Usaili wa SUA uliofanyika Chuo cha Ualimu Sumbawanga Leo ni uhuni uliopitiliza

kamwamu

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,488
3,263
Wanajamvi niwape habari ya usaili ulioitishwa na SUA kuwapata tutorial assistants katika vitivo kadhaa kwenye campus yao ya Mizengo Pinda.

Majuzi ndio nilianza kuhisi mbele kuna mizengwe baada ya kutolewa orodha ya wanaokutwa kitengo cha wildlife Management.

Idadi ya ya watu 32 kuitwa kwa ajili ya post 1 haikunisumbua, bali jina la mmoja ambaye ni mwanafunzi wa masters anayesoma SUA kwa sasa.

Ikumbukwe post tulioitiwa atakaefaulu baadae itabidi akasomeshwe masters. Saa 2 leo asubuhi muda wa kuanza interview, wahusika hawajafika. Saa 4.30 tumeanza usaili namwona bwana wa masters nae yupo. Ilikuwa paper ya saa 1 na nusu.

Matokeo tuliambiwa saa 9. Mpaka saa10.30 ndio anakuja bw mmoja, anatoa kikaratasi mfukoni na kutangaza majina 5 ya waliofaulu, wote ni wahitimu wa SUA na wa masters yumo. Naamini hata hao 4 ni wasindikizaji.

Hata hivo nimeiona Sumbawanga kwa mara ya kwanza.
 
Mkuu relax kwa maelezo yako sijaona tatizo la jamaa lipo wapi kwani yeye kuwa mwanafunzi wa masters hapo atashindwa kuwa tutorial assistant?

Kingine tutorials wengi wanapendelewa wale waliosoma chuo husika ivyo usishangae kukawa na kaupendeleo fulani kwao ila ungekuwa uko fit kwenye paper ungekuwa mmojawapo wa hao wanne na hii tread usingeiandika
 
Hongera mkuu kwa kuiona sumbawanga.

Mimi mwenyewe nimetalii sana kupitia interview mbalimbali za serikalini.

Ila hadi sasa nimekata tamaa sitaki tena kazi zao nimesusa kabisa.

Nilishawahi kupiga interview kama 4 hivi za serikalini halafu unakuta unakomaa mwanzo mwisho kwenye michujo yote mwanaume unatoboa.

Unakuta unaingia kwenye Interview ya mwisho ya oral kila wakitaka kukutoa kwenye reli kidume bado unakaza na kukomaa nao halafu mwisho wa siku kimya hakuna majibu.

Ni ujinga mtupu.
 
Duuuuhh,
Mkuu vip NSSF wameshakupa haki yako? Punguza shutuma Mkuuu huenda hata huko ulikokuwa mdomo ndio Umekutoa. Jifunze kuwa mkimia na kuenenda zako Mkuu hizi paraparaaa hazina mantiki kwa Msomi wa Kiwango chako, waachie Wanasiasa be proffessional.
 
Mkuu relax kwa maelezo yako sijaona tatizo la jamaa lipo wapi kwani yeye kuwa mwanafunzi wa masters hapo atashindwa kuwa tutorial assistant?? Kingine tutorials wengi wanapendelewa wale waliosoma chuo husika ivyo usishangae kukawa na kaupendeleo fulani kwao ila ungekuwa uko fit kwenye paper ungekuwa mmojawapo wa hao wanne na hii tread usingeiandika


Sent using Jamii Forums mobile app
Simlaumu yeye bali wandaaji kuwaita watu kwa post ambayo ni earmarked.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duuuuhh,
Mkuu vip NSSF wameshakupa haki yako? Punguza shutuma Mkuuu huenda hata huko ulikokuwa mdomo ndio Umekutoa. Jifunze kuwa mkimia na kuenenda zako Mkuu hizi paraparaaa hazina mantiki kwa Msomi wa Kiwango chako, waachie Wanasiasa be proffessional.
Mdomo kazi yake ni kuongea, yawezekana wewe ndio mfaidika wa uhuni uliofanyika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chuo hiki kipo Kibaoni karibu na mbuga ya Katavi njia ya kwenda Mpanda na nadiriki kusema “It has promising prospects” wadau mkawekeze katika maeneo mbalimbali kuanzia pale Usevya fursa zipo nyingi.

Nirudi kwenye mada hebu mtoa mada acha kutafuta excuses Panel ilikuwa imejizatiti vizuri nyie madogo wengi mmekuja hamko serious hata kimwonekano na kiukweli ushindani pia ulikuwa mkubwa hivyo usitafute pa kuangukia endelea kujipanga na pambana.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chuo hiki kipo Kibaoni karibu na mbuga ya Katavi njia ya kwenda Mpanda na nadiriki kusema “It has promising prospects” wadau mkawekeze katika maeneo mbalimbali kuanzia pale Usevya fursa zipo nyingi..
Kwa hiyo wewe ni mmoja wa wale mliokuwa mnawachagua vijana wa tutorial?Ila kiukweli hizi kazi kama huna connection na hukusoma chuo hicho ,ila ulisoma chuo fulani hapa bongo kupata kazi ni ngumu.We gii wenu mna watu wenu kichwani.Huyo jamaa wa masters lazima ndo yeye atapita.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom