USAHIHI wa taarifa za Lwakatare; Mkutano wa hadhara na Press Conference

Tumaini Makene

JF-Expert Member
Jan 6, 2012
2,642
6,070
Kumekuwepo na taarifa zinazosambazwa kwa njia mbalimbali za upashanaji habari tangu jana juu ya vitu viwili ambavyo vyote vinamhusu Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA, Ndugu Wilfred Mganyizi Lwakatare.

1. Kwamba atafanya press conference leo, (watu wale wa upande wa pili wameenda mbali hata wametaja muda eti ni saa 4 asubuhi)

2. Atakuwa kwenye mizunguko ya mikutano ya kampeni katika chaguzi ndogo za udiwani zinazoendelea katika hatua ya lala salama maeneo mbalimbali nchini.

Usahihi.

Kwa kuzingatia masuala kadhaa hasa mikakati ya kitaalam katika mapambano ya kisiasa, hususan katika suala hili, press conferense iliahirishwa tangu jana mapema asubuhi, baada tu ya baadhi ya vyombo vya habari kuwa vimetangaza kuwa itafanyika leo, Alhamis. Tuliviarifu vyombo vya habari hivyo. Imesogezwa mbele na taarifa zitatolewa tena.

Suala la mizunguko kwenye kampeni za uchaguzi mdogo...hakuna kitu kama hicho kwa sasa.

Pamoja na kwamba kuna watu wenye mapenzi mema kabisa na vuguvugu la mabadiliko wamekuwa na hamu ya kutaka kumsikia kamanda mwenzao, ndugu Lwakatare akizungumza majukwaani baada ya miezi mitatu ya 'ukatili' mkubwa, pia tumebaini kuwa watu wa upande wa pili, wanataka sana kujua CHADEMA sasa inajua kiasi gani juu ya njama za kuibambikia ugaidi, utekaji na mauaji.

Hivyo upande huo wa pili, ambao unaonekana dhahiri kuwa under pressure ya kutojua kiasi gani mipango yao inajulikana na itaumbuliwa kwa kiwango kipi, umekuwa ukieneza habari za Lwakatare kufanya mikutano ya hadhara kwenye kampeni za uchaguzi wa madiwani, kitu ambacho si kweli.

Baada ya hila na uovu wa watawala na vibaraka wao kushindwa katika jaribio lingine kubwa kabisa wao kuwahi kupanga dhidi ya wimbi la mabadiliko na kutaka kuzuia kasi ya CHADEMA kuwaondoa madarakani, tumwache ndugu Lwakatare apumzike na familia, wakati mipango makini ikifanywa kwa ajili ya matukio yote mawili ambayo Watanzania wanategemea na kuyasubiri kwa hamu yafanyike; mkutano na press conference.

Kitu kimoja cha uhakika ni kwamba, watu wa upande wa pili, ambao tayari hofu yao inajulikana, hawataweza kumchagulia Lwakatare wala kuichagulia CHADEMA kitu gani cha kusema, kama ambavyo wameanza kufanya kupitia forums mbalimbali. Let tthem cool down, wasiwasi wa nini! Yote yakayosemwa itakuwa ni kwa ajili ya maslahi ya Watanzania, haitakuwa kwa ajili ya kuifurahisha 'status quo'.

Ukweli haujawahi kushindwa na uongo, wala dhuluma haijawahi kuishinda haki. Vyote viwili, ukweli na haki, vinaweza kuchelewa tu, lakini hatimaye huwadia. Kwa sababu Lila na Fila havitangamani.

Makene

0752 691569
 
Asante kwa taarifa mkuu,maana naona upande wa pili mapovu yanawatoka kutupangia ratiba wanazojua wao.....
 
Kamanda Makene.

Hilo ni jambo la maana sana. Kuna uzi ulitoka hapa jamvini wa kupendekeza Kamanda Lwakatare ajiunge na timu za kampeni za udiwani Arusha. ukweli nilipinga kwa nguvu zote.

ni wakati muafaka kwa yeye kupumzika na pia kwa chama kutafakari nini cha kufanya kupambana na hizi mbinu mufilisi za MAGAMBA.
 
pamoja sana kamanda...viva CHADEMA mkombozi wa maskini wa Tanganyika...
 
hii ndo taarifa mkuu, tatizo wa upande wa pili wanafanya kazi za uenezi cdm, sasa leo hii hammy D nae kageuka afisa habari wa cdm, kweli wanaweweseka sana hawa watu.
 
Kwa taarifa tu kwa upande wa pili nakupa BIG UP Tumaini Makene na watu ofisi kuu ya CHADEMA.

Nguvu ya kupambana na propaganda ni "assertive" na "authoritative". Naomba na nashauri isiruhusiwe kabisa thread za akina HAMY D and the likes zitoe taarifa na habari muhimu za CHADEMA bila kuwekwa sawa na CHADEMA.

Mfano mzuri ni thread hii. Nawatakia kila la heri kwa mkakati huu
 
asante mkuu, ila kwenye Facebook wall ya Rwakatale leo amefunguka mwenyewe kuwa atazungumza, labda kama ipo hacked na akina Mwigulu.
 
Hongera kwa kuona madhara ya hili. Lakini sijakuelewa kauli yako kuwa taarifa hizi zimekuwa zikitolewa na upande wapili, Hivi Tanzania daima ni upande wa pili?

Humu JF Kuna makamanda walikuwa wanatoa povu jana kwa tahadhari iliyotelewa kumruhusu mtu huyu kuongea kwa sasa, Makene hao ndio unawaita upande wa pili.

Nilitaraji utoe somo kwa makamanda wenu ukweli kuhusu kesi hii kuwa haijafutwa kama navyoona wengi wakiamini na kuwa dhamana hii haifuti kuwa video ile aliyepigwa picha ni Lwakatare tena nyumbani kwake ili mikakati ya kumunyofoa kwenye ukweli huu iandaliwe.
 
41 Reactions
Reply
Back
Top Bottom