USAHIHI: Kuhusu uvumi wa John Mnyika

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
TAARIFA KWA UMMA

Ipo hoja nyepesi mno iliyopikwa na Vijana wa Lumumba juu ya Mbunge wa Kibamba na Naibu Katibu mkuu wa CHADEMA John Mnyika kuwa alimkataa Lowassa

Hoja hiyo ni ya kupuuzwa kwa kuwa haina ukweli wowote ule, na nitalishangaa Jeshi la Polisi kuendelea kukaa kimya,na kumuacha aliepotosha Umma kwa kiwango kikubwa kiasi hicho,jambo ambalo limempa Usumbufu mkubwa Naibu Katibu mkuu kwa chama na Wananchi wake katika jimbo lake.

Nataka kuona nguvu ya Cyber Crime kama kweli sheria hiyo ni dhahiri ni msumeno au huwa inakata upande mmoja tu!.Mnyika ni Kiongozi mkubwa na katika Taasisi kubwa sana nchini CHADEMA,hapaswi kunenewa uongo kwa nia ya kuupotosha Umma naliomba jeshi la Polisi liingie kazini Mara moja kutimiza majukumu yake.

Imetolewa July 03

Edward Simbeye
Katibu Mwenezi BAVICHA Taifa

======

Magazeti ya Leo yaliandika hii habari...

Mnyika matatani

MBUNGE wa Ubungo, John Mnyika, amedaiwa kuwaacha njia panda wadhamini (majina tunayo) ambao walikubali kuidhamini kampuni ya Testa ambayo yeye alikuwa mwenyekiti wa bodi ya wadhamini.

Inadaiwa kwamba Mbunge huyo alichukua uamuzi wa kujiondoa kwenye kampuni hiyo baada ya kuona inashindwa kulipa deni la Sh milioni 300 ambalo linatokana na riba ya mkopo wa Sh milioni 222 ambazo Testa ilikopeshwa na benki ya Standadr Chartered.

Habari za uhakika ambazo MTANZANIA limezipata zinaeleza kuwa kwa miaka mitatu sasa wadhamini hao wamekuwa wakihangaika kutafuta njia ya kujinasua kutoka kwenye deni hilo.

Inaelezwa kuwa nyumba za wadhamini hao ambazo ziliwekwa rehani kupata mkopo huo zipo kwenye hatihati ya kupigwa mnada kufidia deni hilo.

Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari, kampuni ya Testa ilikuwa ikijihusisha na uwakala mkubwa wa masuala ya huduma za fedha kupitia simu za mkononi.

Chanzo chetu hicho kilieleza kwamba Mnyika ndiye aliyekuwa mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa kampuni hiyo na ambaye aliridhia kukopwa kiasi hicho cha fedha katika benki hiyo.

“Mnyika alikuwa mwenyekiti wa bodi ya wadhamini, alikuwa na hisa nyingi kuliko wenzake – ya zaidi ya asilimia 50 – na kwa nafasi hiyo ya uenyekiti saini yake ndiyo ilikuwa inatambulika kule benki ili kuchukua mkopo,” kilieleza chanzo hicho.

Kilieleza pamoja na Mnyika kudaiwa kujiondoa katika kampuni hiyo siku nyingi hata hivyo hakuwasiliana na wadhamini wake na hata benki hiyo kuwaeleza juu ya uamuzi wake huo.

Nyaraka muhimu ambazo MTANZANIA imeziona zinaonyesha kampuni hiyo ilikubaliwa kukopeshwa fedha hizo baada ya kikao cha bodi Januari 25, 2012, Mnyika akiwa mwenyekiti.

“Kikao cha bodi ndicho kilichokuwa na uamuzi juu ya shughuli za kampuni ikiwamo masuala ya kukopa. Januari 25, 2012 wajumbe walikaa na kukubaliana kukopa. Mnyika akiwa mwenyekiti aliidhinisha kwa kutia saini yake Mei 11, 2012 ndipo kampuni ikakopeshwa,” kilieleza.

Nyaraka nyingine kutoka benki hiyo ambazo MTANZANIA imeziona zinaonyesha awali kampuni hiyo ilikuwa ikirejesha vizuri deni hilo, tangu Agosti 31, 2012 hadi Februari 28, 2014.

Nyaraka hizo zinaoneysha kuanzia Machi 31, 2014 kampuni ilishindwa kurejesha fedha zozote hadi kufikia Julai 31, mwaka huu ambao ndiyo ulikuwa mwisho wa kurejesha mkopo huo.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, wadhamini hao walikuwa wakifuatilia maendeleo ya kampuni hiyo kwa mmoja ya wakurugenzi (jina tunalo) na walikuwa wakijibiwa kuwa kampuni inaendelea vizuri.

“Miezi sita baada ya kuzungumza na Mkurugenzi huyo, benki ilituma wawakilishi wake kwa wadhamini na wakakabidhiwa barua ya kuwajulisha kuwa deni halijalipwa na nyumba zao zitapigwa mnada kulifidia,” kilieleza.

Chanzo hicho kilieleza kuwa kutokana na hali hiyo, mmoja wa wadhamini hao amekwisha kufanya juhudi za kukutana na viongozi wa ngazi za juu wa Chadema, chama ambacho anatokea Mbunge huyo kutafuta ufumbuzi wa suala hilo.

“Alishawahi kumfuata Dk. Willbrod Slaa (alipokuwa Katibu Mkuu wa Chadema), Freeman Mbowe (mwenyekiti) na hivi karibuni ameenda kuomba kuonana na Edward Lowassa (Mjumbe wa Kamati Kuu) na iwapo hatafanikiwa yeye na mwenzake wamepanga kuchukua hatua nyingine ambazo hawajaziweka wazi,” alisema.

MTANZANIA ilipomtafuta Mnyika kwa simu kuzungumzia suala hilo simu yake iliita bila kupokewa na alipotumiwa ujumbe mfupi wa maandishi alijibu baadhi ya maswali kama ifuatavyo;

MTANZANIA: Habari mheshimiwa, naitwa… kuna taarifa kuwa nyumba za wadhamini wako zinapigwa mnada kwa sababu umeshindwa kurejesha mkopo wa zaidi ya Sh milioni 200, nini kauli yako juu ya tuhuma hizi?

Mnyika: Hakuna mtu yeyote aliyeweka nyumba kunidhamini waulize wakuambie ukweli.

MTANZANIA: Kuna nyaraka ambazo tunazo moja ikiwamo ya makubaliano ya bodi ya wakurugenzi ambayo wewe ulisaini ukiwa mwenyekiti na ilionyesha wadhamini sita zikiwamo nyumba mbili zilizopo Bunju na Mmbweni.

Mnyika: Iliyokopa ni kampuni si mimi na niliondoka kwenye hiyo kampuni tangu mwaka 2013 bila kupokea fedha yoyote binafsi… hivyo ni vizuri ukawatafuta wenye hiyo kampuni kuwauliza na waulize pia hao wadhamini walinufaika vipi na hiyo mikopo na nani aliwafuata waweke hati zao.

MTANZANIA: Mheshimiwa wewe ulikuwa nani kwenye hiyo kampuni, wajibu wako ulikuwa upi na uliondoka vipi na nani ni wamiliki wa hiyo kampuni?

Mnyika hakulijibu swali hili na alipoombwa kupigiwa hakujibu. Vilevile, alipopigiwa simu yake iliita bila kupokelewa hadi gazeti hili linakwenda mtamboni jana usiku.

Chanzo: Mtanzania
 

Attachments

  • Screenshot_2016-07-03-18-39-45-1.png
    Screenshot_2016-07-03-18-39-45-1.png
    11.8 KB · Views: 160
Hivi mnawashwa na ninI? Si tumewaachia nchi mtawale mnavyopenda. Dola mnayo, hazina mnayo, matrillion mliyoyaficha uswis na kwingineko bado yapo salama na matrillion ya maden mliyosababisha kwa kuiba tunawalipa na hata tukifa watoto na vizazi vijavyo watawalipia. Licha ya yote hayo badoo tuu. MNABOA
 
Hay a wanaCDM hebu tujalieni ukweli wa hiyo statement kama iko sawaa ama laaa..inaenezwa kwenye magroup ya wassap. Angalizo mpaka iwe imehakikiwa na wahusika ndo tuanze yale maneno yetu yasiyo na busara kama nijuavyo JF. Kwa yenye busara yaanze sasa hivi....
Hata kama ni kweli Mnyika kasema hayo lakini wanaCDM wakija hapa watageuka leo na kumponda tena Mnyika kua na yeye kalishwa,hua hawakosi cha kusema
 
Lowassa atarudi tu CCM...nadhani wabunge vijana wa Chadema wamevumilia vya kutosha sasa hawaoni faida yoyote ya kuwa naye tena..Biashara ya uchaguzi imeisha...kila mtu atarudi alipotoka..Juzi kati Lipumba alianza kijirudisha..
 
Sawa sawa mnaweza kuandika lolote mnalotaka ila hakuna Mnyika mpuuzi kiasi hicho. Maccm mmekaa mda mrefu bila kutibua amani UKAWA hivyo mnadhani propaganda zenu zitasaidia.
Kaushauri tu;
Laiti ccm mngejikita zaidi kwenye maongozi yawezayo kuleta maendeleo kwa taifa mkaonesha uwezo wa kuliongoza taifa kuelekea kwenye mafanikio wala si kulitikisa taifa kwa kuminya demokrasia.
Hakuna na nasema hakuna Mtanzania asiyeona mambo mema mnayofanya, hakuna mtu anayetaka kuambiwa kuwa hili ni zuri au hili ni baya. CCM mkitenda mema mtatawala milele, ila mkiendelea kuminya demokrasia, mtaendelea kutawala bila ridhaa ya watawaliwa.
Tendeni mema, acheni kutumia watu kudidimizza upinzani. Tutawaangalia hao wapinzani, tutawapima na mwishoni tutawapa haki yao wanayo stahili. 2020 is not far, tumuunge mkono rais akiinue chama kilipotumbukia si kwa migongo ya watu.
 
Hapo sawa naona kitengo cha propaganda kwa upande wa CDM wanataka kuharibu mambo...source haikuwa nzuri wajua makundi ya wassap na yenyewe. Nadhani atafika hapa Mnyika akanushe au kina Makene nk...
 
TAARIFA KWA UMMA

Ipo hoja nyepesi mno iliyopikwa na Vijana wa Lumumba juu ya Mbunge wa Kibamba na Naibu Katibu mkuu wa CHADEMA John Mnyika kuwa alimkataa Lowassa

Hoja hiyo ni ya kupuuzwa kwa kuwa haina ukweli wowote ule, na nitalishangaa Jeshi la Polisi kuendelea kukaa kimya,na kumuacha aliepotosha Umma kwa kiwango kikubwa kiasi hicho,jambo ambalo limempa Usumbufu mkubwa Naibu Katibu mkuu kwa chama na Wananchi wake katika jimbo lake.

Nataka kuona nguvu ya Cyber Crime kama kweli sheria hiyo ni dhahiri ni msumeno au huwa inakata upande mmoja tu!.Mnyika ni Kiongozi mkubwa na katika Taasisi kubwa sana nchini CHADEMA,hapaswi kunenewa uongo kwa nia ya kuupotosha Umma naliomba jeshi la Polisi liingie kazini Mara moja kutimiza majukumu yake.

Imetolewa July 03

Edward Simbeye
Katibu Mwenezi BAVICHA Taifa
Huyo Mnyika ameshawasilisha malalamiko yake polisi kwamba kanenewa uongo?
 
Back
Top Bottom