 2010
2,076
3,797
Rais John Pombe Joseph Magufuli anaendelea na kampeni kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa tarehe 28 Octoba 2020.

Mimi kama mwananchi wa kawaida, naomba nitoe angalizo kuhusu kutumia helicopter kama usafiri afanyapo kampeni.

Wana anga wanasema rate ya helicopter kupata ajali ni kubwa ukilinganisha na ndege za abiria kwa sababu;

1. Helicopter ina vikorokoro/vifaa vingi ambavyo vinakuwa kwenye movement iwapo angani, kwa maana hiyo kama haikufanyiwa service madhubuti uwezekano wa kifaa mojawapo kufail ni kubwa. Lakini pia tear and wear ya helicopter ni kubwa.

2. Helicopter ina rubani mmoja, na hivyo umaakini ukipungua, hakuna msaada wa rubani mwenza.

3. Taratibu za ukaguzi kwa ndege za abiria na helicopter zinatakiwa ziwe za kiwango cha hali ya juu kutokana na taratibu za anga, lakini mara nyingi, helicopter zinazomilikiwa na watu binafsi au mashirika huwa hazifanyiwi service za maana kama inavyotakiwa.

4. Ni rahisi kutemper na kifaa mojawapo kirahisi na kwa makusudi kabisa ili kusababisha ajali.

5. Mazingira ya urukaji wa helicopter inaweza kuathiriwa na vitu vinavyozunguka na hivyo kusababisha ajali tofauti na ndege za abiria.

Sababu zipo nyingi lakini kwa leo tuachie kwenye hizi tano. Mimi kama raia na mwananchi wa kawaida kabisa, nashauri chama changu cha CCM kimwache mgombea urais wetu aendelee kutumia barabara japo inachosha ili amalizie kampeni zake.

Kumbukumbu:
Mwaka 2014, Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Bilal, Waziri wa Ujenzi Dr. John Magufuli, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Said Meck Sadick na kamanda wa polisi, kanda maalum ya Dar es salaam Suleiman Kova walinusurika kwenye ajali ya ndege ya helicopter iliyokuwa inamilikiwa na JWTZ baada ya ndege hiyo kugonga ukuta na kudondoka kwenye uwanja wa ndege wa Dar es salaam.
 
Kwanza jiulize Kuna ajali ngapi za helikopta Tanzania ? Kuna ndugu yako amewahi kufa kwa ajali ya helikopta ? Kuna mtu yoyote unayefahamiana naye amewahi kufa kwa ajali ya helikopta ? Halafu jiulize maswali hayo hayo juu ya usafiri wa barabarani (magari)
 
Kuna Watu huwa nawashangaa mno na sijui hata Vichwani mwenu huwa mna nini. Hivi kuna Mwanadamu ambaye kapangiwa Kuishi daima Milele?

mkuu hata wewe tunajua utakufa tu,ila ukifa sasa hivi kwa boda boda kwa ubishi wa kutovaa helmet tutapata hasara.maana hata mapopoma mna kazi nyingi pia.
 
Kwanza jiulize Kuna ajali ngapi za helikopta Tanzania ? Kuna ndugu yako amewahi kufa kwa ajali ya helikopta ? Kuna mtu yoyote unayefahamiana naye amewahi kufa kwa ajali ya helikopta ? Halafu jiulize maswali hayo hayo juu ya usafiri wa barabarani (magari)
Upo sahihi kwa njia moja au nyingine. Usafiri wa helicopter ni salama kabisa kuliko gari. Ila tambua usalama unaokuwepo wakati wa msafara wa Rais ni mkubwa sababu panakuwa hamna magari mengine zaidi ya yale ya msafara na hamna magari wanayopishana nayo.
 
Naona mpaka rais kupanda hy hell-kopta bc imesha fanyiwa uchunguz wa kutosha
 
Back
Top Bottom