Usajili wa Simba na Yanga na faida kwa ligi ya Tanzania

muda wa ukombozi

Senior Member
Jun 28, 2013
127
116
Kuna vitu vinaendelea kuhusu usajili ambao tff wameachia dirisha hilo kuanzia 1/07/2022 hadi 30/08/2022 ambapo tunashuhudia mambo kipindi hiki.

Timu ya Yanga Afrika ilichagizwa na uchaguzi, ambapo kipindi ya kampeni kuelekea uchaguzi huo wagombea waliaidi mambo mengi kwa maendeleo ya klabu, mgombea wa uraisi Eng. Hersi aliahidi makubwa ikiwemo kujenga uwanja, lakini kufanya usajili mkubwa kwa msimu unaokuja.

Ambapo tayari Yanga washaanza kuleta wachezaji hao Gael Bigirimana ambaye miaka 10 iliyopita alikuwa ligi kuu ya uingereza, lakini pia wanamtaja Aziz ki ambaye kashawahi kucheza ligi ya hispania.

Simba nao wanahusishwa na kumrudisha Luis Miquison mchezaji wao wa zamani, ambaye amecheza mashindano makubwa ya kombe la dunia kwa vilabu.

Kwenye hili mi naona tayari kwa Afrika tushafika hatua ambayo wachezaji wakubwa wanaanza kupata tamaa ya kuja kucheza ligi ya Tanzania.

Hii itasaidia kujitangaza kwa ligi zetu ambapo tunaweza kupata wadhamini wakubwa ambao wanaweza kuingia kwenye ushindani na Azam.
 
Mlimnukuu vibaya Eng. Hersi, maana aliahidi kuja na kampeni ya kuhamasisha wanachama wachangie kujenga uwanja, na sio kwamba ni pesa inayotoka mfukoni mwake binafsi.

Na kwenye swala la michango wote tunawajua wamnanchi walivyo, huko nyuma kampeni nyingi za namna hiyo zilizo husisha uchangishaji zilikufa kifo cha taratibu na ndio ukawa mwisho wa zoezi la uchangishaji.

Hersi ana amini lile nyomi la kupokea kombe akili dilute in term of mchango ana uhakika wa kujenga uwanja huo anaoufikiria kichwani mwake kitu ambacho sio kweli.
 
Mleta mada anaongelea usajili wa Simba na Yanga na maendeleo ya Soka la Tanzania,wewe unaleta upupu wa Uwanja wa Yanga. Kweli Engineer Hersi kawashika pabaya Makolo.
 
Mleta mada anaongelea usajili wa Simba na Yanga na maendeleo ya Soka la Tanzania,wewe unaleta upupu wa Uwanja wa Yanga. Kweli Engineer Hersi kawashika pabaya Makolo.
Kwani nimeongelea habari za CCM na CHEDAM hapo?

Mbona nami hoja yangu ya uwanja ni sehemu ya maendeleo ya soka?
 
Msimu ujao utakuwa mtamu sana. Hata Azam Fc nao wanajitahidi kufanya usajili wa maana. Wakisajili na mlinda mlango wa kiwango cha juu, basi watatisha.
 
Back
Top Bottom