Usajili wa wachezaji wa kibongo na mikataba ya miaka miwili.

mr vata

JF-Expert Member
Jan 30, 2017
418
500
Sijui imekua ni fashion au vp...
Sijui wachezaji hawaaminiki kwamba watakua na ubora ule ule kwa muda mrefu au vp...
Hili suala linanikanganya kwa kweli. Kwa nini hatuoni mikataba mirefu ya wachezaji zaidi ya miaka miwili hapa tanzania?
Unakuta timu inasajili mchezaji ana miaka 20-24 lkn bado anampa mkataba wa miaka miwili, kwa nini?
Halafu ugonjwa mwingine kwenye soka letu ni kuacha wachezaji muhimu wanalize mikataba...
Hivi inakuaje mtu kama Shomari Kapombe, au Ibrahimu Ajibu, au Aishi Manula wakaachwa mpaka wakamaliza mikataba na kuondoka bure? Wachezaji tegemeo kwenye timu wanaondoka bure! Inaonekana tanzania soka si biashara ni burudani tu. Kwa mtindo huu tutafika wapi? Soka letu limejaa ubabaishaji.
 
Marlex Jr El

JF-Expert Member
Nov 6, 2015
1,794
2,000
Na mi hii kitu imeacha domo langu wazi miaka miwili kama unamsajili mzee wa miaka 33/34
 
Joseverest

Verified Member
Sep 25, 2013
44,074
2,000
Ni utaratibu waliojiwekea mkuu....wanapima uwezo wako..wakiona umeshuka kiwango wanakupiga chini si unajua bongo soka tena
 
Kyawanjubu

JF-Expert Member
May 13, 2017
2,387
2,000
Wachezaji wa kigongo hawajitambui hasa akishacheza zile timu 2 za Kariakoo timu zinaogopa kumpa mkataba mrefu maana hawezi dumu kwenye kiwango kwa muda mrefu kwa mfano kuna dogo anaitwa Hamad juma alikuja simba toka Tanga alicheza mechi 2 za mwanzo wa ligi ndo mazima unaambiwa anapenda tungi balaa kuna kipindi alidai kuanguka bafuni akavunjika mkono kumbe alikua tungi akaanguka kwenye ngazi mwingine ni Mkude baada ya kusaini miaka 2 kipindi kile alipewa ml 50 na Gx 110 alianza ulevi wa. Kupindukia msimu huu ndo karudisha kiwango ili watu watoe dau afu arudie tabia zake
 
Gne gner

JF-Expert Member
Nov 24, 2016
504
500
Sijui imekua ni fashion au vp...
Sijui wachezaji hawaaminiki kwamba watakua na ubora ule ule kwa muda mrefu au vp...
Hili suala linanikanganya kwa kweli. Kwa nini hatuoni mikataba mirefu ya wachezaji zaidi ya miaka miwili hapa tanzania?
Unakuta timu inasajili mchezaji ana miaka 20-24 lkn bado anampa mkataba wa miaka miwili, kwa nini?
Halafu ugonjwa mwingine kwenye soka letu ni kuacha wachezaji muhimu wanalize mikataba...
Hivi inakuaje mtu kama Shomari Kapombe, au Ibrahimu Ajibu, au Aishi Manula wakaachwa mpaka wakamaliza mikataba na kuondoka bure? Wachezaji tegemeo kwenye timu wanaondoka bure! Inaonekana tanzania soka si biashara ni burudani tu. Kwa mtindo huu tutafika wapi? Soka letu limejaa ubabaishaji.
Alafu wakisha maliza mikataba yao,,wanaangaika kuwasainisha tena.,,watu hawalali kila siku kwenye majumba ya wachezaji kutaka saini...
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom