Usafiri wa umma watakiwa kubeba abiria kwa idadi ya viti 'Level Seat' ili kupambana na mlipuko wa Virusi Corona

Habari ya asubuhi.

Kichwa kama kinavyosema serikali iendelee na huu utaratibu wa level siti ukweli Umesaidia sana kwenye ishu za usalama na mlipuko wa magonjwa mengine yanayoambukiza kwa njia ya kugusana na hewa mbali na hiyo korona.

Tangu umeanza huu utaratibu ukweli ustaarabu umeimarika sana ndani ya daladala kuanzia abiria mpaka konda na dereva wake.Pia usalama wa abiria na mali zao umeamarika mara dufu kwa sasa mtu unajisikia huru kabisa hata hewa inakua safi.

Ingawa changamoto zipo lakini nina amini mwanzo mgumu baada ya muda tutazoea na magari yatakua mengi hivyo tabu itaisha.Hapa sasa naomba serikali iwadhibiti trafiki njiani waache kunyanyasa daladala na kuomba rushwa hili litaharibu utaratibu huu maana itawalazimu konda na dereva kujaza abiria mpaka kusimamisha ili kufidia.

Nawasilisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom