Usalama wa Mtu kama Peter Kibatala unawekwa vipi

Uwongo wako huo ,ni mlugulu wakwanza msomi toka tumepata Uhuru
Acha hizo wewe na Dr Nicas Guido Mahinda(RIP) unamuacha wapi? Alikuwaga waziri wa viwanda na mbunge wa Morogoro vijijini.Pia alikuwa muhadhiri wa chuo kikuu cha dar alifundisha Inorganic chemistry.Ila najua unatania tu kufurahisha watu kama hutanii umri wako sio mkubwa hujui historia.Je Askofu Telesphory Mkude unamuacha wapi?
 
Unajua tonatofautiana na ndio maana wengine ni mawaziri na wakurugenzi (walipiwa kodi) na wengine ni wananchi walipa kodi..
Kuna mtu akishakula na kushiba hawazi zaidi ya hapo lakini wengine hata akishiba anatamani na mwenzake asilale na njaa.

Hawa wa pili ndio design ya akina TL, Mbowe, Kibatala nk ambao 'usalama' kwao ni kuona kila wanachokiamini kinatokea hata kama ni kupoteza uhai wake. Sisi wengine usalama wetu ni matumbo tu na ndio maana hata tunapokabidhiwa hazina za umma bado tunaiba tu ili kuakikisha shibe ya kizazi cha tatu, mawazo ya kesho inapangwa na Mungu hiyo kwetu hakuna.
One of the best comment. Asante sana mkuu .umeseusema ukweli.
 
Anaoneka mzuri kwasababu anachanganya kazi na ukada wa chama ule upande wa kuwa kada ndo anachukulia umaarufu pale
 
Katika miaka ya hivi karibuni takribani 10, jina la Peter Kibatala limekuwa maarufu sana. Umaarufu wake unatokana na yeye kuwa Wakili mashuhuri anayetambulika kama wakili msomi, nimekuwa nikifuatilia aina ya kesi anazopangua na dhidi ya watu anaowashinda, hakika kuna baadhi ya kesi anazoshinda inanipa mtazamo kuwa Peter ni mtu makini, anayejiamini, asiyenunulika wala kurubuniwa.

Napata shaka kuwa matendo ya Ujasiri wake yanaweza kuhatarisha hata uhuru wake, nafsi yake nk. Nasema haya kwasababu naamini wale anaowashinda kwenye kesi mbalimbali huwa hawafurahii.

Je watu kama hawa ambao ni hazina fulani hivi nani anafikiri juu yao, Mungu yupo ni kweli lakini hila, chuki navyo vipo. Tarehe 05.08.2021 nimeona akimfuata nadhani mfuasi wa CHADEMA aliyekuwa chini ya Ulinzi wa Polisi katika gari lao tayari kwa kumpeleka rumande kwa kile kinachosadikika kuwa alionyesha bango katika viunga vya Mahakama.

Amesikika Peter Kibatala akimwambi a huyo mwanachama "kamanda usiwe na wasiwasi we nenda Polisi ila tutakutoa kamanda usiwe na wasiwasi tutakutoa kama sio Polisi tutakutoa Mahakamani "

Hili limenitafakarisha sana sana, pamoja nyakati ngumu Mungu huwa anawainua watu kwa ajili ya wale waliokufa mioyo. Peter ni shujaa lakini inabidi nae aangaliwe, usalama wake nk.
GREAT POINT, UBARIKIWE SANA.
 
Acha hizo wewe na Dr Nicas Guido Mahinda(RIP) unamuacha wapi? Alikuwaga waziri wa viwanda na mbunge wa Morogoro vijijini.Pia alikuwa muhadhiri wa chuo kikuu cha dar alifundisha Inorganic chemistry.Ila najua unatania tu kufurahisha watu kama hutanii umri wako sio mkubwa hujui historia.Je Askofu Telesphory Mkude unamuacha wapi?
utani mkuu ila ndo mlugulu wetu kwa kizazi hiki kibatala ndo habari ya dunia

Huyu msomi waziri namkumbuka sana tulimuhoji sana aseme sababu za anguko za viwanda vyetu hakusema hadi anakufa, huyo nimsomi?... Aina ya baregu au waziri mkuu mstaafu warioba ndo tunawataka

Tunatamani kuona msomi ule usomi wako hauteteleshwi na mazingira ya kisiasa,
 
Changamoto sio mawakili kwa mawakili, changamoto ni yeye dhidi ya anaowashinda.
Mawakili kwa mawakili hawana visasi wapo kazini tu wanagombana pale tu wakitoka wanaelewana vizuri..ni kama wabunge tu wa chama tawala na upinzani wakiwa mule ndani utadhani ni maaduni lakini ukiwakuta nje wanakula pamoja na kula pia... Labda tu wakili amkosee mtu lakin suala la kusema kwakua ameshinda kesi ndiyo awe adui siyo kweli..
 
"Word"
Namshauri tu aangalie yaliyowatokea Watangulizi wake Nguli katika Fani Marehemu Masumbuko Lamwai na 'Poti' wangu kabisa wa 'Kizanaki' na aliyekuwa Mbunge wangu wa Butiama ( zamani Musoma Vijijini ) Mzee Nimrod Elirehema Mkono.

Namkubali mno PK, ila ajitahidi ajilinde.
 
Back
Top Bottom