Usafiri wa umma watakiwa kubeba abiria kwa idadi ya viti 'Level Seat' ili kupambana na mlipuko wa Virusi Corona

kunguni wa ulaya

JF-Expert Member
Mar 16, 2014
4,132
6,100
Katika mikakati ya kupambana na ugonjwa wa Corona (Covid-19) serikali kupitia Jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani linasimamia kuhakikisha kila gari ya abiria inabeba abiria kulingana na idadi ya siti zilizopo.

Mfano leo huku Wilaya ya Kigamboni ikitokea daladala imejaza zaidi ya uwezo wake na wengine kusimama, wote waliosimama wanaamriwa kushuka na kusubiri usafiri mwingine.

Pia soma > Waziri Kamwelwe atangaza mkakati wa kupambana na ugonjwa wa Coronavirus kwenye vyombo vya usafiri

----
Habari wakuu, natumai huko muliko hali zenu ni nzuri na mmechukua tahadhari madhubuti dhidi ya Corona

Hakika corona imeleta mabadiliko katika nyanja nyingi, mabadiliko hayo nayaona yakiwa na faida katika sekta ya usafiri wa umma ndani ya jiji la Dar es salaam

Hapo awali iliaminika kwamba Dar bila daladala kusimamisha abiria haiwezekani, sasa korona imefanya hili swala limewezekana

Kila kitu kinapoanza kinachangamoto zake, tumeahuhudia changamoto kubwa ya usafiri imeibuka kutokana na gari zote kubeba abiria level seat lakini naamini hali itazoeleka serikali ikisema hali hii iendelee hata baada ya korona

Watu wanaosafiri ni wengi kuliko mabasi ndani ya jiji hili, hii naona ni fursa kwa wawekezaji kununua basi nyingi kuweza kuenda na hitaji la abiria

Pia serikali angalau ingeongeza bei kwa daladala kwa route iliyokua 400 iwe 600, route ya 600 iwe 800 hii itasaidia kwa wamiliki, madereva na makondakta kupata faida ya kuendesha maisha yao kila siku

Chondechonde, serikali ya nchi hii tunaomba mutangaze wazi kwamba hata baada ya korona usafiri kwa level seat ndani ya jiji ni lazima na uendelee, kwa sasa faini ya 30000 mnayotoza madereva wanaokyuka ni ndogo, inatakiwa iongezwe mpaka 50000 hii itawafanya waheshimu!

Level seat ndani ya jiji inawezekana
 
Ni bora serikali wafanye wasitishe watu wote wasiende makazi hili kuepusha kuenea kwa ugonjwa wa corona kuliko kuzuia usafiri wa umma uwe level seat. Leo kuna adha kubwa ya usafiri kwa sababu ya level seat. Ni hatari sana kwa maendeleo ya uchumi

kitochi
Sasa huoni kwamba wakisitisha kabisa athari kiuchumi ndio itakuwa kubwa zaidi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katika mikakati ya kupambana na ugonjwa wa Corona (Covid 19) serikali kupitia jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani linasimamia kuhakikisha kila gari ya abiria inabeba abiria kulingana na idadi ya siti zilizopo.
Mfano leo huku wilaya ya kigamboni ikitokea daladala imejaza zaidi ya uwezo wake na wengine kusimama, wote waliosimama wanaamriwa kushuka na kusubiri usafiri mwingine.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa route ya Ferry-Machinga complex ina daladala chini ya 10 siitakuwa balaa!
 
Kisemvule-posta ngoma level seat.
Tuombe maambukizi yasiongezeke.
Yakiongezeka ni mwendo wa kukaa ndani tu
 
Ni bora serikali wafanye wasitishe watu wote wasiende makazini ili kuepusha kuenea kwa ugonjwa wa Corona kuliko kuzuia usafiri wa umma uwe level seat.

Leo kuna adha kubwa ya usafiri kwa sababu ya level seat. Ni hatari sana kwa maendeleo ya uchumi

kitochi
Unataka look down sio bure ww

god is good
 
Hayo yote kupoteza mda serikali bado ijafanya kazi yake ya kuzuia kuenea kwa gonjwa hi la covid 19, distancing inayo hitajika ni mita moja kutoka mtu kwa mtu......

Sent using Jamii Forums mobile app
Naona jana baadhi ya misikiti imeshaanza kufungwa. Wakichukua hatua kuepusha mikusanyiko.


Huu msikiti upo Posta karibu na Hindu mandal hospital.
20200330_132459.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom