Usajili wa line za Mawakala kwa alama za vidole

more88

JF-Expert Member
Apr 9, 2016
447
412
Nina line za kuweka na kutoa pesa ambazo nilinunua kwa mawakala wa mitandao husika zenye majina ambayo si yangu.

Kwa wiki kadhaa nimekuwa natumiwa sms kuzisajili kwa alama za vidole.

Nimejaribu kuuliza kama nitaweza kuzisajili jibu nililopewa ni kwamba lazima niwe na TIN NUMBER.

Mimi ni mjasiriamali mdogo ambaye nilikata kitambulisho cha mjasiriamali kile cha 20,000. Mtaji wangu ni chini ya milioni 4 kama alivyoagiza Rais.

Kama ni kweli ifikapo December 31 hizi laini za uwakala watazifunga basi hili zoezi litatuumiza sana wajasiriamali wadogo tuliojiajiri huku.

Ombi: Naomba kama itawezekana watumie hivi vitambulisho vya mjasiriamali pamoja na number ya NIDA kusajili kwa mbadala wa TIN Number kwa wajasiriamali ambao hawana TIN Number au leseni ya biashara.
 
tin ni bure mwanangu nenda tra kachukue huwezi kuwa na pesa au kuwa mfanyabiashara mkubwa kama haulipi kodi
Nje ya ofisi za TRA huwa kuna vishoka wanajihusisha na uuzaji wa TIN ndiyo maana huyu ahangaika
 
Nenda kafuate TIN number...

Nenda ukasajiliwa kama mlipa kodi, mbona ni bure, wasi wasi wako ni upi?

Cc: mahondaw
 
Waliongeza mpaka tarehe 20 January,ngoja tuone lakini bado hili swala kwa mawakala halijakaa poa,litaumiza wengi,udhauri ifikapo tarehe 19 Toa floti yako yote kwenye line ya uwakala ili wakifunga usipate hasara mara mbili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa nimekaa nafikiria itakuwaje voda wamezingua kwelii muhimu ni line isajiliwe kwa vidole mengine mbwembwe tu
 
Nina line za kuweka na kutoa pesa ambazo nilinunua kwa mawakala wa mitandao husika zenye majina ambayo si yangu.

Kwa wiki kadhaa nimekuwa natumiwa sms kuzisajili kwa alama za vidole.

Nimejaribu kuuliza kama nitaweza kuzisajili jibu nililopewa ni kwamba lazima niwe na TIN NUMBER.

Mimi ni mjasiriamali mdogo ambaye nilikata kitambulisho cha mjasiriamali kile cha 20,000. Mtaji wangu ni chini ya milioni 4 kama alivyoagiza Rais.

Kama ni kweli ifikapo December 31 hizi laini za uwakala watazifunga basi hili zoezi litatuumiza sana wajasiriamali wadogo tuliojiajiri huku.

Ombi: Naomba kama itawezekana watumie hivi vitambulisho vya mjasiriamali pamoja na number ya NIDA kusajili kwa mbadala wa TIN Number kwa wajasiriamali ambao hawana TIN Number au leseni ya biashara.
TIN ni bure nenda kachukue.
 
Back
Top Bottom