Usajili wa magari kufanyika mara mbili kwa mwaka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Usajili wa magari kufanyika mara mbili kwa mwaka

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Oct 5, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Oct 5, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,572
  Likes Received: 82,100
  Trophy Points: 280
  Usajili wa magari kufanyika mara mbili kwa mwaka
  Halima Mlacha
  Daily News; Sunday,October 05, 2008 @20:04

  KAMANDA wa Kikosi cha Usalama Barabarani, James Kombe, amesema katika kutatua tatizo la msongamano wa magari barabarani, usajili wa magari makubwa sasa utafanyika mara mbili kwa mwaka.

  Pia amesema wanaandaa utaratibu wa kupiga marufuku kuingizwa kwa magari yote yenye umri wa miaka mitano nchini.

  Akizungumza mwishoni mwa wiki katika mkutano wa waandishi wa habari Dar es Salaam, Kamanda Kombe alisema imebainika kuwa moja ya sababu kubwa inayosababisha msongamano wa magari barabarani ni kuwapo kwa magari mengi mabovu.

  "Tunafahamu kuwa msongamano wa magari ni kero kubwa hasa katika majiji kama Dar es Salaam, ndio maana safari hii tumepanga registration ya magari makubwa itafanyika mara mbili kwa mwaka na itafanyika kwa kompyuta kama gari ni bovu litafutiwa leseni," alisema Kombe.

  Alisema pamoja na magari hayo makubwa pia magari madogo nayo yatafanyiwa usajili na kukaguliwa mara tatu kwa mwaka na iwapo litakuwa na umri wa miaka mitano halitaruhusiwa.
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Oct 5, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,572
  Likes Received: 82,100
  Trophy Points: 280
  Haya ya kutoruhusu magari yenye zaidi ya miaka mitano kuingizwa nchini na pia kutoyapa leseni magari yenye zaidi ya miaka mitano ambayo tayari yako barabarani nimeanza kuyasikia tangu 2005, tunakaribia 2009 bado yanazungumzwa tu!!! utekelezaji ni ZERO!!!!
   
 3. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #3
  Oct 5, 2008
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Vipi zile show room za kila kona Dar, najua magari mengine ni karibia 20 yrs old.....watayafanya scrappers?
   
 4. K

  Kithuku JF-Expert Member

  #4
  Oct 5, 2008
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Utekelezaji wa kitu kama hiki hatuutaki kabisa maana utatuzidishia umaskini. Yaani ati gari la miaka mitano lisisajiliwe? Huo uwezo wa kununua magari mapya bongo nani anao? Na kitu kinachosababishia gari ubovu ni umri wa gari au ni utunzaji? Mbona mimi nina gari la mwaka 1990 na linafanya kazi vizuri sana halina ubovu wowote? Hawa watu sasa wanataka mafisadi tu ndio waendeshe magari barabarani! Kwa hiyo mimi ambaye nimetunza Nissan yangu kwa makini (ambayo pia nilinunua mtumba 10 years ago), ati nipewe adhabu kwa kunyimwa leseni, ili nirudi kwenye daladala? Nilidhani polisi wana akili na busara ya kutosha ya kuzingatia vigezo vingine vya ubora wa gari badala ya umri pekee, kumbe nao ni vihiyo? Mbona kuna magari yana miaka miwili tu barabarani lakini yameshakuwa mabovu na yanasababisha ajali? Hata James Kombe ambaye nilidhani ana akili analeta proposal ya ajabu namna hii, kweli nimeshangaa sana! Hii ya kuzingatia umri wa gari kama kigezo cha ubora, hata Ulaya ambako ndiko tunakoiga mambo mengi hakuna hii, wao wana utaratibu wa grading wenye vigezo vingi ambavyo ni mechanical, na sio tarakimu ya mwaka lilipotengenezwa gari. Hapa niliko nina rafiki ambae majuzi kanunua kwenye auction Landrover ya mwaka 1971 (ex-military), ni nzima na nzuri mno, na anatamba nayo kweli anasema amekuwa akiota kumiliki gari kama hiyo tangu akiwa mtoto maana alikuwa anaiona kwenye sinema (niligundua baadae kuwa huo pia ndio mwaka aliozaliwa). Sasa sisi tunakatazwa mali adimu kama hizo tusiwe nazo! Kwa hiyo sasa bwana Kombe anataka "mkweche" wangu nikauuze kama skrepa? Kwa hili bwana Kombe hatukubaliani kabisa, hili tutafikishana mbali wallahi! Mnataka magari wabaki nayo mafisadi tu wanaomudu yale yasizidi miaka mitano! Hapatatosha naapa!
   
 5. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #5
  Oct 6, 2008
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Kithuku,
  Umegusa penyewe hapo. Kama ni magari chakavu basi waweke standards ambazo kila gari linaweza kupimwa. Mimi nina mkweche wangu 1987 BMW lakini kila mwaka linapita inspection na kitu wanachoangalia hapa Marekani ni safety--wanakagua breki, taa, na kuona kuwa halitoi moshi wa kuchafua hewa (catalytic converter) Mbali ya hapo ni mwendo mdundo tu. Na kwa teknolojia ya siku hizi gari la miaka mitano kurudi chini bado ni jipya kabisa, na ni Watanzania wangapi wataweza kumudu magari ghali aina hii? Wanataka tuwaachie wao mafisadi barabara wapite na Lexus zao na Range Rover wakitutimulia vumbi na carbon dioxide.
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Oct 6, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,572
  Likes Received: 82,100
  Trophy Points: 280
  Unachosema ni kweli kabisa kwamba kuna wengine wanayapigiza vibaya magari yao na kuongeza uchakavu na mwingine unaweza kumkuta ana gari lina miaka 20 lakini bado liko order ile mbaya. Mimi nina mkweche wangu una miaka 12 sasa lakini wengi huwa hawakubali na kudhani lina miaka miwili au mitatu. Nalipepeka service kila linapohitajika kwenda service, nalipiga polish ndani na nje mara moja kwa mwaka, ukiliona linaonekana mma kabisa. Labda uamuzi wa kutolipa gari leseni uwe ni ubovu wa gari hilo na labda linatoa hewa chafu kwa kiasi kikubwa kuliko inavyostahili, vinginevyo miaka mitano si muda halali wa kutoliruhusu gari kuwa barabarani.
   
 7. O

  Ogah JF-Expert Member

  #7
  Oct 6, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Hivi huyu James Kombe elimu yake (speciality) ni ipi............maana mambo anayozungumza mmmmhhh
   
 8. M

  Moelex23 JF-Expert Member

  #8
  Oct 6, 2008
  Joined: Oct 8, 2006
  Messages: 497
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  sorry, kwani traffic polisi anaweza kupanga policy nchi yetu hii?? Wizara ya fedha si ndio ina haya mamlaka au??

  Naona since mkuu wa Kaya hakai Dar, basi kila mtu anadhani anaweza kupanga vitu anavyovitaka binafsi.

  Hii ni non starter and can not be implemented!!!

  Anajua Bajeti ya nchi inategemea kodi hizo za ushuru wa magari au?? Insurance companies nazo si zitacollapse au???

  Kombe tulia na shughulika na mambo yaliyo chini ya idara yako, this is above ur pay grade homie!!!
   
 9. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #9
  Oct 6, 2008
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Nimesoma habari hii katika moja ya magazeti ya kila siku na kupata mshangao mkubwa na kauli ya Kamanda Kombe.

  Tatizo la msongamano wa magari katika jiji kongwe la Dar es Salaam linatakiwa liongelewe kwa kuangalia tafiti zilizokwishafanywa juu ya msongamano wa magari. Endapo kila mtu mwenye mamlaka ya kusema juu ya msongamano akijisemea la kwake matokeo yake ni vurugu zisizohitajika kwa wakazi. Ni vema Kamanda Kombe angebainisha vyanzo vyote vilivivyoanishwa katika tafiti zinazohusu msongamano wa magari hapo Dar.

  Lakini hili jambo la kukurupuka, kesho tutasikia Wizara husika ya miundombinu inakuja na version yake, Jiji na version yake, Regional Adm na version yake, Sumatra halikadhalika.

  Kwa hii amri ya Polisi aliyoitoa Kamanda Kombe, nadhani ni wake up call kwa serikali kutoa kauli ya pamoja ya 'wakubwa' wote badala ya kusubiri mambo yakiharibika iwe ni issue ya kisiasa ya kumtaka Rais aingilie kati.

  MTAZAMO WANGU:
  Tatizo kubwa la msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam ni ukosefu wa barabara za kutosha. Nilitegemea kamanda Kombe angetueleza

  Jiji la Dar es Salaam lina magari mangapi yanayotembea kila siku?

  Je, ni magari mangapi ambayo yanaingia Jijini kila siku?

  Je, ni kilometa ngapi za barabara za jiji la Dar es Salaam ambazo zinapitikia walau bila ya matatizo?

  Je, ni kilometa ngapi zinazohitajika kwa matumizi ya wakazi wa Jiji?

  Je, ndani ya miaka mitano hii, ni barabara ngapi mpya zimejengwa katika jiji la Dar? (Siongelei ukarabati wa Kilwa Rd, Shekilango Rd au Sam Nujoma Rd).

  Je, Kamanda Kombe ana taarifa zozote za kitafiti zinazoonesha kuwa wananchi wa kawaida (kama vile watumishi wa serikali na wengine wa umma; wafanyibiashara ndogondogo; wakulima wadogodogo nk) wana uwezo wa kumudu kununua magari mapya na kuyalipia ushuru unaotakiwa na serikali?

  Je, anaposema kuwa magari yenye zaidi ya miaka mitano yapigwe marufuku kuingizwa nchini inalenga wananchi wenye kipato gani?

  Je, kupiga marufuku kusajili gari lenye umri zaidi ya miaka mitano lina mantiki yoyote? Je kama gari la zaidi ya miaka mitano ni bora zaidi ya la miaka mitatu, kamanda Kombe anataka kutuambia ni nini?

  Je, kutokana na hali ya ugumu wa maisha hasa kwa kupanda kwa bei ya mafuta ya petroli na chakula, Kamanda Kombe haoni kuwa ni kuwabebesha mzigo mkubwa wananchi wa kulipia gharama za ukaguzi na usajili kila baada ya muda mfupi? Je ni viwango gani ambavyo vinakubalika katika ngazi ya kimataifa?

  Angalizo, matatizo ya Jiji la Dar es Salaam siyo matatizo ya nchi nzima, hivyo basi si vyema kutoa 'amri' ambazo zitawaumiza wananchi wengine wasio wakazi wa Jiji la Dar kwa sababu tu watoa amri hao wamekosa vision ya kuongoza na kutatua matatizo katika maeneo yao waliyokadhiwa kiutendaji.

  Kwa taarifa tu:
  Jiji la Dar es Salaam halikujiandaa kwa ongezeko la wakazi wake na hadi leo hii bado halijachukua hatua zozote madhubuti za kupambana na ongezeko la wakazi. Sifa kuu ya majiji ni kukua kwa majiji hayo ambayo yanaletwa na ongezeko la watu.

  Takribani barabara zote za jiji hazikidhi kabisa ongezeko la watu na ukuwaji wa jiji.
  Wakazi wengi waJiji wanategemea barabara chache na zenye uwezo mdogo kimatumizi.

  Hebu tuangalie barabara zinazotegemewa katika jiji kubwa kama la Dar:

  Kanda ya Temeke:

  Kilwa Rd Temeke/Chang'ombe Rd na Nelson Mandela EW.
  Idadi ya magari...?
  Idadi ya watumiaji wabarabara...?

  Kanda ya Ilala:

  Nyerere Rd, Uhuru St; Kawawa Rd; Nelson Mandela EW.
  Idadi ya Magari...?
  Idadi ya watumiaji wa barabara...?

  Kanda ya Kinondoni:

  Morogoro Rd, Bagamoyo Rd/Alli Hassan Mwinyi Rd; Old Bagamoyo Rd; Kawawa Rd; Nelson Mandela EW/ Sam Nujoma Rd.
  Idadi ya magari...?
  Idadi ya watumiaji...?

  Kwa kifupi wakazi wa jiji wapatao zaidiya milioni Tatu wanategemea zaidi barabara nilizozitaja hapo juu.

  Kwa hiyo kamanda Kombe anataka kutuambia kuwa barabara hizo ziwachwe wazi kwa matumizi ya watanzania wachache na wageni wenye uwezo wa kuagiza magari mapya na ninadhani ndiyo hao ambao kamanda Kombe anawawakilisha katika hoja yake nzima.


  Hitimisho:
  Tatizo la msongamano wa magari jiji litatuliwe kwa kushirikisha wadau wote na siyo amri za Kamanda Kombe.
   
 10. K

  Kithuku JF-Expert Member

  #10
  Oct 6, 2008
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  What is wrong with *ombe? Ona Zombe, Pombe, na sasa Kombe! Just kidding!
   
 11. C

  Chuma JF-Expert Member

  #11
  Oct 6, 2008
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mafisadi wanafanya juu chini kuzuia magari ya miaka 5...Huyu Kombe hamna kitu kichwani...Viongozi wetu wanapenda kukurupuka!!!
   
 12. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #12
  Oct 6, 2008
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  TATIZO kubwa la nchi yetu... ni kwamba kila mtu/idara/wizara ikitoka inalipuka na la kwake bila kuangalia idara nyingine au wizara nyingine ina maslahi/athari gani katika suala linaloamualiwa au linalopangwa... eventually kwenye utekelezaji mambo yanashindikana!!! Thus why wananchi wanaambiwa jambo lakini eventually halitokei

  in short "There is no Proper Coordination within the Government System"
   
 13. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #13
  Oct 6, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  To be short this is a Kasheshe's collapsed government mhh
   
 14. K

  Kipanga JF-Expert Member

  #14
  Oct 6, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 679
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  .....Mh!! Ogah, usije kukuta mtu mzima alikula short cut tu mpaka hapo alipo sasa ndio maana politiki mingi, matendo zero......
   
 15. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #15
  Oct 6, 2008
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Elimu? Unacheza nini. Darasa la nane
   
 16. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #16
  Oct 6, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  tungeweza kujenga fly over pale ubungo, morocco, kilwa road, kamata baadaye tukajenga ring roads eg , mbezi beach kuunganisha mbezi luis uatona tatizo la misongamano likawa historia. ACHANENI NA WALEVI KAMA AKINA KOMBE
   
 17. JuaKali

  JuaKali JF-Expert Member

  #17
  Oct 7, 2008
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 785
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kwa amri ya kombe ina maana magari yatupwe bado yakiwa kwenye warrant? maake kwa hesabu watengeneza magari wengi wanakupa angalau 6 years warrant (60,000 miles to 100000 or 5 to 10 years Whichever comes first). Kwa kufikiria kidogo sana maneno ya kombe ni maneno ya mkosaji hana jipya. Angefanya utafiti kabla ya kuropoka kwenye vyombo ya habari. Tanzania itakuja endelea tu pale watu kama kombe wakiondolewa offisini. Kuna mikangafu kibao barabara hapa kwa bush mbali na utajiri wa hii nchi sembuse Bongo. KOMBE ANGALIA UNACHOONGEA!!!!
   
 18. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #18
  Oct 10, 2008
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Juakali,
  Unachosema ni sawa kabisa lakini hatuna vipaumbele katika utekelezaji wa mambo.

  Kwa mfano:
  Ukianzia pale Bunju unaweza kufika Kigamboni Ferry bila ya hata kuingia katikati ya mji.
  Niliwahi kuitafiti nakuitumia njia hii wakati fulani.

  Unaanza safari yako Bunju inakuleta hadi Mbezi ya Morogoro Road. Ukitoka pale unakuja hadi Kimara mwisho unaingia kuelekea Segerea ambapo huko utakutana na barabara ya Pugu. Utaendelea zaidi kuelekea usawa wa Pugu Kajiungeni halafu unachukua njia ya kuelekea Chanika ambapo ukizidi kuifuta njia hiyo itakupitisha Mbande hadi Mbagala Mwisho, then unaelekea Kongowe ambapo utakutana na barabara inayoelekea Kibada , mjimwema hadi kigamboni ferry.

  Kama hii barabara ingetengenezwa kwa kiwango cha kimataifa na kuangalia mahitaji ya miaka 30 ijayo, ingeleta tofauti katika hali ilivyo leo.
   
 19. M

  Mkora JF-Expert Member

  #19
  Oct 11, 2008
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 360
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Lakini mimi mambo mengi yanayofanyika Tanzania kwa kweli siyaelewi kabisa, mfano mwak jana nilikuwapo kule wameamrisha magari yote yawe na fire extinguisher kama huna fine 20,000 na watu wananunua sasa mbona manufacturer hawaja recomend hicho kitu yaani pale wanapoweka mbele inapunguza hata hiyo panoramic view
  Ukija katika umri wa gari huu ni wazimu kabisa kwani under 5 year ya Europe inakuwa na Euro 4 gas emission ni tofauti na under 5 years ya India na chinaambao wamenunua mitambo ya zamani ya Europe kutengeneza magari mengi bado ni Euro 2 or even 1 gas emission ili kuendeleza nchi zao sas tumuulize huyu Kombe under five years ya wapi ulaya au India
   
 20. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #20
  Oct 11, 2008
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,212
  Likes Received: 314
  Trophy Points: 180
  Kwani hatuna chombo maalumu (NGO or otherwise) cha kupigania HAKI za wananchi? Maana serikali ya CCM imeacha kabisa kujali maisha yetu.

  Chombo kama kipo basi kiende mahakamani kipate restraining order dhidi ya Kombe na hao waliomtuma. Maana katumwa huyo, sio hivi hivi.

  Hii njia ya kupigania haki kupitia mahakama inafanya kazi wakati mwingine. Nakumbuka kuna kipindi serikali ilitoa amri mabasi ya Dar Express yasimamishe huduma zake (baada ya ajali mbili). Kwa vile mkuu wa hayo mabasi si mtu wa mzaha, alikwenda mahakamani na akaweza kulazimisha serikali isiyasimamishe mabasi yake.

  Hawa wabaya wetu wananunua magari kwa kutumia fedha za umma, na wanabadilishiwa mengine baada ya miaka michache tu. Sasa wanadhani hata sisi tunaotegemea fedha za jasho letu wenyewe tunaweza kufanya hivyo?

  Ieleweke hivi: Sehemu kubwa ya sisi Watanzania, hata wale ambao tumefuta ujinga, haijawahi kuendesha gari lenye umri huo mnaotaka wa chini ya miaka 5. Si kwamba hatupendi, ni hatuwezi. Sasa na hiki kidogo tulichonacho mnataka kutunyima?

  Ni rahisi kwa wale waliovimbisha matumbo kwa kutafuna fedha za umma kufungua vinywa vyao (in between eating and drinking), na kusema SASA TUENDESHE MAGARI YENYE CHINI YA MIAKA 5 TU. Kilichobaki ni sisi kupigania haki zetu mahakamani. Au tuendelee na kawaida ya "kuwaomba watuonee huruma"?
   
Loading...