Usajili mpya wa Brella: Husajiliwi kama huna kitambulisho cha Taifa, NIDA nao wanachelewa kutoa kitambulisho

EMMANUEL JASIRI

Senior Member
Feb 2, 2015
127
62
Brella mmetutangazia mfumo mpya wa usajili, sisi ambao tulijisajili tumetakiwa kuweka kwa upya taarifa zetu,.

Wengine wetu hasa mimi binafsi niliweka namba ya leseni yangu ya udereva hapo awali, sasa napoenda kujaza upya taarifa zangu nadaiwa Kitambulisho cha Taifa ambacho wengi wetu hatuja kabidhiwa bado.

Mimi binafsi NIDA wamechua taarifa zangu na picha lakini bado hawajanipa kitambulisho cha Taifa, kilicho nisikitisha zaidi ukipiga simu Brella wanadai mfumo unataka hivyo hawana msaada ila niwapigie NIDA, nikipiga NIDA simu haipokelewi.

Hivi kweli kwa Mtanzania mwenye nia ya kupata mafanikio kwa mfumo huu ambao anapotaka msaada wa haraka kwa mambo muhimu kama haya halafu simu yake haipokelewi, kweli ni changamoto iliyo nihuzunisha, sisi ambao hatuja kabidhiwa vitambulisho vya Taifa halafu tunadaiwa hatma yetu ni nini?

Shughuli zetu zinawategemea ninyi Brella na NIDA tusaidieni huku hali maisha yetu yanawategea ninyi.

Naomba majibu toka kwenu.
 
Brella mmetutangazia mfumo mpya wa usajili ,sisi ambao tulijisajili tumetakiwa kuweka kwa upya taarifa zetu,wengine wetu hasa mimi binafsi niliweka namba ya leseni yangu ya udereva hapo awali,sasa napoenda kujaza upya taarifa zangu nadaiwa Kitambulisho cha Taifa ambacho wengi wetu hatuja kabidhiwa bado,mimi binafsi NIDA wamechua taarifa zangu na picha lakini bado hawajanipa kitambulisho cha Taifa,kilicho nisikitisha zaidi ukipiga simu Brella wanadai mfumo unataka hivyo hawana msaada ila niwapigie NIDA ,nikipiga NIDA simu haipokelewi,hivi kweli kwa MTanzania mwenye nia ya kupata Mafanikio kwa mfumo huu ambao anapotaka msaada wa haraka kwa mambo muhimu kama haya halafu simu yake haipokelewi,kweli ni changamoto iliyo nihuzunisha,sisi ambao hatuja kabidhiwa vitambulisho vya Taifa halafu tunadaiwa hatma yetu ni nini?Shughuli zetu zina wategemea ninyi Brella na NIDA tusaidieni huku hali maisha yetu yanawategea ninyi ,naomba majibu toka kwenu.
Mkuu pole sana
Lakini unashauriwa kwenda katika ofisi za NIDA ulizojiandikisha. Pale utapewa namba yako ya kitambulisho ambayo ndiyo inahitajika. Naamini utapata namba kutokana na hatua uliyosema umefikia katika kuwapa "details" zako hao NIDA
Pole sana
 
Hapa Dodoma sijajua ofisi ya NIDA ipo wapi maana tuliandikishwa kwa Mwenyekiti wa Kijiji kuhusu vitambulisho,nina ambiwa niende NIDA Dar,kwa sasa nipo DODOMA.
Nadhani ofisi zao huwa kwenye ofisi za wakuu wa Wilaya ama Manispaa...ila sina uhakika kivileeeee
 
Sijui kama NIDA Wana ofisi Dodoma zaidi nimepiga simu sana haipokelewi wakati mwingine inakatika
upload_2018-3-27_15-7-58.png


Ofisi zao hizo unaingia kwenye website unapata

Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
 
Back
Top Bottom