John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 365
- 1,373
Jana hata kabla ya Simba kutoa taarifa kuhusu kumsimamisha Bernard Morrison nilieleza kuwa mchezaji huyo amesimamishwa kwa sababu ya utovu wa nidhamu kwa kile kilichodaiwa kuwa alitoroka kambini.
Baadaye Morrison akapost kwenye pages zake kuwa kuna kitu kikubwa kinakuja akiwa ameweka picha ameshika mabegi kama mtu anayesafiri.
Sasa taarifa za ndani ya Simba zinaeleza kuwa klabu hiyo haina mpango wa kuendelea kuwa na mchezaji huyo, hivyo wanachosubiri ni kumalizika kwa mkataba wake ambao umesalia miezi mitano, kisha wamalizane naye kwa kuwa hajaonyesha uwezo walioutarajia.
Mbali na hapo inaelezwa kuwa kuna kigogo wa Klabu ya Yanga yupo tayari kusimamia shoo ili mchezaji huyo arejee Jangwani, jambo ambalo limewagawa baadhi ya viongozi.
Kwa hatua iliyopo ni kuwa Morrison anaweza kufanya mazungumzo na klabu nyingine yoyote kwa kuwa kanuni inamruhusu na ikiwezekana kusaini mkataba wa awali.
Hakuondoka Yanga vizuri, hiyo ni hoja ya baadhi ya viongozi wanaopinga kurejea kwake klabuni hapo wakionekana watakuwa wanamrudisha mtu aliyewakosea heshima, lakini wale wanaounga mkono kurejea kwake wanataka arejee ili wawaumize wapinzani wao wa jadi, Simba.
Hivyo, ni suala la muda kusubiri nini kitatokea, Simba wapo kwenye presha ya matokeo na kiwango bora, je, wataendelea kumfikiria Morrison au watapuuzia na kumuacha akiondoka ikiwezekana kwenda Yanga kirahisi? Muda utazungumza ila suala la Morrison kuondoka Simba hilo halikwepeki kwa sasa.