Usahihi wa taarifa ya Stika za Usalama Barabarani huu hapa

N'yadikwa

JF-Expert Member
Aug 10, 2014
6,825
9,532
Kamanda wa Police Traffic nchini Fortunatus Musilim amekanusha taarifa kwamba Stika za Usalama zinalipiwa tzs 8000 na ukaguzi ni 15,000 amesema Stika hizo ni Buku Tano tu 5000 Tzs na mhusika atailipa baada ya gari yake kukaguliwa na Vehicle Police.

Tuache kulishana matango pori jamani...zaidi soma mwenyewe Mwananchi;

Kikosi cha Usalama Barabarani kimesema taarifa inayosambaa kwenye mitandaoni ya kijamii kuhusu ukaguzi wa magari na utoaji wa stika za usalama barabarani haina ukweli.

Kamanda wa kikosi hicho, Fortunatus Musilimu amesema ukaguzi umeanza leo Jumanne, Oktoba 17, 2017 baada ya uzinduzi wa wiki ya nenda kwa usalama uliofanyika jana Jumatatu mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.

Taarifa iliyosambaa mtandaoni leo Jumanne ilieleza stika za wiki ya nenda kwa usalama barabarani hazitotolewa na trafiki barabarani kwa kuuzwa na kwamba, zilitakiwa kutolewa tangu Agosti, 2017 lakini zimezuiwa kwa kuwa mwaka huu kuna utaratibu mpya.

Taarifa hiyo ilieleza kwamba mkaguzi wa gari dogo atalipwa Sh15,000 na wa gari kubwa atalipwa Sh30,000, huku stika ikiuzwa Sh8,000.

Kamanda Musilimu akizungumza na mwandishi wa Mwananchi amesema, “Taarifa hizo si za kweli na aliyekutumia mwambie atafute chanzo cha taarifa kama ulivyofanya wewe. Kwanza, ukaguzi wa magari utafanyika nchi nzima na ni wa lazima.”

Musilimu amelaani taarifa hizo akisema zinalenga kuwachafua. Amesema ukaguzi unafanyika kwa awamu kwa kuhusisha magari ya abiria na magari ya kubeba mizigo.

Kamanda amesema ukaguzi utafanyika katika sehemu husika kama vile kwenye vituo vya mabasi, gereji, vituo vya polisi na sehemu itakayotangazwa na mkoa husika.

“Magari ya mizigo na ya abiria ndiyo yataanza kwa muda wa miezi mitatu ya ukaguzi na ubandikaji wa stika. Hapa tunajumuisha daladala, mabasi ya abiria, malori na teksi. Magari mengine madogo yatatangaziwa muda maalumu,” amesema.

Kamanda Musilimu amesema baada ya ukaguzi na ofisa kujiridhisha, mmiliki wa gari atalipia Sh5,000.

“Maofisa wetu watakuwepo sehemu maalumu iliyopangwa. Kifungu cha 39 cha Sheria ya Usalama Barabarani Sura ya 168 inasema gari linalotembea ni lazima liwe salama, hivyo stika zote zitatolewa baada ya ukaguzi na kupewa fomu ya polisi namba 93 inayoonyesha chombo chako ni salama,” amesema.

Kamanda Musilimu amesema taasisi au kampuni zina nafasi ya kuomba kupatiwa huduma ya ukaguzi katika maeneo yao.

“Mashirika makubwa wanayo nafasi ya kuomba kukaguliwa mahali walipo nasi tutawafuata. Kipindi hicho kikipita operesheni kubwa ya kukamata vyombo hivyo itafuata,” amesema.
 
Back
Top Bottom