USAHIHI: Kilichotokea kati ya Juliana Shonza na Wabunge wa Upinzani kwenye viwanja vya Bunge, Dodoma

Kuna vilaza waliobarikiwa kuwa vilaza na wakaupokea ukilaza kwa moyo mkunjufu na vigeregere wanaangalia zile picha, still photos za tukio lilivuoyokea na wanafanya hitimisho kuwa Juliana ndo hakuwa sahihi.
Sasa kama ulikuwa hujifahamu ulivyo, hii ndio description halisi ya wewe ulivyo .... !
 
Wanajamvi,

Kwa muda sasa nimekuwa kimya sana kuchangia na kushiriki mijadala mbalimbali inayoendelea kwenye jamvi letu hii ni kutokana na majukumu yanayonikabili ikiwemo kazi pamoja na shule.

Nalazimika kurudi tena jukwaani kutolea ufafanuzi wa kile kilichotokea jana katika viwanja vya bunge kwani nimepokea simu nyingi na ujumbe mbalimbali, na kwa maelezo yao nimegundua kuwa upo upotoshaji mkubwa wa kilichotokea na kinachoendelea. Katika hali kama hiyo busara yangu ikaniongoza kuja kulitolea ufafanuzi.

Mtakumbuka kuwa siku ya jumatatu ya tarehe 5 June, 2017 Bunge liliazimia kumsimamisha Mbunge Halima Mdee kwa kipindi cha Mwaka mmoja, na azimio hili lilitokana kwa kiasi kikubwa na hoja yangu ya kutaka Mhe Halima aongezewe adhabu ambayo mara ya kwanza ilikuwa ni ndogo na isiyofanana na aina ya makosa aliyoyafanya. Kitendo hicho kiliwaghadhibisha wabunge na viongozi wa CHADEMA, hivyo wakakutana mjini Dodoma na kupanga mikakati ya kunidhuru.

Kama kawaida nikapata taarifa hizo mapema sana hata kabla ya kikao chao hakijaisha nami nikachukua hatua ya kwenda kuripoti katika vyombo vinavyohusika na Ulinzi na Usalama wa raia kuwa upo mkakati wa aina hiyo, hatua hiyo iliwafanya washindwe kufanikisha mkakati wao. Hivyo tangu hapo wakawa wanafikiria mbinu nyingine za kutaka kunishughulikia.

Kilichotokea jana ni matokea ya kufeli kwa mipango yao ya kidhalimu dhidi yangu, jana walidhihirisha wazi wazi kilichomo ndani ya vifua vyao juu yangu. Jana, nimeshambuliwa, kwa mara nyingine tena nimetukanwa na kudhalilishwa tena ndani ya viwanja vya bunge.

Nimesikitishwa na vijana waliotumwa kuja kunishambulia, hawakuja kwa bahati mbaya bali ni sehemu ya maelekezo waliyopewa, nao kama kawaida bila kufikiria athari ya maelekezo hayo wakaamua kuyatekeleza na kuja kunishambulia na kunidhalilisha, tena wengi ni wabunge Vijana ambao mimi siku zote nimekuwa nikiwaheshimu na kuwafanya wenzangu, nikiamini kuwa Viongozi Vijana tuna mzigo mzito mabegani mwetu wa kuongoza kizazi cha leo na kesho, na ili tufike mbali hatuna budi tutembee na kizazi chetu na tushirikiane baina yetu. Inasikitisha kuona Vijana kwa mara nyingine tena wanakubali kutumwa kumshughulikia kijana mwenzao. Taarifa kuwa nimeshambuliwa na watu wazima hazina ukweli wowote, ni vijana waliotumwa.

Naomba niwakumbushe jambo moja, miaka 5 iliyopita nikiwa na umri wa miaka 25 tu nilikuwa na UJASIRI wa kupambana na aliyewatuma jana, i dare to stand against ur so praised DEMIGOD, and i made my way out victoriously.

Naandika historia yangu kwa mkono wangu, U should always be alarmed and alerted mkitumwa kushughulika na mimi, i have never been soft in my life, go easy on urself. Wapo wanaoitengeneza historia, kuna wanaoiandika na wapo wanaoitazama historia ikitengenezwa na kuandikwa.,mmeamua kuendelea kubaki watazamaji.

Ingefaa zaidi kushughulika na Chama chenu kuliko kushughulika na JULIANA, i am just UNBREAKABLE.
Hapa sijaelewa! Huu ni ufafanuzi wa kilichotokea au ni ujumbe kwa Chadema kuwa wewe sio wa mchezo mchezo na wakishasoma wakukome au mimi ndio sijui kusoma???
 
Yaani kama ni uzushi,ccm mmefuzu !.
Roho mbaya kiasi hiki
nakutafutia wanawake wenzio,mlango wa jela,
ukiwa bado wewe ni ke
na unao au utapata wato
to,huoni kama unajenga laana kwa mikono yako mwenyewe,itakayo,tafuna uzao
wako baadae ?

Ila kama una huo moyo,
jitahidi.mavuno yake,ya
taonekana na viumbe wote,watakao kua hai,
wakati huo.nakutakia
heri,katika kazi uliyotumwa yakuangamiza upinzani
Tanzania.Mungu usiyed
hihakiwa,na uliyekuepo,
Ukishudia hili tukio,Uliye
muona huyo ccm na hao wa upinzani,kazi yako sio
kuharibu,ila nikutengeneza.naomba,
Utengenezaji wako,ukatamalaki katika
pito hili gumu la hawa wa
mama wa upinzani,itoshe tu nikushukuru nikiamini
kua wewe ndiwe Mungu wa
kweli na haki,Amen.
 
Halafu linajiamini hili. ...kwani ni nani nchi hii. ...tukuamini wewe kwa lipi kwani hapa mahakani. ...subiria kesi yako huko tuondolee balaa hapa
 
MBUNGE CCM AZUA TAFRANI
Nimejaribu kutafakari mada aliyoileta mbunge wa kuteuliwa dhidi ya Mbunge wa kuchaguliwa sipati picha. Nadhani hawa wateuliwa wa chama "twawala" kuna namna inatumika ili wateuliwe. Nina shaka sana kwamba "WANATUMIKA" sana kabla ya uteuzi. Ikiwa hayo yaliyoandikwa gazetini ndivyo kisha Mh. Kubenea anashtakiwa basi tuna safari ndefu nchi hii kuelekea kwenye HAKI na DEMOKRASIA.
 
Unashangaa vijana kumshughulikia kijana mwenzao..!! Wewe ulivyowashughulikia akina Halima ndani ya Bunge, wenyewe ni wazee!!! Jifunze heshima kwa watu wote.
 
Mwanamke yyt anayejichubua ana matatizo ya kisaikolojia. Huwa namdharau mwamake yyt yule anayejichubua rangi yake nyeus ili awe mweupe. Mtu wa hivi huanza kujidharau na kujiona hana thaman akiwa na rangi yake halisi, huamua kujibadirisha kwa kujichubua na kuwa mweupe. Mtu wa aina hii lazima awe hajiamin. Wewe Juliana Shonza nilishakudharau tangu nilipoona umejichubua. Mtu yyt wa aina yako ana mapungufu kwny kufikir kwake.

Back to the topic, ulichoandika sio usahii, ni blah blah tu...
 
Hata kama ni mimi madelu system ningeosha rungu na kukimbia.Siwezi kukaa na mwanamke wa design hii.Ni aibu sana.
 
Ushauri wangu kwako kama ndugu dada, mdogo wangu na mtanzania mwenzangu: Nafasi tulizopewa katika maisha yetu tuzitumie vizuri hasa pale tunapo kwenda kumwabudu mungu muumba wa mbingu na nchi. Mtangulize mungu achana na kibuli na malingo, Mungu ni mwaminifu kila wakati. Unatumia nafasi yako vibaya na huenda ukaja kuijutia kwa kujiuliza" kwanini sikuwa mnyenyekevu kwa wale wenye kunyanyua ndimi zao za upanga" Tubu na umrudie mungu wako.
 
Account ya @julianashonza imekuwa hacked humu Jf hawezi andika upuuzi kama huu
 
Back
Top Bottom