Usafirishaji parcels kwa njia ya mabasi ya Zuberi ni tatizo

chipuluma

New Member
Nov 25, 2021
1
0
Jamani yaani hawa Zuberi ni tatizo kama utapotrlewa na mzigo.

Basi mwezi wa kumi si nikatumiwa mzigo toka Dar

Yaani mzigo ulifuatiliwa mwezi mzima na haukupatikana

Boss wao yule zuberi mwenyewe ana kiburi cha kimataifa! Hana ushirikiano kabisaaaa

Nawashauri mnapotumia mabasi ya zuberi kutuma mizigo yenu muwe mmeshajitoa muhanga kama ukipotea itakua historia

Na nasikia kuna mchezo wanafanya hao ma agent kule Dar

Kuna agrnt mmoja pale Kariakoo anaitwa deo huyu ukituma mzigo bila kulipa pesa eti utalipiwa na mpokeaji huwa anaificha mizigo na kuiuza

Yaani hawa jamaa ni tatizo kubwa sana.
 
Kusafirisha parcel na basi n hatari aisee.Mm juzi nilisafirisha mzigo wa 2.5m kutoka dsm. Aisee nilipoona masharti ya tiketi sikulala usiku mzima.

Yaan chochote kikitokea kwenye mzigo hawahusiki.

Napoenda kuifuata nakuta mzigo wameweka nje na ni electronic device nikawaza ingenyesha mvua hapa nilikuwa nimeisha.
Hawa jamaa mteja kwao ni fala
 
Hao zuberi nilichoka siku nimepanda basi lao natoka Mwanza kuja Dar wahudumu ni wahuni hawana sare wanalala stendi wachafu hawanawi uso muda wote wanawaza kupiga madili tu lakini jamaa kwa kununua mabasi mapya yuko vizuri hakaagi na mabasi mishipa tatizo watenda kazi wake
 
Msiharibu jina la kampuni kwa uzembe wa watu wachache.

Zuberi na miongoni kwa makampuni yanayofanya vizuri katika usafirishaji, wana miaka zaidi ya 20 kwenye transportation industry.
 
Back
Top Bottom