Usalama Jijini Dar

Kishazi

JF-Expert Member
Nov 14, 2007
491
250
Wadau mimi binafsi na ninaamini wakazi wengi wa jiji la Dar wanakerwa na vitendo vya kihalifu ambavyo vimekuwa kwa kasi kubwa. Watu wanakabwa na kunyang'anywa magari kama vile wizi wa simu; watu wanaumizwa na kuuawa kila siku; watu wanaibiwa kibabe hasa kwenye mataa ya ubungo kwa kung'olewa site mirrors kwenye magari yao bila msaada wa polisi; na miezi kadhaa watu walikuwa wanakabwa sana kwenye daraja la salender karibu kabisa na kituo cha polisi. Watu wanaogopa hata kwenda kwenye shughuli za kijamii wakihofia kukabwa au kuvamiwa magetini mwao wanaporudi.

Majambazi wana confidence ya ajabu, wanashika silaha na kuwaua wananchi bila kusikia lolote toka kwa kina Kova, Lukuvi na viongozi wengine. Waziri wa Mambo ya Ndani amekuwa kama picha tu, kwani hatumsikii hata kidogo hadi nasahau kama kuna hiyo wizara hapa nchini. Jeshi nalo linaongoza kwa kushirikiana na majambazi, watu wanavamiwa usiku, polisi wanapigiwa lakini response inajitokeza baada ya masaa mawili kwa kigezo cha kupotea njia.

Tunakwenda wapi jamani; watu tunaishi kama tuko kwenye nchi yenye vita..!! Wasiwasi tele, ukitembea barabarani huna amani, ukifika nyumbani kwako huna amani, utafikiri hatuna serikali. Kama kuna mdau anafahamiana na kina Kova na Mwema, awaambie wafanye kazi ya ziada kwani wimbi la ujambazi limezidi sasa.


Kuna mdau kaniarifu kuwa leo asubuhi kwenye Power Breakfast kuwa kuna familia imevamiwa na baba wa familia hiyo ameuawa kinyama na majambazi. Tumesikia mengi yakiwemo ya kina Prof. Mwaikusa. Sidhani kama kuna u-seriousness kwenye usalama wa raia.

Hali inatisha...!! Naomba kuwasilisha hoja wadau.
 

N-handsome

JF-Expert Member
Jan 23, 2008
2,374
1,500
Polisi wote njaa kali na wanashirikiana na vibaka na majambawazi, si mnamkumbuka yule polisi jambazi aliyejiua Kurasini?
 

Nyati

JF-Expert Member
Mar 6, 2009
2,331
2,000
NI HATARI KUBWA WAZEE. Nashukuru kwa kuianzisha hii kwa kweli watu hawa majambazi wamekuwa wengi sasa ama wanafanya kazi kwa njia za ajabu kabisa wanakufuata kwenye geti kutaka pesa ukikosa wanakufanyia.

Kwa sasa maeneo ya tabata na Segerea ndiyo wamepiga kambi kwa wiki hizi mbili. Walikuwa Kimara na Mbezi, Matukio mengi hayatangazwi lakini karibu kila siku mtu anavamiwa.

Waanga wanaeleza juu ya watu wenye ujuzi wa kushikiria silaha na wasio na masihara hata kidogo wanaua watu kama kuku vile.

Ushauri kwa sasa wakikuvamia kumbuka kuwa mpole angalau inaweza kukupa uwezekano wa kuendelea kuishi kwani POLISI wako Bize na uchaguzi na kura za maoni. Sijui kwanini wasikiri kushindwa ili RAIS aagize UWT waingilie hali ni ya hatari kwa sasa.

Kuhusu Ubungo nako kwachekesha, waweza poteza maisha kwa vijana wale wanaokimbilia Darajani wakisha fanya uhalifu wao. na hii inafahamika kwa askari wa kituo cha Ubungo lakini hakuna hatua zozote. Ndo maana akijitokeza mtu kama Mrema pamoja na mapungufu yake yote watu wanamuhabudu, kwani waliopo wameshindwa trivial things
 

Dick

JF-Expert Member
Feb 10, 2010
477
0
Usalama wa raia si kipaumbele chao, kipaumbele chao ni kuwafurahisha watawala. Kalagabaho!
 

Jethro

JF-Expert Member
Mar 23, 2009
2,221
1,225
Usalama wa Rai uko matatani karibibia mikoa mini
Mwanza ndio usiseme yaani kumeongezeka kupita zile enzi za kina nyamhanga 1980's
Huko Tabora nzega Uvamizi wa mabasi ndio kama kawa
Arusha ndio non stop crime zone ever in tanzania mpaka jumuhia za madola ziliisema Arusha ya tishia kwa ujambazi tena wasiraha za kutisha
Dar nako ndio sasa nako utazani ndio mvua ya majambazi inanyesha.
Kweli G. Hando wa kipindi cha PB-Clouds FM aliongelea swala la majambazi baaada ya tukio lililotoke juzi kwenye familia mmoja ambayo baba aliuwawa inavyonekana ni kama walitumwa kuwa pesa sijui anayo yule mzeee kumbe the same day morning marehemu ali deposite pesa bank.

Napenda uliza zile pikipiki za polisi a.k.a voda faster hazionekani kabisa mitaaani ni kwa nadra sana utakutana no na utashangaa kipindi cha chaguzi ndio mtaziona mijini zikizunguka sasa sielewi Kamanda Kova mwafanya nini na IGP Mwema na Masha kama waziri wa mambo ya ndani mbona hawa viongozi wetu hawana desturi ya kuvunja record ya kitu alichokifanya kwa wananchi wakawakumbuka??
 

Mundu

JF-Expert Member
Sep 26, 2008
2,708
2,000
Ningependa vibaka hawa wawaibie na kuwatesa kina Makamba, Lukuvi ili wajue jiji. Hovyo kabisa! Jamaa hawako serious hata kwa mambo ambayo waliyapokea na kujifunza bure toka kwa wakoloni. Yaani usalama wa Raia!!
 

RedDevil

JF-Expert Member
Apr 30, 2009
2,377
2,000
Kuna thread moja ilitolewa kuelezea jinsi ubalozi wa Autralia nchini kenya ulivyotoa tahadhali hali ya amani, siikumbi ni lini but it was last month watu tukabisha kweli lakini kumbe wenzetu ni majasusi yalishaona siku kibao. Kagakeshi alikana kuwa tanzania iko poa hakuna ujambazi.

Pili inshu ni maisha watu hawana pesa, viongozi wetu mafisadi wanajinemesha kila siku wakati kuna watu hata mulo wa siku ni bahati kuupata.
Wito wangu, kama tutafanikiwa kuvunja mwisho wa ccm, then fumua fumua lazima iwepo! watu wafanyishwe kazi, mashamba yapo! tufungue makarakana, mashamba makubwa, afisa kilimo wapelekwe kutoa shamba darasa hakuna tena njaa.

watu wafanye kazi siyo kupiga soga 24 hours, watakula wapi. saa nyingine ni project ya wakubwa kuua na kuiba.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom