Usaili wa SUA uliofanyika Chuo cha Ualimu Sumbawanga Leo ni uhuni uliopitiliza

Kuwaamini na kuwapa first priority si kwa sababu ya ubora wao, wanahofu ya kushusha hadhi ya chuo. Mi nilisomea UDSM, lakini tukiweka ushabiki pembeni, kwa kilimo na misitu, SUA is the best. Lakini wildlife na tourism MWEKA ni level nyingine.
Ulisomea bachelor yako ya wildlife chuo gani. Kwa SUA waliosomea SUA ni firstly priority. Wanawaamini wanafunzi waliosomea pale kuliko chuo kingine

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanajamvi niwape habari ya usaili ulioitishwa na SUA kuwapata tutorial assistants katika vitivo kadhaa kwenye campus yao ya Mizengo Pinda.

Majuzi ndio nilianza kuhisi mbele kuna mizengwe baada ya kutolewa orodha ya wanaokutwa kitengo cha wildlife Management.

Idadi ya ya watu 32 kuitwa kwa ajili ya post 1 haikunisumbua, bali jina la mmoja ambaye ni mwanafunzi wa masters anayesoma SUA kwa sasa.

Ikumbukwe post tulioitiwa atakaefaulu baadae itabidi akasomeshwe masters. Saa 2 leo asubuhi muda wa kuanza interview, wahusika hawajafika. Saa 4.30 tumeanza usaili namwona bwana wa masters nae yupo. Ilikuwa paper ya saa 1 na nusu.

Matokeo tuliambiwa saa 9. Mpaka saa10.30 ndio anakuja bw mmoja, anatoa kikaratasi mfukoni na kutangaza majina 5 ya waliofaulu, wote ni wahitimu wa SUA na wa masters yumo. Naamini hata hao 4 ni wasindikizaji.

Hata hivo nimeiona Sumbawanga kwa mara ya kwanza.

Pole sana
hii ipo sana, sio tu huko, na dunia ingine wala hata si kujuana au rushwa
Naamini unachosema, hao ni wapuuzi tu

"Fikiria umetoka sayari ya Mars na unaishi sayari ya Jupiter, umetafuta kazi, na ili wa Jupiter kutekeleza kipengele cha Usawa(Equality) wanakuita kwenye usaili pamoja na waliotoka Neptune mpaka Pluto, lakini kazi anapata wa kwao wa Jupiter, halafu wanasema lakini tumefuata Usawa (Equality)na tumewaita wote kutoka sayari mbalimbali lakini hawajafanikiwa."

Hii imenikuta sana mpaka nikashinda, sikukata tamaa

Endelea kupambana utapata
 
Duuuuhh,
Mkuu vip NSSF wameshakupa haki yako? Punguza shutuma Mkuuu huenda hata huko ulikokuwa mdomo ndio Umekutoa. Jifunze kuwa mkimia na kuenenda zako Mkuu hizi paraparaaa hazina mantiki kwa Msomi wa Kiwango chako, waachie Wanasiasa be proffessional.
Wanamjua huenda
 
Chuo hiki kipo Kibaoni karibu na mbuga ya Katavi njia ya kwenda Mpanda na nadiriki kusema “It has promising prospects” wadau mkawekeze katika maeneo mbalimbali kuanzia pale Usevya fursa zipo nyingi.

Nirudi kwenye mada hebu mtoa mada acha kutafuta excuses Panel ilikuwa imejizatiti vizuri nyie madogo wengi mmekuja hamko serious hata kimwonekano na kiukweli ushindani pia ulikuwa mkubwa hivyo usitafute pa kuangukia endelea kujipanga na pambana.


Sent using Jamii Forums mobile app
Ukifika usevya kula kuku kwa selikal mi ntalipa tu
 
200
Daaah, mimi sikuhangaika kabisa kupata kazi. Sikuwa na connection, nilifosiwa kuapply, nilizifanya kwa kiburi na kujiamini sana. Nlikuwa najibu kwa dharau sababu maseali yalikuwa rahisi sana. Kulikuwa na watu wananizidi vyeti, na wala sikuwa na mtu aliyenifahamu. Niliapply sehemu mbili idara ya maji mwanza na hapa nlipo siwezi kutaja. Ila pote nlipata. Nikachagua huku sababu ya tofauti ya elf 50 tu. Ilikuwa 2008. Sikuwahi kusota nimemaliza udm 2007

Sent using Jamii Forums mobile app
2008 hapakuwa Na competition ya kutosha kama vijana wanaomaliza kipindi hiki. Kuna intake kama 5 ziko mtaana. Kwa hiyo vichwa kwenye kila intake wanahudhuria interview hapo hapo majina ya mfukoni
 
Unaonekana ulishapata kisingizio cha kushindwa mapema kabla ya interview.Hata ningekuwa mimi natoa kazi wewe ningekuchuja mapema kabisa unaonekana hata kwenye hiyo test umeandika malalamiko badala ya majibu

Labda kuwasaidia na wengine ambao wako katika harakati za kutafuta ajira.waajiri wowote hasa wa sasa wanaangalia sana pamoja na vitu vingine kitu kinaitwa "ATITUDE" .Unajua mkiitwa kwenye interview ujue wote mliohudhuria mna kidhi sawa zile sifa za msingi ,ila wanatafuta mwenye sifa za ziada .Kutegemeana na aina ya kazi, Ukiwa na vielement vyovyote vya ujuaji kupita kiasi na kiburi flan hivi ujue utachujwa mapema.Utaniuliza sasa watanijuaje tabia siku ya kwanza tuu?.Ni hivi , kuna maswali yatakayolenga kuangalia hicho kitu.na unaweza usijue kwamba swali linakupima atitude. Interview structure na questions zimekuwa structured kupata uhalisia wa mtu wanayemtaka.Hakuna mtu anayetaka akuweke kwenye kazi yake halafu umletee uanaharakati au ushindwe kufanya kazi au vyote kwa pamoja

Siku nyingine tutazungumzia namna bora ya kuishi mahali pa kazi.kutengeneza mahusiano yenye tija na kupunguza/kuepuka ugomvi na mabosi wetu na hata wafanyakazi wenzetu.Maana hili nalo ni tatizo kwa vijana wengi wanao ajiriwa sasa.mtu anaingia kazini leo baada ya wiki ameshaizoea ofisi utadhani ana miaka kumi.
 
Wanatafuta 'tutorial assistant', na ukipata utatakiwa ukasome ili uwe assistant lecturer. Umesema alikuja mtu ambaye ana soma Master, kama yuko vizuri hata mimi ningemchukua yeye (huoni kuwa anampunguzia mwajiri kazi ya kumsomesha hiyo Master ambayo angekusomesha wewe)
Mbona kuna watu wana masters wapo wengi?
Wasingesumbua kuita ita watu kupotezeana muda na gharama
 
Mwombaji wa Masters huyo ameover qualify hastahili kuwepo, pia hata Kama hukuainisha wakati anaomba huo ni uhuni, na anapaswa kwenye cv awe alionesha hivyo, maana ya kuhitaji TAs inafahamika, nadhani wahusika wa utumishi wanaopelekwa huko hawana sifa, hivi nafasi ya assistant lecturer mwenye degree moja anaruhusiwa kuomba na kuitwa kwenye usaili, Tanzania kuna upuuzi hapo usikute ukabila umetumika, fuatilieni kwenye hio panel au hizo panels hawakosi watu walau wa kabila moja kuanzia watatu kila session au minimum wawili, mtoa maada nitafutie orodha ya panel members kwa idara zote mimi sitaongea ntawaachia nyie na jamhuri , hii nchi ethnic skewness inachekewa sana na unakuta VC na Ma DVC hawaelewi na kutoona rafu za kipumbavu na kimakusudi kabisa. Ajira za vyuo vikuu zina uozo sana, hata kwenye panels watu wanachaguana kwa kusudio la uovu, na kusipokuwa na transparency kwenye mtihani wa mchujo hasa usimamizi wa marking na total marks, kingine kukosekana kwa uniformity kwenye maswali ya oral, na kualika panelists ambao hawawezi kuwa objective kwa kukosa ufahamu wa maswali ya eneo la fani au bobezi kwa mwombaji hivyo kujikuta anatoa marks kwa kukisia, this fatal mistake has really now become a tradition. With the ongoing employment scarcity the maximum levels of fairness and transparency should be our priority. Nchi ni yetu sote njia takatifu ni nyembamba na kuwapitisha kondoo wafaao kwa bwana ni lazima roho wa bwana wa kweli akae ndani yetu na ajitawale ndani yetu. Impartiality may be an intergral part of God's commandments.
 
Duuuuhh,
Mkuu vip NSSF wameshakupa haki yako? Punguza shutuma Mkuuu huenda hata huko ulikokuwa mdomo ndio Umekutoa. Jifunze kuwa mkimia na kuenenda zako Mkuu hizi paraparaaa hazina mantiki kwa Msomi wa Kiwango chako, waachie Wanasiasa be proffessional.

Hizo ni kejeli na si uungwana, naona mwendokasi imekupa jeuri usikejeli kwenye maada ambazo huna faida nazo na wewe sio mwajiriwa na haushiriki kuajili kwenye sekta yq umma
 
Mkuu relax kwa maelezo yako sijaona tatizo la jamaa lipo wapi kwani yeye kuwa mwanafunzi wa masters hapo atashindwa kuwa tutorial assistant?

Kingine tutorials wengi wanapendelewa wale waliosoma chuo husika ivyo usishangae kukawa na kaupendeleo fulani kwao ila ungekuwa uko fit kwenye paper ungekuwa mmojawapo wa hao wanne na hii tread usingeiandika
Umemjibu vizuri Sana. Amechemka pepa anakimbilia huruma za JF
 
Unaonekana ulishapata kisingizio cha kushindwa mapema kabla ya interview.Hata ningekuwa mimi natoa kazi wewe ningekuchuja mapema kabisa unaonekana hata kwenye hiyo test umeandika malalamiko badala ya majibu

Labda kuwasaidia na wengine ambao wako katika harakati za kutafuta ajira.waajiri wowote hasa wa sasa wanaangalia sana pamoja na vitu vingine kitu kinaitwa "ATITUDE" .Unajua mkiitwa kwenye interview ujue wote mliohudhuria mna kidhi sawa zile sifa za msingi ,ila wanatafuta mwenye sifa za ziada .Kutegemeana na aina ya kazi, Ukiwa na vielement vyovyote vya ujuaji kupita kiasi na kiburi flan hivi ujue utachujwa mapema.Utaniuliza sasa watanijuaje tabia siku ya kwanza tuu?.Ni hivi , kuna maswali yatakayolenga kuangalia hicho kitu.na unaweza usijue kwamba swali linakupima atitude. Interview structure na questions zimekuwa structured kupata uhalisia wa mtu wanayemtaka.Hakuna mtu anayetaka akuweke kwenye kazi yake halafu umletee uanaharakati au ushindwe kufanya kazi au vyote kwa pamoja

Siku nyingine tutazungumzia namna bora ya kuishi mahali pa kazi.kutengeneza mahusiano yenye tija na kupunguza/kuepuka ugomvi na mabosi wetu na hata wafanyakazi wenzetu.Maana hili nalo ni tatizo kwa vijana wengi wanao ajiriwa sasa.mtu anaingia kazini leo baada ya wiki ameshaizoea ofisi utadhani ana miaka kumi.
Best Comment ya karne kwa wanaotafuta kazi wooote. Hutaki "endelea kulalamika naitwa intaviews lkn kazi sipati".
 
Mimi mwenyewe nilishawah kupiga interview 2 za Tanesco moja nilienda kufanyia Mtwara na zote nilikuwa nakomaa napita kwenye mchujo hadi naingia oral halaf mwisho wa siku kimya hakuna majibu.Na interview nyingine nilienda kufanya Songea Tanroad nayo hola,Na kabla ya hapo nilishawahi kufanya TPDC michujo yote nikapenya baada ya kupiga oral kimya ndio maana nilikata tamaa kabisa na kazi za serikali.
Shirika ambalo ni rahisi kupata ni Idara ya maji mikoani,sio Dar.
Watu wasiowahi kukutana na hizi changamoto watamkebehi mtoa mada hawajui kuwa haya mambo yapo sana.
Ili

nikuta mimi Tanesco Mwanza. Nimechoma nauli toka Dar mpaka Mwanza plus accomodation halafu ni vile tunaenda kuhalalisha watu wapate kazi. Toka siku hiyo nimeachana na kuomba kazi napiga mishe zangu binafsi na maisha yanaenda.
 
Maisha ni safari ndefu isiyo na utabiri wa badae nimefanya interview SUA Mara ya kwanza ilikuwa mwezi wa 4/2015 tulikuwa 9 akapata ndugu yangu sikuhuzunika tulifurahi pamoja Mara ya pili ilikuwa mwezi 9/2017 tulikuwa 10 interview ikarudiwa sababu some panel members were also referees of interviewed candidates na mwaka Jana mwezi wa 12 tulikuwa 33 anahitajika 1 kwenye interview ya written wakabaki 5 wenye above 50% Mimi nilikuwa wa 6 na alama 46.

Nimalizie tu kushinda usahili ni mchakato sio Bahati ile post baadae ikagundulika nilikatwa tu kimkakati inatia uchungu lakini ni hatua nzuri kupitia katika harakati za kuwa MTU bora zaidi wala sikurudi nyuma natambua maisha yana No No nyingi sana kuliko Yes tunatumia akili lakini kamwe usifosi sana kitu subiri muda wako utafika

Mwezi ule wa 12/2019 nikarudi na mfadhaiko sana wa nafsi sikukuu zote nikawa busy kuomba scholarships za kusoma njee kufikia February 2020 niliweza kuomba scholarship kibao zilizotolewa na wizara ya elimu ikiwemo
Hungary, China embassy, Turkish embassy, Indian council of agriculture, Queen Elizabeth, Bangor university Distance learning, Poland scholarship.

Mpaka sasa 2 zimetiki bado nasubiria majibu mengine ila angalau na matumaini mengine ya kubadili kabisa mwelekeo na ni fursa nzuri kuliko ata nafasi niliyokuwa napambania kwa badae naweza kupata tena zaidi ya nafasi niliyozani nimepotezewa. Hujui hatma ya Mungu na maisha yako

Pia Shida nyingine sio kupata!!! Bali namna gani utatumia nafasi uliyopata kujenga fursa zaidi? Kuongeza connection zenye tija? Elimu utakayopata itanufaisha namna gani jamii yako? Wewe utabadilika kwa namna gani? Ukimaliza kusoma je utarudi kuwa mzigo kwa taifa lako? Hapa lazima uwe na mkakati unapopata scholarship sio kusoma tu!! Kutembea tembea nchini kwa watu tu bila mipango!! Kupiga selfie tu!!!

Kijana usikate tamaa endelea kupambana Nina story nyingi sana kuhusiana na interview na viroja vyake mwaka 2014 nilihudhuria interview ya Barric Gold Mining ilifanyikia Serena hotel DSM tulikuwa watu zaidi ya 400 tukafanya amplitude test total candidates waliokuwa wanahitajika ni 26

Majibu kutoka round 2 tukabaki 48 post yangu nikabaki na mdada so tulikuwa 2 kwenye oral interview ilifanyikia masaki nikapita bila kupingwa kilichofwata kazi sikupata Mimi internship akapewa yule Dada alikuwa ni mtoto wa balozi akafanya miezi michache akaenda nje kusoma ..... Nikawa nawasiliana nae bla blaa siku akaniambia I wish hii nafasi yako ningekuachia I am very sorry for you Kevi bla bla ikapitaga

Kisa kingine nilichokosaga ilikuwa ISEC shoppers plaza kumbe walitakiwa kubalance gender interview ipo karibu mwishoni Jamaa nasikia anaambiwa itabidi apunguze wakaka ambawo tayari amesha wachagua japo wao bado hawajui kama tayari Mimi na wengine ilikuwa bado hatujafanyiwa so automatic possibility ya kuchaguliwa mkaka kwa tuliobaki ikawa Zero.......

Ukikosa usilalamike endelea kukaza na kuwa stable zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu kusoma masters na PhD kunaweza ongeza frustration zaidi ya unavyofikiria
 
Ni kweli mkuu,ukishindwa kuitumia degree yako na kuibadilisha kujiongeza kimtaani zaidi ukienda kusoma tena ndio utazidi kuchanganyikiwa hasa pale unapomaliza masters yako halafu ukirudi Bongo unakosa hata kazi ya kufagia barabara.
Mkuu kusoma masters na PhD kunaweza ongeza frustration zaidi ya unavyofikiria
 
Ni kweli mkuu,ukishindwa kuitumia degree yako na kuibadilisha kujiongeza kimtaani zaidi ukienda kusoma tena ndio utazidi kuchanganyikiwa hasa pale unapomaliza masters yako halafu ukirudi Bongo unakosa hata kazi ya kufagia barabara.
Yh wengi wanafikiri akishapata PhD Basi umasikini Keisha..kumbe wanajidanganya
 
Back
Top Bottom