Lubebenamawe
JF-Expert Member
- Oct 27, 2014
- 1,971
- 2,232
Wadau kuna malumbano yamezuka yanahusu uteuzi wa wabunge wa kuteuliwa na Rais kwamba wabunge wanaume wamezidi idadi. Wengi wamedai kwamba katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inamwelekeza mheshimiwa Rais kwamba katika kuteua lazima wabunge wanawake wawe kwa uchache watano. Kwa hiyo basi Mheshimiwa Rais amefanya makosa kuteuwa watu ( wanaume) sita kuwa wabunge.
Wengi wametaja kipengele hicho kinachompa Rais mamlaka ya kuteua wabunge kuwa ni ibara ya 66 (e) kwa ajili ya kujenga hoja yangu nanakili kifungu hicho kwa lugha ya kiswahili na lugha ya kingereza.
Kwa kiswahili
Bila ya kuathiri masharti mengine ya ibara hii, kutakuwa na aina zifuatazo za Wabunge, yaani-
(a) Wabunge waliochaguliwa kuwakilisha majimbo ya uchaguzi;
(b) Wabunge wanawake wa idadi inayoongezeka, kuanzia asilimia ishirini ya Wabunge waliotajwa katika aya ya (a), (c ) na (d), itakayotajwa mara kwa mara na Tume ya Uchaguzi kwa taarifa iliyochapishwa katika Gazeti la Serikali baada ya kupata kibali cha Rais, watakaochaguliwa na vyama vya siasa vinavyowakilishwa Bungeni, kwa mujibu wa ibara ya 78, na kwa kuzingatia masharti ya uwiano wa uwakilishi baina ya vyama hivyo;
(c) Wabunge watano waliochaguliwa na Baraza la Wawakilishi kutoka miongoni mwa wajumbe wake; (d) Mwanasheria Mkuu;
(e) Wabunge wasiozidi kumi walioteuliwa na Rais kutoka miongoni mwa watu wenye sifa kwa mujibu wa ibara ya 67, isipokuwa sifa iliyotajwa katika ibara ya 67(1)(b).
Toleo la kiingereza ( English version)
1) Subject to the other provisions of this Article, there shall be the following categories of Members of Parliament, that is to say:-
(a)members elected to represent constituencies;
(b)women members being not less than thirty percentum of all the members mentioned in paragraphs (a), (c), (d), (e) and (f) with qualifications mentioned in Article 67 elected by the political parties in accordance with Article 78, on the basis of proportion of votes;
(c)five members elected by the House of Representatives from among its members;
(d)the Attorney General;
(e)not more than ten members appointed by the President from amongst persons with qualifications specified under paragraphs (a) and (c) of subarticle (1) of Article 67 and, at least five members amongst them shall be women;
Ukisoma matoleo yote mawili unaona kabisa kwamba kuna tofauti; kwamba toleo la kiswahili halijaweka mpaka wa uteuzi kwa maana yake ni kwamba Mhe Rais anaweza kuteuwa watu wanaume wote 10 kuwa wabunge wa kuteuliwa. Lakinj toleo la kiswahili limeweka mpaka kwamba katika uteuzi atakaofanya Mheshimiwa Rais angalao watano wawe wanawake.
Huo ni utata mkubwa sana na unapaswa kuangaliwa kwa mtazamo wa kisheria wala si kwa kisiasa?? Je sheria inasema nini hapa pale inapotokea toleo la sheria kwa kiswahili kuwa tofauti na toleo la kiingereza?? Je ni toleo lipi lifuatwe??
Kwa mujibu wa Section 84 ya Interpretation of Laws Act
(1)Lugha za sheria za Tanzania zitakuwa ni Kiswahili au Kiingereza au lugha zote mbili.
(2) Pale ambapo Sheria yoyote imetafsiriwa kutoka lugha moja kwenda lugha nyingine na kuchapishwa kwa lugha zote mbili, na iwapo itatokea mgongano au kutakuwa na mashaka ya maana ya maneno, maelezo, lugha ambayo imetumika wakati wa kupitisha Sheria hiyo na Bunge ndiyo itakayokuwa ya kipaumbele.
Kifungu kilichonakiliwa hapo juu kinaelekeza kwamba iwapo sheria imechapishwa kwa lugha zote mbili na ikatokea mgongano au mashaka katika maneno/ maelezo yaani toleo la lugha moja linakuwa na maana inayokinzana/tofautiana na toleo la lugha nyingine, kinachotakiwa kutumika hapa ni toleo la lugha ambayo ilitumika na Bunge kuipitisha sheria husika.
Swali muhimu sana je lugha ipi basi amabayo ilitumika kuipitisha Katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania???
Katika kesi Daudi Pete v. Republic [1993] TLR 22 at p. 33 mahakama iliweka bayana kwamba; "that the controlling version of the Constitution is the Kiswahili one and not the English version because the Constitution was enacted in Kiswahili." (Maana yake ni kwamba toleo la kiswahili la Katiba ndiyo lenye nguvu na sio toleo la Kiingereza kwa sababu Katiba ilipitishwa katika lugha ya Kiswahili.)
Kwa hiyo basi kutokana na uamuzi wa Mahakama katika kesi ya Daudi Pete pale inapotokea kuna tofauti ya maana au maelezo baina ya toleo la Kiswahili la Katiba na toleo la Kiingereza la Katiba, maana iliyopo kwenye toleo la Kiswahili ndiyo itakayotumika.
Kwa maelezo hayo niliyotoa ni dhahiri kuwa uamuzi wa Rais Mheshimiwa John Pombe Magufuli uko sahihi kisheria wala hauko kinyume na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977.
Copied from somewhere.