Usahili Utumishi zitumike lugha zote

Mundana

Member
Jun 8, 2015
57
125
Habari Za Mchana,

Poleni na majukumu na mihangiko ya Kila Siku na Kwa wale watakaofanya Usahili kesho niwatakie Usahili Mwema.
Sasa nirudi Kwenye topic, hili suala nimekua nikiliangalia Sana kwenye Usahili ukienda lugha inayotumika kuwasahili ni kiingereza. Hivi wanavyofanya hawatendi haki kabisa Yan unakuta MTU Ile kazi anaiweza vizuri na anaimudu akipewa kuifanya sasa kwenye suala la kujieleza au kujitetea Kwa lugha ya kiingereza inakuwa mtihani lakini anajua yupo vizuri, Sasa walau Utumishi basi wangekuwa wanaruhusu lugha zote mbili zitumike kiingereza na Kiswahili hasa kwenye usahili wa ana kwa ana na wa vitendo.

Kufanya hivyo kutawasaidia Wale watu ambao wanasifa na wanakizi vigezo vya hiyo Kazi na wao wapate nafasi. Haki inatakiwa kotekote kuleta usawa, hasa ukizingatia lugha ya Kiswahili ndo lugha yetu ya Taifa, kwanini wasiipe kipaumbele.

Kuna siku miaka ya nyuma nilienda kwenye Usahili sehemu Fulani Hivi, tulikuwa ni wengi Sana, tukapunguzwa Sana katika hatua zile za awali yan written na practical sasa ikabaki hatua ya mwisho ya oral nilikuwa na Dada mmoja hivi tunasubiri kuingia kwenye oral ya mwisho, Yule Dada mpaka nilimuonea huruma na machozi yanamtoka nikamfuata kujaribu kumuuliza nini kilichokuwa kina mliza, akaniambia kuwa Amalia kwasababu Yeye kujieleza Kwa lugha ya kiingereza hajui kabisa anajua Tu Ile ngeli ya kwenye makaratasi na sio kusimama mbele za Watu ukajenga hoja na wakuelewe vizuri kwake yeye ni mtihani, hivyo anaona kabisa hiyo Nafasi ameshaikosa tayari, uzoefu wa KAZI anao mzuri Tu lakini hapo kwenye lugha ndo palimshinda kabisaa hawezi hata kidogo.

Nikajaribu kumpa Moyo asikate Tamaa ajaribu Bahati yake, ikafika zamu yake kuingia, Yan Hata dakika moja haikuisha akawa Ametoka
Ile kazi hakufanikiwa kuipata hatua ya mwisho ndo ilimfelisha.

Utumishi wajaribu kuangalia Hilo suala walau basi wabalance lugha zote mbili zitumike kiingereza na Kiswahili ili kuwapa nafasi wengine waweze kupata Kazi. Mbona kwenye matangazo Yao ya Kazi wanatuandikia Kwa Kiswahili hasa Yale ya kuitwa kwenye Usahili au kuitwa Kazini.

Nawasilisha.
 
Mpatuka

JF-Expert Member
Nov 15, 2015
1,170
2,000
Kama chuo ulisoma kwa kiingereza na ukafaulu, basi lazima wakuulize kwa lugha uliyofaulia. Kushindwa kwako lugha ndiyo fursa kwa wengine nafasi ni chache na waombaji ni wengi.
 
Mundana

Member
Jun 8, 2015
57
125
Boss mbona katika oral unaruhisiwa kutumia aidha kiswahili ama kiingereza.

Na ipo hivyo siku zote.

Sent using Jamii Forums mobile app
Inategemea Sanaa
Au Labda kama Kazi yenyewe ni ya ulinzi au ya ubeki Tatu lkn sio Utumishi
Tena Mkuu usije ukajichanganya wakuruhusu uongee Kiswahili na wewe ukaongea imekula kwako ni mtego Huo
Labda itokee kwenye hiyo panel kuna MTU unajuana nae unaweza kubebwa.
 
Baba Joseph17

JF-Expert Member
Jul 15, 2013
9,428
2,000
Habari Za Mchana
Poleni na majukumu na mihangiko ya Kila Siku na Kwa wale watakaofanya Usahili kesho niwatakie Usahili Mwema.
Sasa nirudi Kwenye topic, hili suala nimekua nikiliangalia Sana kwenye Usahili ukienda lugha inayotumika kuwasahili ni kiingereza. Hivi wanavyofanya hawatendi haki kabisa Yan unakuta MTU Ile kazi anaiweza vizuri na anaimudu akipewa kuifanya sasa kwenye suala la kujieleza au kujitetea Kwa lugha ya kiingereza inakuwa mtihani lakini anajua yupo vizuri, Sasa walau Utumishi basi wangekuwa wanaruhusu lugha zote mbili zitumike kiingereza na Kiswahili hasa kwenye usahili wa ana kwa ana na wa vitendo.
Kufanya hivyo kutawasaidia Wale watu ambao wanasifa na wanakizi vigezo vya hiyo Kazi na wao wapate nafasi. Haki inatakiwa kotekote kuleta usawa, hasa ukizingatia lugha ya Kiswahili ndo lugha yetu ya Taifa, kwanini wasiipe kipaumbele.
Kuna siku miaka ya nyuma nilienda kwenye Usahili sehemu Fulani Hivi, tulikuwa ni wengi Sana, tukapunguzwa Sana katika hatua zile za awali yan written na practical sasa ikabaki hatua ya mwisho ya oral nilikuwa na Dada mmoja hivi tunasubiri kuingia kwenye oral ya mwisho, Yule Dada mpaka nilimuonea huruma na machozi yanamtoka nikamfuata kujaribu kumuuliza nini kilichokuwa kina mliza, akaniambia kuwa Amalia kwasababu Yeye kujieleza Kwa lugha ya kiingereza hajui kabisa anajua Tu Ile ngeli ya kwenye makaratasi na sio kusimama mbele za Watu ukajenga hoja na wakuelewe vizuri kwake yeye ni mtihani, hivyo anaona kabisa hiyo Nafasi ameshaikosa tayari, uzoefu wa KAZI anao mzuri Tu lakini hapo kwenye lugha ndo palimshinda kabisaa hawezi hata kidogo.
Nikajaribu kumpa Moyo asikate Tamaa ajaribu Bahati yake, ikafika zamu yake kuingia, Yan Hata dakika moja haikuisha akawa Ametoka
Ile kazi hakufanikiwa kuipata hatua ya mwisho ndo ilimfelisha
Utumishi wajaribu kuangalia Hilo suala walau basi wabalance lugha zote mbili zitumike kiingereza na Kiswahili ili kuwapa nafasi wengine waweze kupata Kazi. Mbona kwenye matangazo Yao ya Kazi wanatuandikia Kwa Kiswahili hasa Yale ya kuitwa kwenye Usahili au kuitwa Kazini.
Nawasilisha.
Kwani shuleni ulisoma masomo Kwa lugha Gani? Kwenye usaili swali 1 tu ndilo la kujieleza wewe mwenyewe mengine yote ni ya kitaalam field uliyosomea, watu wanazani ukifanyiwa usaili Kwa kiswahili ni Rahisi sana wanashindwa kuelewa kuwa Masuala uliyoyasoma Kuna baadhi misamiati yake Kwa kiswahili ukiulizwa utabiki unababaika kuelewa maana yake
 
Mundana

Member
Jun 8, 2015
57
125
Kama chuo ulisoma kwa kiingereza na ukafaulu, basi lazima wakuulize kwa lugha uliyofaulia. Kushindwa kwako lugha ndiyo fursa kwa wengine nafasi ni chache na waombaji ni wengi.
Nashukuru Sana Mkuu umeliona Tatizo
Tatizo ni mfumo Wetu wa Elimu bado Sio Rafiki haumuandai MTU kujiajiri Wala kuajiriwa.
Wao wamekazana Tu Vijana mjiajiri wakati mfumo bado Sio Rafiki basi waniajiri wao bado mfumo wao pia wa kuajiri sio mzuri.
Unachomokaje Hapo Kaka.
 
Mundana

Member
Jun 8, 2015
57
125
Kwani shuleni ulisoma masomo Kwa lugha Gani? Kwenye usaili swali 1 tu ndilo la kujieleza wewe mwenyewe mengine yote ni ya kitaalam field uliyosomea, watu wanazani ukifanyiwa usaili Kwa kiswahili ni Rahisi sana wanashindwa kuelewa kuwa Masuala uliyoyasoma Kuna baadhi misamiati yake Kwa kiswahili ukiulizwa utabiki unababaika kuelewa maana yake
Nimesoma Shule wanayofundisha Lugha ya kiingereza.
Yan Mkuu Shida inaanzia Wapi unajua Shida inaanzia kwenye Lugha tuliyofundishwa Huku chini maanisha awali, shule ya msingi na sekondari
Wangeamua Tu lugha moja itumike mwanzo mwisho kama ni Kiswahili basi Kiswahili kama ni kiingereza kiingereza mwanzo mwisho.
Unaona majirani zetu Kenya wao wapo vizuri, mfumo wao ni Mzuri wameamua lugha ya kiingereza itumike mwanzo mwisho na ndo wanayofundishia.
Na ndo maana kwanye lugha ya kiingereza wapo vizuri.
Lakini Sisi huku kwetu wamechanganya kiingereza na Kiswahili toka unavyoanza awali na msingi kidogo sekondari na vyuoni.
Sasa basi huo mchanganyo wao waliotuanzishia huku chini wahuruhusu pia hata kwenye Usahili ili MTU aweze kujieleza hata Kwa Kiswahili ikubalike na iwe rasmi na yeye huyu MTU aweze kupata nafasi.
 
Tatizo siyo kuchanganya lugha ya kiswahili na kiingereza, nachokiona kwasasa walimu wengi hawajui Kiinglish kwahiyo hata kufundisha wanakuwa wanaongea kiswahili badala ya Kiinglish Ili mwanafunzi elewe na hiyo inasababisha watu wengi kujieleza Kwa Kiinglish ni tabu sana
 
Top leader

JF-Expert Member
Aug 20, 2020
2,745
2,000
Mkuu pale we activate mode ya kuongea kingereza wale ni wabongo kikubwa usisite tembea ngeli hata broken humo humo umalize jiamini utakacho ongea English ni mtihani haswa conversation za kujibu hapo Kwa hapo kwa wabongo
 
Msonjo

JF-Expert Member
Oct 13, 2019
986
1,000
Nimesoma Shule wanayofundisha Lugha ya kiingereza.
Yan Mkuu Shida inaanzia Wapi unajua Shida inaanzia kwenye Lugha tuliyofundishwa Huku chini maanisha awali, shule ya msingi na sekondari
Wangeamua Tu lugha moja itumike mwanzo mwisho kama ni Kiswahili basi Kiswahili kama ni kiingereza kiingereza mwanzo mwisho.
Unaona majirani zetu Kenya wao wapo vizuri, mfumo wao ni Mzuri wameamua lugha ya kiingereza itumike mwanzo mwisho na ndo wanayofundishia.
Na ndo maana kwanye lugha ya kiingereza wapo vizuri.
Lakini Sisi huku kwetu wamechanganya kiingereza na Kiswahili toka unavyoanza awali na msingi kidogo sekondari na vyuoni.
Sasa basi huo mchanganyo wao waliotuanzishia huku chini wahuruhusu pia hata kwenye Usahili ili MTU aweze kujieleza hata Kwa Kiswahili ikubalike na iwe rasmi na yeye huyu MTU aweze kupata nafasi.
Umesema kweli.

Kama tunasema wasomi wanatakiwa wawe wanakimudu kiingreza vizuri basi inabidi mfumo wetu wa elimu uwe unasapiti hilo, maana kuitumia tu kama lugha kwa level za sekondari na chuo haitoshi.

Ndio maana watu wanakosa kujiamini.
 
Mundana

Member
Jun 8, 2015
57
125
Tatizo siyo kuchanganya lugha ya kiswahili na kiingereza, nachokiona kwasasa walimu wengi hawajui Kiinglish kwahiyo hata kufundisha wanakuwa wanaongea kiswahili badala ya Kiinglish Ili mwanafunzi elewe na hiyo inasababisha watu wengi kujieleza Kwa Kiinglish ni tabu sana
Sawa Mkuu Nakubaliana Na Wewe kuwa tatizo ni walimu wanaotufundisha, wanatufundisha kiingereza Kiswahili aka kiswanglishi.

Lakini Pia ikumbukwe hao walimu wenyewe nao walikuwa wanafunzi walifundishwa na mfumo huo huo wa kiswanglishi kwahiyo ni kama Tu muendelezo wa walichofundishwa.

Ifike Mahali tukubaliane kitu kimoja kama tumeamua Kiswahili basi iwe Kiswahili kuanzia awali mpaka chuo kikuu
Kama ni kiingereza ni kiingereza mwanzo mwisho,

Kama ni kuwaandaa watu wajiajiri wenyewe basi tutengenezewe mazingira mazuri toka uku chini awali mavyuo ya UFUNDI stadi yawe ya kutosha n.k

Kuliko sasa hivi hatueleweki mfumo tunaoutumia unawaumiza Vijana wengi Sana mtaani ndo maana tatizo la ajira limekuwà KUBWA Sanaa
Inabidi Tueleweke tusiwe kama Chura,
Chura haeleweki kama amesimama au amekaa au amechuchumaa.
 
Isaak

New Member
Oct 16, 2020
4
45
Nafurahia sana kuona MAWAZO chanya na huru Kwa kila mtu anavyojadili nami nasoma kiumakini na weledi ili siku yangu isinipite,Na natamani ningejua ukiitwa kwenye usaili hasa upande wangu wa udereva tu ndo professional yangu kwenye vitendo sina shaka hata kujielezea pia ila Kuna laziada wanaloliitaji maana nimeitwa mahala wajuzi tujuzane.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom