Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 29,323
- 40,172
Usalama wa mtu anayetoa pesa kwenye hivi vibanda vya huduma ni mdogo sana.
Leo bi mkubwa alitembelea kibanda kimoja kwa ajili ya kupata huduma ya kutoa salio,na alifanikiwa kutoa kiasi cha mia nane.
Baada ya kupata huduma wakati anatoka katika eneo hilo kama hatua tano hivi, ghafla akatokea kibaka na kunyakua pochi na kukimbia kusikojulikana.
Mbaya zaidi hajamtambua hata sura kwa sababu alikuwa kama vile ameshikwa na bumbuwazi. Baadaye ndio anakumbuka kupiga kelele wakati hata muhusika hajulikani alipo.Alivyonipa taarifa imeniuma sana...lakini nilichoshukuru hakujeruhiwa.
Sasa najiuliza: Katika hali ya namna hiyo ni wangapi wanakwepa hii 'risk' ya kuibiwa pamoja na kujeruhiwa? Na je hivi vibanda vina ulazima wa kuwa na walinzi ili kuzuia wizi wa namna hii?Au baadhi ya vibanda vinashirikiana na wezi/vibaka?