Usajili wa magari ya Serikali umefikia namba STL, magari binafsi mbona yamekaa sana namba D?

Kwenye utaratibu wa ku-namba magari herufi I na O haziwekwi kwa sababu zinafanana na 1(moja) na 0(sifuri) hivyo wanaondoa confusion.
Kwa sasa tupo DQ mbona sion DO ililukwa au kuna technical ishu hapa tujuzeni wadau hapa
 
  • Thanks
Reactions: cmp
We jamaa hivipunde umenichekesha.
Ipo hivi, hayo magari ya serikali si kwamba yamefika usajili wa STL bali ni hivi
STL _secta na taasisi za lazima
STK_Sekta na taasisi za kiserikali
DFP_ Donor funded projects
SU_Shirika la umma
SM_serikali za mitaaa
N.k
STL?? No way....
 
Uko sahihi.... Ilianza ST (Serikali ya Tanzania) then STA, B, C, D etc
Umepotosha kwenye STL na STK, ST naamini zilianzia A mimi nimeanza kujitambua nimekuta kwenye STG,zikaja STH, STJ, STK then STL,
 
  • Thanks
Reactions: cmp
DAA
Hapo kwenye A ya kwanza lazima magari yafikie 9999 ndiyo no ishift kuwa DAB
Kwenye B lazima magari yafikie 9999 ndiyo ishift kuea DAC mfano gari yangu ni DDW 275 mpaka ilipo hapo ilihitaji mgari mengi sana yasajiliwe...ndiyo maana sasa hivi nafikiri tupo kwenye DM....
Hujamuelewa.... Mfano namba D iliyopo sasa inabidi isajili magari 9999 baada ya hapo hiyo D itakuwa imejaa wsnahamia E...
Usimlishe maneno, hajamaanisha D nzima ndo 9999, bali DAA 9999, DAB 9999, DAC 9999. Namba zetu hata 1,000 hazifiki, sembuse 9,999?? Nimekuwekea hapo juu maneno yake uyasome tena
 
  • Thanks
Reactions: cmp
Ulishawahi kumuona mtu aliyevamia swali na kujifanya anajua sanaaaaaa,full masifa halafu akaanza kushuka swali hilo kwa mbwembwe lakini bahati mbaya hajui chochote na anashuka pumbaaaaaaa

Basi watu hao wana sifa km zako mkuu.Hv we hayo magari ya serikali umeanza kuyaona leo au?mpaka kutletea hizo tafsiri za uongo za STK na STL??

Dah aisee halafu unakazia eti "Sekta na Taasisi za Lazima" we jamaa ww komaa kutudanganya wakubwa zako.
Hizo maana yake nini mkuu, Mm zinanishindaga sana
 
Mkuu STI sijaiona umesahau au haikuwepo?
Mkuu mi hiyo kwa kweli sikuwahi kuiona aisee hizo nilizoziorodhesha nimezishuhudia kwa macho yangu na hiyo STA mzee aliomba kuuziwa ilikuwa kwenye taasisi aliyokuwa akifanya kazi ilikuwa landrover 109 miaka mingi iliyopita.
 
Back
Top Bottom