Usajili wa simu zilizotumika kabla ya kuuzwa

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
13,108
18,326
Kuna umuhimu mkubwa sana TCRA kuweka utaratibu wa wananchi kusajili simu zao zilizotumika ili ziende sokoni kwa mauzo.

Hili ni kutokana na kwamba soko la simu zikizo tumika lina changamoto nyingi sana kwa sababu wengi wana amini zimeibiwa.

Utaratibu kama huu utawezesha hata kuwa na maduka maalum ya simu zilizo tumika baada ya kupewa usajili na TCRA.

Kwa hiyo mtu akitaka kuuza simu yake atatakiwa kuonana na kitengo husika cha TCRA, ana sajili kama mmiliki halali na kisha kupeleka sokoni kwa mauzo.

Kwa namna hii serikali itapata fedha pia kwa tozo ndogo zitakazo kuwepo.

Naleta hoja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani mtu atoke nanjilinji ndani ndani kule aende wilayani kusajiri simu afu arudi kumtafuta jamaa aliyefika bei, huyo mtu atakuwa bado anamsubiri tu?

Simu kama ni yako lazima utakuwa na vielelzo vya manunuzi ikiwemo list ambayo hasa ndo ya muhimu na ndo itathibitisha simu ni mali yako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Muuzaji uwe na risiti yako uliyonunulia mkononi wakati unauza nadhani inatosha.

Hata kama ni Mtu wa tatu ilimradi kuna risiti ya mnunuzi wa awali.

Labda tu kuwe na utaratibu wa Simu ikiripotiwa imeibiwa basi iwe black listed, kuwepo namba ambayo Mununuzi ataweza kupiga ku confirm kwamba simu haina tatizo ndio alipe.
 
Siku lazima mtu aende wilayani ila inaweza kuwa ni online.

Hii ji muhimu sana kwa watu wenye simu kali.. sizungumzii simu ya elfu hamsini.

Hii itasaidia kuwa na soko zuri la simu zilizo tumika na kuzuia simu za wizi.

Leo hii ukiuziwa simu hujui kama ni ya wizi au ni ya umiliki halali?

Wengi wamenujua lakini baada ya siku 3 unaapigiwa simu na polisi eti simu ji ya wizi.
Muuzaji uwe na risiti yako uliyonunulia mkononi wakati unauza nadhani inatosha.

Hata kama ni Mtu wa tatu ilimradi kuna risiti ya mnunuzi wa awali.

Labda tu kuwe na utaratibu wa Simu ikiripotiwa imeibiwa basi iwe black listed, kuwepo namba ambayo Mununuzi ataweza kupiga ku confirm kwamba simu haina tatizo ndio alipe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna umuhimu mkubwa sana TCRA kuweka utaratibu wa wananchi kusajili simu zao zilizotumika ili ziende sokoni kwa mauzo.

Hili ni kutokana na kwamba soko la simu zikizo tumika lina changamoto nyingi sana kwa sababu wengi wana amini zimeibiwa.

Utaratibu kama huu utawezesha hata kuwa na maduka maalum ya simu zilizo tumika baada ya kupewa usajili na TCRA.

Kwa hiyo mtu akitaka kuuza simu yake atatakiwa kuonana na kitengo husika cha TCRA, ana sajili kama mmiliki halali na kisha kupeleka sokoni kwa mauzo.

Kwa namna hii serikali itapata fedha pia kwa tozo ndogo zitakazo kuwepo.

Naleta hoja.

Sent using Jamii Forums mobile app
kwani simu zinasajiliwa au laini?
kwahiyo unataka uuze laini yako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom