Usajili wa laini za simu kwa alama za vidole against ujumbe uliozagaa leo

bowlibo

JF-Expert Member
Dec 10, 2011
3,191
2,000
Wadau habari za wakati huu.

Naenda kwenye mada moja kwa moja. Leo nimepokea jumbe zenye maana na angalizo jumuishi kama hiyo attachment inavyojieleza.

Sasa swali ninalojiuliza ni kwamba iwapo mimi nimeshajisajili kwa kuchukuliwa alama za vidole kwa nini mtu mwingine ajisajili kwa kutumia namba yangu ya Nida system ishindwe kumreject na hapohapo hatua za awali za kisheria zichukue mkondo wake?

Nawasilisha, ila kama kweli namba moja ya NIDA inaweza kusajili watu wawili basi system hiyo ifanyiwe overhaul.

Karibuni
IMG-20191028-WA0020.jpg
 
Dusabimana

JF-Expert Member
Oct 24, 2019
277
250
All New Bio-metric Registration requires FINGER print which tally with NIDA ID number. Thus, its not possible for anyone to use your NIDA ID copy or number to register a new SimCard. Government and MNOs forecasted on this risk sometimes back before Kick off of this project.
Hata mimi nilikuwa nafikiri kitambulisho cha NIDA ndo kinahusika kusajili line za simu kwa biometrik, nashangaa tena kuna copy!
 
Panya Mabaka

JF-Expert Member
Apr 3, 2014
552
500
Ninachojua labda anayesajili anaweza kutumia alama zako za vidole hasa kwa wale wanaotumia smart phone au kompyuta kwani wanaweza kujifanya wanaedit taarifa.

Kuna uwezekano ukimaliza kusajili anaweza kujifanya anaedit kumbe anakopi alama zako za vidole na au anaingia kwenye taarifa zako zote na kuedit namba kuweka namba mpya kisha kuirudisha akisha maliza kufoji.

Mtoa mada ana wazo jema ila cha muhimu ni kusajili katika ofisi inayojulikana namba zote ili ikitokea jambo lolote unapata pa kuanzia. tuepuke vishoka wanaozunguka mitaani maana wanaweza kufanya lolote kwa sababu ya njaa
 
Evari77

JF-Expert Member
Apr 25, 2015
541
500
Acha kupotosha, numbers ya kitambulisho au kitambulisho kinatumimika kwanza ku verify jina lako lililopo na usajili wa awali visipo fanana unaambiwa uende mahakamani,

Pili jina likiwa sahii na picha yako na wewe ulivyo ndipo unaweka kidole ,tigo wao wanatuma text yenye number code ya kusajilia kwenye line yako hii ni kujua kama line unayo ni yako, Voda ni rahisi zaidi inategemea na mfumo wao

Mwisho ni vigumu sana kutumia number ya kitambulisho cha mtu kusajilia wakiweka number kuna connection kati ya NIDA kuweza kuona kumbukumbu zako

bowlibo,
 
Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
12,144
2,000
Aliye toa tangazo bado yuko na akili ya kijijiji.

Mwambie awe anapiga kopi na mikono yenu.
Wadau habari za wakati huu.

Naenda kwenye mada moja kwa moja. Leo nimepokea jumbe zenye maana na angalizo jumuishi kama hiyo attachment inavyojieleza.

Sasa swali ninalojiuliza ni kwamba iwapo mimi nimeshajisajili kwa kuchukuliwa alama za vidole kwa nini mtu mwingine ajisajili kwa kutumia namba yangu ya Nida system ishindwe kumreject na hapohapo hatua za awali za kisheria zichukue mkondo wake?

Nawasilisha, ila kama kweli namba moja ya NIDA inaweza kusajili watu wawili basi system hiyo ifanyiwe overhaul.

Karibuni
 
Mzee Mukaruka

JF-Expert Member
Jun 18, 2012
713
500
All New Bio-metric Registration requires FINGER print which tally with NIDA ID number. Thus, its not possible for anyone to use your NIDA ID copy or number to register a new SimCard. Government and MNOs forecasted on this risk sometimes back before Kick off of this project.
Kwa sisi tusiojua Kiingereza, "Mpenda pombe" anasema hivi, Usajili mpya kwa kutumia alama za vidole unataka ALAMA YA KIDOLE inayoendana na NAMBA YA KITAMBULISHO CHA NIDA. Hivyo, haiwezekani kwa mtu yeyote kutumia kitambulisho chako cha NIDA au NAMBA kusajili laini mpya.Serikali na MNOs walisha liona hili na siku za nyuma kabla hata mradi huu kuanza. Nadhani nimesaidia kidogo. Halafu nyie mnaoandika KIMOMBO humu hamjui kuwa Kimombo ni wito!
 
KUTATABHETAKULE

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
3,060
2,000
Mimi nimesajilia namba tu
Unatoa Namba na jina tayari unasajiriwa. Je huu utaratibu una njia ya kucheki kama alama za vidole vya aliyejisajiri ni vya huyo anayetumia jina hilo? Vinginevyo hapa pana tatizo. Na pia anayetaka kufanya maovu, atajisajiri kwenye kampuni nyingine ya SIMU ambao mhusika hajajisajiri.
 
bowlibo

JF-Expert Member
Dec 10, 2011
3,191
2,000
Copy sio cha kushangaza. Maana tunahitaji tu namba ya nida.
Kinachoshangaza ni finger print anatoa wapi?
That is my point 👍

Na kwa watu wa Nida watueleze possibilities za hili kutokea au watutoe hofu in their own way.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom