Usalama wa Mtu kama Peter Kibatala unawekwa vipi

Heri nyingi zimeorodheshwa katika Mathayo 5:

"......Heri yenu nyinyi watu wakiwatukana, wakiwadhulumu na kuwasingizia kila aina ya uovu kwa ajili yangu. Furahini na kushangilia maana tuzo lenu ni kubwa mbinguni......"

Heri hizo zinamhusu sana mtu kama Peter Kibatala, kamanda Mbowe na wa namna hiyo. Lakini si SSH, Diwani, Sirro wala Muliro.
Umemsahau ibilisi mwendazake
 
hao unaosema ni heri, ungelijua namna walivyo.............. kwao Ifakara, ungenyamaza tu. hawajamtanguliza Mungu wala nini kwa hiyo don't involve God on this please. wacha tutaniane kisiasa sisi kwa sisi, Mungu mweke pembeni usimwingize kwenye uchafu huu.
 
Lakini poa wakili yeyote tule huwa hana kosa kumtetea mteja.Ndo maana utaona kesi ya mauaji kabisaaa lakini muuaji anapata wakili wa kumtetea,sasa unadhani ndugu wa yule aliyeuawa watamchukuliaje?Wanajua kuwa ile ni kazi na yupo kazini so hana kosa kwa kufanya kazi yake.

Ndo maaana Kibatala hana shida na hata mtu akimletea shida anajitafutia karma na kubeba dhambi tu.

Poa hao wanaowakamata wapinzani wanajua kuwa hili tulilomkamata nalo ni la uongo hivyo ndo maana wanaona kumdhuru wakili ni kujiongezea liana na dhambi zaidi kwa Mungu.Hata wao wana mioyo.
 
Hakika ndugu, ukiiangalia ile clip kwa jicho la haki, bila kuwa upande wowote ule, lazima lazima lazima utatafakari.
Kwa kweli ile clip imenipa tafakuri sana. nimeamini bado kuna watu wanasimamia taaluma zao
 
hao unaosema ni heri, ungelijua namna walivyo.............. kwao Ifakara, ungenyamaza tu. hawajamtanguliza Mungu wala nini kwa hiyo don't involve God on this please. wacha tutaniane kisiasa sisi kwa sisi, Mungu mweke pembeni usimwingize kwenye uchafu huu.

Ulikumbuka kumkumbusha Sirro au mwendazake kutomhusisha Mungu au ndiyo kuchanganyikiwa sasa huku?

Hiiiiii bagosha!
 
Hili limenitafakarisha sana sana, pamoja nyakati ngumu Mungu huwa anawainua watu kwa ajili ya wale waliokufa mioyo. Peter ni shujaa lakini inabidi nae aangaliwe, usalama wake nk.
Unamuagiza nani wa kuangalia usalama wa kibatala
 
Katika miaka ya hivi karibuni takribani 10, jina la Peter Kibatala limekuwa maarufu sana. Umaarufu wake unatokana na yeye kuwa Wakili mashuhuri anayetambulika kama wakili msomi, nimekuwa nikifuatilia aina ya kesi anazopangua na dhidi ya watu anaowashinda, hakika kuna baadhi ya kesi anazoshinda inanipa mtazamo kuwa Peter ni mtu makini, anayejiamini, asiyenunulika wala kurubuniwa.

Napata shaka kuwa matendo ya Ujasiri wake yanaweza kuhatarisha hata uhuru wake, nafsi yake nk. Nasema haya kwasababu naamini wale anaowashinda kwenye kesi mbalimbali huwa hawafurahii.

Je watu kama hawa ambao ni hazina fulani hivi nani anafikiri juu yao, Mungu yupo ni kweli lakini hila, chuki navyo vipo. Tarehe 05.08.2021 nimeona akimfuata nadhani mfuasi wa CHADEMA aliyekuwa chini ya Ulinzi wa Polisi katika gari lao tayari kwa kumpeleka rumande kwa kile kinachosadikika kuwa alionyesha bango katika viunga vya Mahakama.

Amesikika Peter Kibatala akimwambi a huyo mwanachama "kamanda usiwe na wasiwasi we nenda Polisi ila tutakutoa kamanda usiwe na wasiwasi tutakutoa kama sio Polisi tutakutoa Mahakamani "

Hili limenitafakarisha sana sana, pamoja nyakati ngumu Mungu huwa anawainua watu kwa ajili ya wale waliokufa mioyo. Peter ni shujaa lakini inabidi nae aangaliwe, usalama wake nk.
Mawakili kwa mawakili hawana visasi wapo kazini tu wanagombana pale tu wakitoka wanaelewana vizuri..ni kama wabunge tu wa chama tawala na upinzani wakiwa mule ndani utadhani ni maaduni lakini ukiwakuta nje wanakula pamoja na kula pia... Labda tu wakili amkosee mtu lakin suala la kusema kwakua ameshinda kesi ndiyo awe adui siyo kweli..
 
Back
Top Bottom