AshaDii
Platinum Member
- Apr 16, 2011
- 16,190
- 18,077
Habari wana JF...
Siku zinavozidi kwena ndio ajali za barabarni zinavozidi kushamiri katika maeneo mbali mbali ya nchi . Kumekua na ajali nyingi na mbaya za watu kupoteza maisha ama kulemaa hadi maeneo ambayo bara bara ni nzuri kabisa hadi observers mwashangaa hasa ilikuaje.
Katika historia ya inchi yetu hii changa sasa hivi idadi ya wamiliki wa magari ni kubwa than ever before Leseni zinavotolewa na mafunzo yanayotolewa kwa wananchi wengi ni ya kienyeji mno! Na ni ukweli na uwazi usiopingika kwamba Watanzania tulio wengi ni mabingwa wa kupenda shortcuts na twapenda saana kurahisisha mambo. Idadi kubwa za lesseni za magari hutolewa hata mhusika anaekatiwa hayupo hapo walau hata kwa interview kuhakikisha kua kweli kapitia Mafunzo stahili.
Serkali imekuja na system mpya na nzuri ya njia ya kupata lesseni (toka lesseni mpya ziwe introduced) as much as kuna some unneccessary berueacracy zinahusishwa pale; ukweli unabaki kua kama kila mmoja ambae ana lesseni angepitia zile stages zooote; hata hao wenye age 50+ ambao wamewekwa kama exceptions katika baadhi ya vipengele ingeweza kabisa ku minimise idadi ya Lesseni zisizo stahili. Badala yake imekua ukiritimba wa hali ya juu na a way and sorce of income katika baadhi ya vipengele hasa pale ambapo Traffic inatakiwa asaini kua wastahili.
Hata hivo nia na madhumuni ya hii thread ni kama a dedication to all those who have lost their lives katika road accidents .. na kutaka na kuomba michango ya my fellow members ambao kweli wana uzoefu mkubwa wa udereva Kwamba kwa wale members ambao hua twapita pita humu hasa via mobile na while wapo on the wheel OR not on the wheel or what ever mode you are using tuweze pata tips za vitu gani ambavo mtu (dereva hata mpita njia) aweza epuka kufanya ili kuweza zuia ajali. Ajali nyingi ambazo zingetokea zingeweza kabisa kuepukika ama kuokoa maisha endapo tu huyo mhusika angeweza pata tip husika. JF is a social network with more than 60000 members Naamini kwa dhati kabisa kua hatutakosa tips za kutosha kuweza zingatia tuwapo barabarani.
Na naamini pia kwmba ni weengi ambao wamepitia experience za road accidents nyiiingi na kwamba waweza share those terrible/horrible na terrible experiences na sababu zilizo cause na ni dhahiri kua zingeweza kwepeka kabisa. Poleni woote ambao mshawahi pata ajali, mshawahi poteza wapendwa/ndugu na jamaa katika ajali na hata kama ushawahi guswa in one way or another katika ajali hizi za kila siku za barabarani.
Kuna wengine ni madereva kabisa lakini hata alama za barabarani hawajui za maanisha nini na wala ziko ngapi Watu wanakufa kwa ajali ni wengi jamani inabidi tubadilike na naamini nakujua kua Change starts from us. Tujaribu kua responsible na tuweze kumbushana. Nitashukuru kwa wale woote ambao watatupa uzoefu wao na kutoa tips . Hata kama ni moja ama a List of them.
Tip zangu
- Please dont drive and use a mobile Ni wengi saana wadharau hii tip, but ni moja ya factor ambayo inachangia saana ajali. Hio ajali sio lazima ipoteze maisha but hata ile tu kuharibu resources (in this sense gari yako) na kuanza gharama ambazo ungeweza epusha.
- Please do not overtake kwenye corner na hata mahala popote hatari bila kupewa ruhusa na aliekutangulia. Ni hatari.
- Please do not forget to use your seat belt.
Mategemeo yangu ni kua tips nyingi na za kitaalam zaidi zitatoka among members.... nategemea sana toka kwenu. Natanguliza SHUKRANI.
Pamoja Saana.
AshaDii.
P.S
Will really appreciate Lack of Uchakachuzi.