Usajiri ligi kuu Tanzania,Simba yaibomoa Yanga!!!

CHAI CHUNGU

JF-Expert Member
Feb 20, 2012
7,128
2,000
Ni kama record fulani hivi ya kuibomoa Yanga kisaikorojia.
Baada ya Yanga kumnyakua kipa wa zamani wa Simba Juma K Juma,Simba wao wamewasajiri makipa wawili wa zamani wa Yanga Yaw Berko na Ivo Mapunda ktk kukiimalisha kikosi chao.
Huku Berko akiwa na mkataba wa miezi6 Ivo kasaini mkataba wa miezi18 msimbazi wakati Juma K Juma akiwa amejifungia Yanga kwa miaka miwili.
 
Belo

JF-Expert Member
Jun 11, 2007
12,624
2,000
Simba wana matatizo makubwa kwenye kamati yao ya usajili kwa misimu 3 hakuna walichofanya.Angalia viwango vya Chuji,Yondani,Ngasa,Barthez hawa wote viwango vimezidi kuongezeka baada ya kujiunga Yanga.
 
Lupweko

JF-Expert Member
Mar 26, 2009
13,660
2,000
Simba wana matatizo makubwa kwenye kamati yao ya usajili kwa misimu 3 hakuna walichofanya.Angalia viwango vya Chuji,Yondani,Ngasa, Barthez hawa wote viwango vimezidi kuongezeka baada ya kujiunga Yanga.
Kweli kabisa, kiwango cha Barthez kimeongezeka sana, zile goli tatu ni bahati mbaya tu, na hata Juma Kaseja amesajiliwa tu hivyo hivyo, lakini atakuja kukaa benchi :becky::becky:
 
idawa

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
24,071
2,000
Sasa hapo Yanga imebolewa vipi?
Wakati hao wachezaji hayupo hata mmoja aliekua na mkataba na Yanga...
 
mwangalingimungu

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
1,292
2,000
Sure, acha Yanga tubomolewe, fujo tumeanza wenyewe.
Kwani Mapunda na Berko wamehamia Simba wakitokea Yanga? Inawezekana Yanga wamefanya fujo kwa kumnyaka JKJ akiwa mbioni kusajiliwa upya Simba. Lakini Simba wamempata Berko kivyao, wakati Yanga ikiwa hata haina tena mpango naye. Kama unahisi fujo wameanza Yanga, sawa. Lakini kwa hili Simba hawajafanya fujo yoyote.
 
Makoye Matale

JF-Expert Member
May 2, 2011
6,491

Mkuu hivi ni vijimambo vya watani! Nd'o utani wenyewe.
 
mwangalingimungu

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
1,292
2,000
Mkuu hivi ni vijimambo vya watani! Nd'o utani wenyewe.
Sawa, lakini wapenzi wa Yanga utani wao haufiki Tambuka Relini! Wamefungwa vibao vitano tu na Mnyama wakatoka uwanjani huku wakiwavurumishia mitusi wachezaji wao wenyewe, seuze mimi na wewe! Chunga nao sana!
 
FaizaFoxy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
71,278
2,000
Ni kama record fulani hivi ya kuibomoa Yanga kisaikorojia.
Baada ya Yanga kumnyakua kipa wa zamani wa Simba Juma K Juma,Simba wao wamewasajiri makipa wawili wa zamani wa Yanga Yaw Berko na Ivo Mapunda ktk kukiimalisha kikosi chao.
Huku Berko akiwa na mkataba wa miezi6 Ivo kasaini mkataba wa miezi18 msimbazi wakati Juma K Juma akiwa amejifungia Yanga kwa miaka miwili.

Huoni hata haya kuiharibu lugha yetu tamu ya Taifa namna hii?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom