Shoctopus
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 3,434
- 1,985
Nakumbuka niliponunua line ya Airtel mara ya mwisho nilipigwa picha kwa usajili.
Sasa nasikia hii haitoshi, lazima nisajili tena kwa kidole.
Wamesema kutosajili kwa kidole ni kosa (la jinai). Adhabu yake ni faini ya shilingi milioni au kifungo jela miezi sita au vyote!
Ajabu hapa ni kwamba wahusika sio kwamba hawanijui kwa majina yangu, umri na sura au kama hawanijui labda kwa kidole changu tu, sio sura nk! Kwasababu kidole peke yake bila jina, sura, umri kinatosha?
Yaani kwa wahusika kukosa alama ya kidole changu ninastahili kwenda jela?
Hamjasikia mtu amezaliwa bila mikono. Sasa huyo mtamsweka jela kwa kukosa alama ya kidole au simu kwake ni marufuku?
Hivi tumewakoseeni nini hadi kustahili manyanyaso usiku na mchana mwaka mzima?
Tunawezaje kuishi kwa amani na furaha kama mnatutesa kwa kutunyima haki zetu kwakuwa tumeshazeeka, halafu tuishi kwa vitisho kwa kutosajili simu kwa kidole tu?
Sisi ndio tumekula matrilioni ya fedha za nchi au tumegeuka watuhumiwa wa ugaidi?
Kuna watu wanapenda kutuchonganisha na Serikali bila sababu za msingi.
Hakuna mtu mwenye akili timamu atapinga zoezi la kusajili kwa kidole. Ila kila mtu ana sababu zake kutokamilisha usajili, baadhi ya hizo sababu wahusika wanazijua. Hii mambo ya deadline na vitisho ili iweje?
Kila siku watu wananunua simu na huwezi kusema mwisho wa kununua simu ni December 31, baada ya hapo hamtasajili simu kwa vidole?