Usalama UDSM Wa Mashaka

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
213
Mimi sio mkazi wa eneo la Chuo kikuu cha Dar es salaam , lakini naishi pembeni mwa eneo hilo na muda mwingi sana nakuwa ndani ya eneo la UDSM kwa ajili ya shuguli zangu nyingi zinazonilazimu mimi kuwa katika eneo lile .

Kwa siku za karibuni kumetokea matukio zaidi ya 3 ambayo kwa kweli yanatishia usalama sio wa UDSM pekee bali hata ya majirani wa maeneo yale kama mimi binafsi .

Siku ya jumamosi mchana kama kawaida yangu nilielekea chuoni mchana , lakini kule njiani nilikutana na dimbwi la damu na kibanio cha nywele cha mwanamke , mbele kidogo nikaona chupa ya pombe imepasuka nikajua kuna jambo limetokea .

Ikabidi niende kituo cha polisi kuulizia kulikoni kama wana taarifa zozote za tukio lile , kutuo cha polisi hawajua hata kama kitu kama kile kimetokea ndani ya chuo kikuu tena karibu na kituo cha polisi si unajua polisi walivyo wakaidi ? wakaniomba nisiendelee kuuliza chochote kile .
…………………………………………………………………………………………..
Zamani kidogo niliwahi kupita usiku eneo hilo nikakutana na vijana wakanipa shilingi 500 wakaniambia niende kupanda dala dala nisipite kule kwa sababu kuna shuguli inaendelea ilikuwa zamani sana nilikuwa bado mdogo mdogo kumbe walikuwa wanafanya hivi ?

……………………………………………………………………………………………

Basi nikaanza kuulizia ulizia mambo huku mlimani usalama ukoje , nikaambiwa sasa imekuwa ni dili sana vibaka kibao ndani ya chuo na maeneo jirani na hakuna yeyote anayejali kuhusu suala hili kwanza nani atapambana nao wale askari wanaopita pita wote wazee wazee watapambanaje na wahalifu wanaokuja na kuondoka ?

……………………………………………………………………………………………

Wiki mbili zilizopita kuna kijana alikuwa anapita toka hall 5 kwenda hall 7 kupitia njia ya kanisani , alikuwa amebeba mkoba wake , alishangaa anaitwa anti alipogeuka tu kisu kikali kikakata mkoba wake na yule kijana akakimbia na ule mkoba ilikuwa saa 5 asubuhi yule dada alipiga kelele weee kila mtu akamshangaa utafikiri wanaangalia ze comedi .

Huyu dada alichunwa na kile kisu kilivyokuwa kikali , katika mkono wake kwahiyo akaendelea kukaa tu vile vile afanye nini mali yake ameshakwenda tena kinguvu ?

…………………………………………………………………………………………..
Sasa taarifa nilizosikia hivi karibuni ni kwamba vijana wa maeneo ya msewe ambayo mimi ni mwenyeji kidogo huko wamepanga kuweka mtego ili waweze kuwakamata watu hawa na kuwauwa kabisa na hili ni jambo la hatari sana kwa wananchi kuamua kuchukua hatua mkononi wanafanya hivi kwa sababu imani yao kwa walinda usalama wa eneo hilo wameshindwa kufanya kazi hiyo ya kuwapa wananchi usalama na uhuru wao sasa sijui itakuwaje ngoja tuone .

Watamchukuwa msichana mrembo wampe simu nzuri ya gharama na kumvalisha mambo mengine halafu awe na mazoea ya kupita pita maeneo yale waone nani atamsogelea au kwenda kujaribu kumpora ndio wafanye kazi yao hao wananchi wenye hasira .
 
Hapo sasa umenena sio kule unako beza watu wasizingumzie UFISADI eti kwa vile ni wapinzani.Hapo umenena itabidi tuhoji hapo UDSM usalama wa hapo chuo.
 
Shy
Habari inatisha sana hiyo, kwanza ninapinga kwa nguvu zooote raia kujichukulia sheria mkononi, pili ninawashutumu vikali jeshi la polisi kwa kujitia upofu wa matukio haya,
nakumbuka wakati fulani nilivunjiwa na majambazi halafu kama ujuavyo mie mtoto wa mjini niliwasaka mpaka nikawatia mkononi na kuwakabidhi polisi, kilichofuata ni kuyeyushwa na mpelelezi wa kesi hadi nikanyoosha mikono na kesi haikufika popote... polisi wakiamua lolote wanaweza, wakiamua kulea uhalifu huwa wanaulea kweli, wakiamua kuukabili wanajua how to combact, wanawajua vibaka majina mpaka rangi za mashuka wanayolalia.

Nadhani ifike mahala hawa dada zetu wakubali kuwa urembo au ulimbwende huja kwa mazoezi wala si kwa kujisiliba mikemikali, wajifunze mbinu za kujilinda ili hatimaye tuone jinsi wanavyoweza kuwatengua vizazi vibaka uchwara, pili jeshi la polisi lichukue nafasi yake ya dhamana kwa mali na usalama wetu, kingine ni utawla wa chuo kuweka taa ktk vichochoro vyake huku ikiimarisha ulinzi wa doria stukizi,

ila nakokludi kuwa labda hao polisi mbali ya kufaidika na ukabaji huo, labda pia wanashiriki kukaba au wanatoa mafunzo kwa wakabaji...
 
Shy,

Mambo ya vibaka na majambazi kuvamia wananchi wasio na hatia hayapo UDSM tu bali nchi nzima.Na sababu mojawapo inayochangia hali hii ni kukata tamaa na maisha kwa vijana wengi nchini mwetu.Serikali yao imewasahau,wazee hawataki kuachia madaraka,ufisadi unatukuzwa na kukumbatiwa na chama tawala,vigogo na watoto wao ndiyo wanaonekana kula vilivyo keki ya Taifa .Angalia tu jinsi watoto wa vigogo wanavyopewa kazi katika idara mbalimbali serikalini na hata kwenda kusoma nje hata kama hawana sifa zinazofaa.Kweli mimi sitashangaa kuona vijana wakigeuka majambazi na ndiyo maana kila siku tunapiga kelele na serikali ya CCM kuwekeza kwenye Taifa la baadaye na siyo kuleta usanii.

-Wembe
 
1. Pazungushiwe uzio chuo kizima.
2. Paanzishwe tozo (road toll) kwa kila gari linalopitia hapo chuoni (kwa wasio wafanyakazi wa UDSM).
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom