Usafiri wa wabunge kuelekea Bungeni Dodoma mwaka 1984! kumbe inawezekana!!

wamoro

Member
Sep 16, 2009
62
16
Wada katika pitapita zangu nimekutana na hiki kitu,hivi hata sasa haiwezekani kufanya hivi kwa masilahi ya masikini wa taifa hili??
 
Attachments

  • 425380_289803211087334_100001729730344_785479_1350693144_n.jpg
    425380_289803211087334_100001729730344_785479_1350693144_n.jpg
    95 KB · Views: 1,307
JK akiamua kuweka masrahi ya Taifa mbele inawezekana na Posho anaweza shusha mpaka Tsh.50,000/= na wakawa wanalala Guest za Tsh.7000/=
 
JK akiamua kuweka masrahi ya Taifa mbele inawezekana na Posho anaweza shusha mpaka Tsh.50,000/= na wakawa wanalala Guest za Tsh.7000/=

Wabunge wa kileo wamevimba matumbo, kwa mlango wa basi hawapiti . . .
 
Kiongozi wa shughuli za serikali Bungeni alikuwa Edward Morengi Sokoine kabla ya kufa katika ajali April 1984 !!!
 
Wabunge wa kileo wamevimba matumbo, kwa mlango wa basi hawapiti . . .

Serikali ikiamua linawezekana basi tu uzembe wa serikali yetu isiyo sikivu, enzi za mzee Julius mbona yalikuwa yanawezekana haya.
 
Matatizo yote haya ya posho ni kutokama na wabunge kuendekeza starehe pindi wawapo bungeni.
Usiku kucha wanashinda chakonichako, wingine wakiwa na malaya kwenye guests na kumbi za muziki. Ikifika asubuhi wanaenda kulala tu pale mjengoni, wengine wanasingizia wamekunywa dawa, kumbe ni starehe za usiku tu!
 
Hizo ndiyo enzi za mwalimu bwana......! alibana matumizi ya wakubwa yule mzee bwana hadi akawa anaweza kusomesha wanfunzi vyuo vikuu bure, usafiri wa treni reli ya kati na Tazara ulikuwa timamu matibabu yalikuwa bure..daftari likiisha shuleni lililoisha linacchanwa kidogo unapewa jipya!!!!!
Mwalimu angekuwa ndiyo raisi kwa sasa nchi yetu ingepiga hatua sana maana sasa kuna mahela mengi yanaishia kwenye mikono ya mafisadi.... na walafi wengine wakiwamo wabunge!
 
Hapo wakipanda komba, mchungaj lwaka, si gar tayar tani zimetimia watamuweka na bi kiro.

mibunge yenu ilivyozoea anasa ipande basi weeh thubutu watanuniana humo bungen na sijui hata kama miswada itapita.
 
Wada katika pitapita zangu nimekutana na hiki kitu,hivi hata sasa haiwezekani kufanya hivi kwa masilahi ya masikini wa taifa hili??

JAMAA WAMEITOA MBALI HII NCHI NA WALIKUWA NA NIA YA DHATI KUPIGA HATUA ZA FULL INDEPENDENCE. ONA TOFAUTI YA WABUNGE WETU ILIVYO

kenya bungeni

KENYAS.jpg

uk bungeni
ukuk.jpg

tz bungeni
tz bunge.jpg

wasira ana haki ya kusinzia bungeni
 
Kwa ubinafsi wa wabunge wetu wa leo wakiambiwa wafanye hivi watapiga kura ya kutokuwa na imani na serikali iliyo madarakani.
 
Jaribu kutafuta nyingine inayoonyesha jinsi walivyokuwa wanazungukia wananchi wa majimbo yao ya uchaguzi. Hii ya kuelekea bungeni ni nzuri.
 
Wakati huo viongozi walikuwa kwa wito na wapo kimaslahi ya wengi lakini leo hii wapo kibiashara zaidi.

Makinda alikuwepo wakati huo kwanini asitumie uzoefu wake? au Leo ndio uheshimiwa sana?
 
Samahani wakuu,
Hivi mwaka 1984 kurudi nyuma, Rais wa Tanzania alikuwa nani vile!
 
Samahani wakuu,
Hivi mwaka 1984 kurudi nyuma, Rais wa Tanzania alikuwa nani vile!

Alikuwa Rais wa Ukweli Mwl. Julius Kambarage Nyerere... Alistaafu kwa hiyari mwaka 1985. Mzee Ruksa akashika kijiti.. Japo JKN alipenda arithiwe na Dr. Salim A. Salim.
 
Alikuwa Rais wa Ukweli Mwl. Julius Kambarage Nyerere... Alistaafu kwa hiyari mwaka 1985. Mzee Ruksa akashika kijiti.. Japo JKN alipenda arithiwe na Dr. Salim A. Salim.

Na laaana hiii ndio inatutafuna sasasaasasasa, na kuna mijutu ikamwita hizibur, sijui na nininhasa hiyo izibu mpaka asiwe mtawala wa tanzania
 
Hizo ndiyo enzi za mwalimu bwana......! alibana matumizi ya wakubwa yule mzee bwana hadi akawa anaweza kusomesha wanfunzi vyuo vikuu bure, usafiri wa treni reli ya kati na Tazara ulikuwa timamu matibabu yalikuwa bure..daftari likiisha shuleni lililoisha linacchanwa kidogo unapewa jipya!!!!!
Mwalimu angekuwa ndiyo raisi kwa sasa nchi yetu ingepiga hatua sana maana sasa kuna mahela mengi yanaishia kwenye mikono ya mafisadi.... na walafi wengine wakiwamo wabunge!

Mkuu Kisigino kuna watu huwa wanaona hilo haliwezekani !
 
Back
Top Bottom