Usafirishaji mahindi kwenda Kenya kiholela kutoka mji wa Himo

dicaprio

Member
Dec 18, 2010
59
10
Niko hapa Himo usiku huu, Fuso kadhaa (zapata 30 hivi ) zinajiandaa kupeleka mahindi kupitia Kitobo eneo la kusini mashariki ya mji huu na nyingine zikipita njia ya Rombo na Holili. Serikali imesahau kwamba mahindi yamesafirishwa kwa takriban mwezi na nusu sasa mahindi yakianikwa na kupimwa mwa mizani ili kupatikana kilo 100. Wapo wahudumu wa kijiji hiki wanaojishughulisha na kukusanya ushuru ingawa siyo rasmi na si OCS wala ngazi yoyote inayoliona hili la kuondoa nafaka kwa kasi. Tayari hali ya njaa itajiri ingawa ni wazi hata soko la Himo sado ya mahindi sasa ni shilingi 2300 na raia wakishindwa kumudu ilhali majirani wanaofika sokoni hapa Jumatatu na Alhamisi wakishambulia bidhaa hii kwani wana uwezo wa soko. Wana JF naomba niwataarifu hili jambo
:angry:
 
Mikoa ya kaskazini inakabiliwa na ukame ambao utasababisha janga la njaa. Jana nimepita hapo mizani Himo,nimeona malori makubwa yakiwa yamejaa magunia ya mahindi yakiteremshwa na kupakiwa ktk mafuso.
 


sasa ninaomba nikutaarifu wewe , ni kwamba mambo haya yalishaanza kutendeka miaka kumi iliyopita.
 
do you support or condemn ....?

Let our smallholder farmers access market! This is still an issue in the Mkweeere's country!

Because NFRA has failed to show the way. We expected this agency to be a lead organ in supporting our farmers who are struggling for the market but in vain! Now, if Kenyan are paying super prices that is good, but our farmers should be educated not to sell all their produce, allow them to sell the surplus (that is what our local governments are supposed to do).

Wacha Mangis watengeneze pesa!!
 

Mimi ni Mkulima na hili swala la kuzuiwa kuuza mazao nje linaniuma sana unahangaika kuinvest vipesa vyako na kushinda umepiga magoti kuomba Mungu mvua inyeshe serikali huwa inakuangalia tu halafu ukivuna wanakupangia pa kuuza bila kujali bei ya kuuzia kuna umuhimu wa serikali kuanza kununua mahindi ya wa kulima kwa bei nzuri kama njia mojawapo ya kuwasubsidize wakula badala ya kumwaga askari mipakani kukamata malori that's very unfair nchi zenye serikali serious ndivyo wanavyofanya kuwasaidia wakulima na pia kuepusha baa la njaaa
 
jamani kulima tulime sie halafu pakuuza mtupakie nyie. Kwa nini mnatunyanyasa wakulima? Badala ya kuhakikisha chakula kinazalishwa cha kutosha ili kuwanyanyua wakulima kutoka kwenye umaskini mnaendelea kuwakandamiza na sheria zenu mbovumbovu. Ndo mnategemea wawekezaji wakubwa watawekeza kwenye kilimo cha nafaka kwa staili hii?
 
That is good,wacha wauze sana tu wakusanye yote wauze..nasema hivi sababu mkulima ananyanyaswa sana,serikali imeshindwa kununua kwa bei halisi ndo maana vijana wanakimbilia mjini,wanaachana na kilimo kisichokuwa na tija..heri wauze kuliko yawaharibikie,heri wauze waweze kutumia fedha wanazopata kwa kujengea,kukuza mitaji,kulipia watoto ada n.k...kamwe wananchi hawatopata njaa kwa hilo bali ni changamoto na kilimo kitakua pele mazao yatakapopatiwa soko bora na la uhakika,hata mimi nitawekeza kwenye kilimo kama soko lipo...
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…