Usalama wa raia kwa sasa sio kipao mbele cha Polisi tena?

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,143
18,774
Ukiangalia tukio la hivi karibuni la FFU kupiga raia na ni muda gani ulipita kabla jeshi la polisi halijachukua hatua, karibuni siku nne au tano, basi ni rahisi kuona kuwa usalama wa raia na mali zao sio kipao mbele tena cha jeshi letu la Polisi. Inaonekana kama jeshi la Polisi sasa limejikita zaidi katika mambo ya kisiasa na kufuatilia wapinzani kulingana na matakwa ya uongozi uliopo madarakani wa CCM.

Kitu kinachofanya hilo liwe dhahiri ni ile spidi na nguvu kazi ambayo jeshi la Polisi linatumia kufuatilia makosa madogo madogo kama kauli zinazotolewa na viongozi wa upinzani, kuzidisha muda kwenye mkutano wa kisiasa, makala za magazeti na hata jumbe za raia katika mitandao ya kijamii. Polisi huchukua hatua mara moja!

Mara nyingi hata tumesikia kauli kuwa ikiwa jeshi letu la Polisi lingepambana na ujambazi nchini kwa jitihada na rasimimali kwa kiwango kile kile wanachotumia kushughulika na wapinzani na makosa ya kisiasa, basi hali ya usalama ingeimarika sana nchini. Juzi hapa tulishuhudia Polisi kufikia hatua ya kutuma askari kwenye press conference ili kumkamata Sheikh Ponda kabla hata Polisi hawajajua Ponda angesema nini, na hata kukamata waandishi wa habari ili wawaambie Ponda alisema nini kwenye press conference.

Kama raia wa Tanzania, tunasubiri kuona mamlaka za juu zikiwawajibisha Polisi kwa kuchelewa mno kuchukua hatua kwa FFU waliokuwa wakipiga raia. Kwa nini ichukue zaidi ya siku moja kabla hali ile kudhibitiwa? Haiingii akilini kwamba Polisi pamoja na IGP walikuwa hawana habari na kilichokuwa kikiendelea. Je, waliacha makusudi raia waendelee kupigwa?

Ningependa kumkumbusha Raisi Magufuli na IGP kuwa katika tukio kama lile la FFU kupiga raia, raia walikuwa na kila haki ya kujilinda dhidi ya mashambulizi yale ya FFU (self defence). Raia hawakufanya hivyo si kwa uoga, bali kwa kutojua haki yao ya self defence katika mazingira kama yale. Sasa kama hali hii itaachiwa iendelee, au hatua zisichukuliwe dhidi ya Polisi walioachia hili likaendelea kwa zaidi ya siku moja, basi kuna siku watasikia mpambano wa kumwaga damu kati ya polisi na raia, si tu FFU kupiga raia wanaokimbia. Mark my words.
 
Sidhani kama kweli watakuja kujuta
Mkuu, ulimwengu huu unabadilika kila siku. Ni kweli watu wanabaki wale wale, lakini systems zinabadilika. Jana kulikuwa na KANU, leo haipo. Jana kulikuwa na Idd Amin, leo hayupo. Lakini watu waliokuwepo wakati wa KANU, wakati wa Idd Amin bado wapo!
 
Mkuu, ulimwengu huu unabadilika kila siku. Ni kweli watu wanabaki wale wale, lakini systems zinabadilika. Jana kulikuwa na KANU, leo haipo. Jana kulikuwa na Idd Amin, leo hayupo. Lakini watu waliokuwepo wakati wa KANU, wakati wa Idd Amin bado wapo!
Noted
 
Kipaumbele sasa hivi nikukusanya mapato.. Maana jeshi LA polisi limegeuka TRA kivuli
 
Back
Top Bottom