Faana
JF-Expert Member
- Dec 12, 2011
- 31,814
- 33,178
Ndugu wanajamvi:
Katika pitapita yangu na mwenyeji wangu leo usiku huko mji kasoro bahari nimekutana na hali ambayo kikosi cha usalama barabarani hawatakiwi kusubiri tamko la Rais au Waziri ili kuongeza usalama kwa abiria wanaotumia barabara wakati wa usiku.
Daladala zinafanya safari usiku zikiwa na abiria lakini hazina taa, na zingine zina taa moja mbele, kiasi kwamba unapopishana nazo utadhani ni pikipiki, na zilizo nyingi hazina kabisa indicators wala taa za kuashiria gari linasimama,
Kwa jinsi nilivyoona, tatizo hili ni rahisi sana kulifuatilia ama kwa kufanya ukaguzi wakati mabasi husika yakiwa katika stand ya kupakilia abiria au kwa kuitisha ukaguzi kama ilivyo wakati wa kutoa stika za wiki ya usalama barabarani.
Nawasilisha