Usajili wa timu zetu ni kwa lengo la kuziimalisha au tunataka sifa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Usajili wa timu zetu ni kwa lengo la kuziimalisha au tunataka sifa?

Discussion in 'Sports' started by Miwatamu, Oct 11, 2012.

 1. Miwatamu

  Miwatamu JF-Expert Member

  #1
  Oct 11, 2012
  Joined: Oct 2, 2012
  Messages: 1,453
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 133
  Tangu msimu wa usajili ulipoanza kwa timu zetu hapa nchini hasa za Yanga, Simba na Azam, yalisemwa mengi na wengine hata kufikia hatua za kujiapiza na kuwekeana dau kana kwamba wao ndio wanaoingia dimbani na kusababisha ushindi kwa timu husika.

  Binafsi nimekuwa mpenzi wa timu ya Yanga kwa kipindi cha muda mrefu, hasa mara baada ya timu ya Pan African kusambalatika, ambayo naamini kuwa ni timu pekee iliyokuwa ikinipa burudani ya kandanda safi kuliko timu nyiingine yeyote hapa nchini.

  Katika siku za hivi karibuni kumetokea biashara kichaa ya timu au wafadhili wao kutumia fedha nyingi kupita uwezo wa mapato yake kwa kusajili wachezaji wenye majina makubwa ambao pamoja na sifa zao hata wanapojiunga na timu husika hujikuta wakicheza mpira uliochini ya kiwango kana kwamba wametokea mchangani!

  Swali langu kwenu washika dau, hivi kweli tunatumia nguvu na pesa nyingi kiasi hiki kwa ajili ya kubadili soka la nchi hii, au ni kutaka kuonesha kuwa tunazo pesa za kununua mtu yeyote kama vile tunavowanunua wapiga kura wakati wa kampeni za kisiasa kwa lengo la kumpaisha mtoaji pesa bila kujali nini kinachoendelea hapo baadaye?!

  Nimeamua kuandika thread hii baada ya kuangalia kiwango cha mchezo ambao umekuwa ukioneshwa na timu ya Yanga ambacho hakilingani na kiasi cha pesa zilizotumika katika uundaji wa timu hii, na haswa baada ya kuangalia mechi iliyomalizika muda kitambo kati yake na Toto African ambao ulikuwa mbovu mno. Je, washika dau mnasemaje katika hili?
  Ni bora turejee katika soka letu la ridhaa au bora liende tu?.
   
 2. M

  Mkandara Verified User

  #2
  Oct 11, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Swala la Mpira linaanza toka maandalizi ya vijana wetu iwe mpira wa mchangani, mashuleni hadi Taifa. Maadam Mpira sasa hivi ni Biashara kitakachotazamwa ni soko tu..Inawezekana wewe ndiye hufahanmu faida zake lakini wanaowekeza fedha zao ndio wanajua manufaa ya manunuzi hayo. Kama tunaweza kununua mali feki kutoka China, unaona maajabu gani kuleta wachezaji feki vilevile.. Ebu fikria hili Tanzania haina mchezaji hata mmoja Ulaya anayechezea daraja la kwanza sasa tunategemea kuwa na kiwango gani cha mchezo huu..
   
 3. o

  obwato JF-Expert Member

  #3
  Oct 11, 2012
  Joined: Sep 7, 2012
  Messages: 1,189
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Hoja yako ina mashiko lkn hapa si mahala pake. Any way nachangia kidogo. Baadhi yao wana mchango kwa timu husika, karibu wachezaji wa kigeni wa Yanga wote ni muhimu na wana uwezo kuliko wazawa wanaocheza namba zao japo hakuna ubishi kuwa Mbuyi Twite hakusajiriwa kwa umuhimu au ubora wake bali ni kumkomoa Rage, kwa Simba Okwi ni exceptional lkn Akufor, Sunzu, Keita nayule mkenya ni wazuri but hawatofautiani sana na wazawa wanaogombania nao namba.
   
 4. Miwatamu

  Miwatamu JF-Expert Member

  #4
  Oct 11, 2012
  Joined: Oct 2, 2012
  Messages: 1,453
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 133
  Obwato; Kwa kiasi fulani umeeleza mchango mzuri katika hili.
   
 5. grafani11

  grafani11 JF-Expert Member

  #5
  Oct 12, 2012
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 15,534
  Likes Received: 342
  Trophy Points: 180
  Mkuu kwa kuwa umewataja sana Yanga ngoja tuwasubiri watuambie ni kwanini kila mwaka wanasajili halafu nguo za wachezaji wao wanaandika Rage, je wanasajili kwa ajili ya kuendeleza kikosi chao au kuikomoa Simba SC, kama ni hivyo mbona Simba SC haitetereki wanaotetereka ni Yanga, hawajifunzi tu?
  Twende kazi....
   
 6. grafani11

  grafani11 JF-Expert Member

  #6
  Oct 12, 2012
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 15,534
  Likes Received: 342
  Trophy Points: 180
  Obwato wewe unataka hoja hii ipelekwe jukwaa gani?
   
 7. Miwatamu

  Miwatamu JF-Expert Member

  #7
  Oct 12, 2012
  Joined: Oct 2, 2012
  Messages: 1,453
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 133
  Na ndiyo maana nimeamua kuleta thread hii kwenu ili tupate jibu muafaka kwani inaonekana usajili tunaoufanya ni kwa ajili ya kumuonesha mwingine nani zaidi na wala si kwa lengo la kuleta mabadiliko katika soka letu. Bado nahitaji kupata jibu toka kwako.
   
 8. grafani11

  grafani11 JF-Expert Member

  #8
  Oct 12, 2012
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 15,534
  Likes Received: 342
  Trophy Points: 180
  Ni ulimbukeni wa baadhi ya wajumbe wa kamati za usajili za timu husika mfano Yanga kutaka kuonesha nguvu ya pesa chafu waliyonayo, kama ingekuwa kwenye muziki tungewaita mapedeshee wanaohonga hela ndefu kwenye shoo ili wapate sifa wakati baadhi tunawajua wanaishi nyumba za kupanga na watoto wao wanaishi kwa dhiki.

  Matokeo yake wanahusika pia kumlazimisha kocha kupanga watu waliowasajili wacheze hata kama hawana viwango ili kulinda heshima zao.
   
 9. B

  Baba Kiki JF-Expert Member

  #9
  Oct 12, 2012
  Joined: May 31, 2012
  Messages: 1,368
  Likes Received: 489
  Trophy Points: 180
  Kuna tofauti kubwa sana kati ya kusajili wachezaji wazuri na kutengeneza timu nzuri. Wewe unachozungumzia ni kwamba mchezo uliooneshwa na Yanga jana haulingani na kiasi cha pesa kilichotumika.

  Bila kutafuna maneno, naweza kukuhakikishia Yanga itendelea kucheza mchezo wa aina hiyo kwa muda mrefu kwa sababu zifuatazo; -

  1. Yanga inabadilisha zaidi ya wachezaji 5 wa kikosi cha kwanza kila msimu kwa zaidi ya miaka mitano mfululizo
  2. Yanga haijabahatika kukaa na kocha mmoja kwa misimu miwili ili aweze kugundua mapungufu ya timu ktk msimu mmoja na kurekebisha msimu mwingine
  3. Usajili unafanyika kisiasa, kwa shinikizo la viongozi wasiojua mahitaji ya kiufundi ya timu.
  4. Shinikizo kubwa la kushinda kutoka washabiki bila kujali uwezo halisi wa timu na mipango ya muda mrefu ya kiufundi ya timu. Hapa nina maana shinikizo likiwa kubwa sana linasababisha watu kulazimisha ushindi
  5. Kutokuwa na timu nzuri za vijana, hivyo kukosa watu waliokulia ktk klabu hiyo wenye kuweza kuujua zaidi utamaduni wa mpira wa klabu
  6. (Joke) Huo ndio huwa mpira wa Yanga. Pasi ndefu, mbio nyingi, matumizi ya nguvu.
   
Loading...