Usajili wa namba za simu kutumia alama za vidole ni kwa sababu zipi?

Utaratibu wa finger print haupo tanzania tu. Hata india, Nepal na Nchi nyingine za Asia nikiwa sina uhakika sana na china wanatumia huu mfumo. Finger print ina faida nyingi sana ikiwemo kuongeza usalama na mengine mengi. Cha muhimu na cha kuzingatia ni kwamba mfumo huo hautodhuru mtu yoyote na wala hauna hasara yoyote ile.

Nahisi serikali inataka kudhibiti ulipaji wa kodi wa makampuni ya simu kwa kujua idadi ya watu wanaotumia mtandao husika. Au labda nchi inajaribu kucop na maendeleo ya sayansi na tecnolojia maana nchi za wenzetu zimeanza huo mfumo mda sana.
Kuhusu swala la kodi ndo Maana wanachukua alama za vidole napingana na ww sio kweli.kuna njia tofauti wanaweza kufanya kuliko kuwapangisha watu foleni
 
Mlimani city ni kwa wateja wa vodacom tu. Sasa we unatumia tigo au halotel nenda mlimani city kasindikize wenzako.
2915fb33dbcf6ce8e0ac3ff5962055e5.jpg



Acha kupotosha watu mzee
 
Mimi najua nimesajiliwa na jina langu ni lile lile, hata nikipiga *106# naambiwa usajili wangu umekalimika wananitajia na jina langu kabisa sina shida, foleni niliyokaaga wakat wa kusajili simu na muda nilioupoteza siku tatu nzima unatosha sana, hizo fingerprint wataweka za kwao, tusikae tunayumbishwa yumbishwa, kwani nchi wanazotumia finger print hamna wizi wa kimtandao? Watu vyuma havijakaza tunapambana na hali zetu tuanze kupangishwa foleni tena kah!
 
Alama za vidole yaani finger print, usajili wa line unahitaji finger print kama sahihi ya mmiliki wa line kwani kila mtu ana fingerbprint yake isiyofanana na ya yeyote mwingine, na inasaidia hasa inapotokea shida inayohusiana na uhalifu wa kupitia mtandaoni
 
Nyambaf, tumia akili wewe. Unalink vitu visivyofanana.
Una-link utambulisho wa mtu sio vitambulisho, fingerprint ni unique hata ichukuliwe na taasisi 101 itabaki ileile

By the way, kutukana ni upuuzi na beware baada ya hili zoezi hii tabia ya kutukana kiholela itakutokea puani
 
Back
Top Bottom