Usafiri wa Umma Dar: Nafasi ya wanasiasa na watendaji

double R

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
2,398
2,538
Mara ya kwanza kufika Dar nikiwa mtoto mdogo nilipatwaa na hisia mchanganyiko. Niliona barabara pana kwa mara ya kwanza, magari mengi,magorofa mengi na taa za barabarani vilinivutia sana. Tatizo tu ilikuwa kero kusafiri kwa daladala na joto. Niliuliza maswali kwa mama mbona magari mengi lakini watu wanagombania na kubanwa sana? Mama alinijibu watu ni wengi na hayatoshi.

Miaka zaidi ya 20 leo, Dar es salaam ina tofauti sana na miaka ile. Mji umepanuka, vitu na watu wameongezeka sana. Kuna mabadiliko mengi yanayoonekana na yanavutia kwa macho. Tofauti hata ya miaka 3 nyuma iko wazi. Dar es salaam jiji linakua kwa kasi.

Ambacho hakijabadilika na pengine hali ni mbaya ni hali ya usafiri wa umma. Idadi ya magari imeongezeka ingawaje mengi hayako katika hali nzuri. Barabara zimeongezeka na njia zimeongeka lakini mpaka leo tunagombania magari.

Kuna sehemu Tanzania miaka hiyo magari yalikuwa hayafiki leo yanafika na wanapanda kwa staha. Dar kuliko endelea kabla watu bado wanagombania gari.

Nimewatafakari hawa muuguzi wa Muhimbili ambaye miaka yote anaenda kazini kwa usafiri, mhudumu wa ofisi ya serikali ambaye ofisi yao haina gari,
Mtoto aliyeanza kusoma shule ya msingi hadi chuo akiwa hapa, mfanyabiashara wa karume kwa miaka 5 haya ndo maisha yao ya kila siku.

Watumiaji wa usafiri huu ni wengi sana. Lakini inaonekana siyo serikali au wenyewe hawajali hii hali. Inawezekana watu wameamini hii ndio stahiki yao kusafiri kidhalili mkiwammebanana kama taka kwenye gunia.

Traffic police wa dar hili kwao si tatizo. Ukizidisha mzigo kwenye usafiri wako binafsi utakamatwa lakini si daladala.

Sumatra kwao hili si tatizo. Viongozi wa mji huu kutwa wanasemea barabara au matengenezo ya barabara au miundo mbinu ya kisasa ya barabara na si hali ya abiria.

Dar ina wabunge wengi na madiwani wakutosha lakini wao wanaongelea umiliki wa UDA na si hali ya wasafiri.

Mwendokasi ilihadithiwa kuwa itakuwa suluhisho, imeondoa foleni lakini udhalilishaji ule haujatoka.

Kama wakazi wa dar ambao wengi wamesoma hadi darasa la saba na vidato wanatendewa hivi seuze huko ambako hawapo.

Haihitaji PHD kujua kuwa hili si sawa. Na si kweli kuwa miji yote yenye watu wengi na kipato kama chetu hali ni hii.
Hapo Nairobi tu kuna unafuu na SA hali tofauti kabisa.

Nadhani ni wakati muafaka wakazi wa jiji hili kuongelea vipaumbele halisi kwenye siasa na kwa watendaji.
Kama kuna fedha za kutindua barabara kila mwaka, kama kuna tunakopa kwa ajili ya mwendokasi basi tunaweza kutatua na hili. Si sawa kuwa kuongoza kwenye rekodi za makusanyo ila maisha yenu ya kila siku yakawa hayaguswi kwa zaidi ya miaka 20 na tukaona tunaendelea.
Hadithi za uchumi kukua na maisha bora hazijayagusa maisha ya watu wa dar wasio na uwezo wa kununua gari.
Mimi nimeona niseme, msikie sio sawa. Kama ni kuwanyima kura nalo ni sawa.
 
Barikiwa sana, umeongea kilichokua akilini mwangu. Jana asubuhi nilishuhudia wakazi wa jiji la Dar wakigombania daladala, inasikitisha sana. Hali ni mbaya sana ni bora kuwepo hata njia za watembea kwa miguu watu watembee kuliko kinachotokea.

Waandishi wa habari wanaweza kusaidia kwenye hili, watengeneze makala ionyeshe hali ya usafiri ilivyo, labda viongozi na wengine ambao hawajui adha wanayopata wananchi wa kawaida wataweza kujifunza kitu.

Wakazi wa Dar wana mateso makubwa sana kwenye usafiri.
Mara ya kwanza kufika Dar nikiwa mtoto mdogo nilipatwaa na hisia mchanganyiko. Niliona barabara pana kwa mara ya kwanza, magari mengi,magorofa mengi na taa za barabarani vilinivutia sana. Tatizo tu ilikuwa kero kusafiri kwa daladala na joto. Niliuliza maswali kwa mama mbona magari mengi lakini watu wanagombania na kubanwa sana? Mama alinijibu watu ni wengi na hayatoshi.

Miaka zaidi ya 20 leo, Dar es salaam ina tofauti sana na miaka ile. Mji umepanuka, vitu na watu wameongezeka sana. Kuna mabadiliko mengi yanayoonekana na yanavutia kwa macho. Tofauti hata ya miaka 3 nyuma iko wazi. Dar es salaam jiji linakua kwa kasi.

Ambacho hakijabadilika na pengine hali ni mbaya ni hali ya usafiri wa umma. Idadi ya magari imeongezeka ingawaje mengi hayako katika hali nzuri. Barabara zimeongezeka na njia zimeongeka lakini mpaka leo tunagombania magari.

Kuna sehemu Tanzania miaka hiyo magari yalikuwa hayafiki leo yanafika na wanapanda kwa staha. Dar kuliko endelea kabla watu bado wanagombania gari.

Nimewatafakari hawa muuguzi wa Muhimbili ambaye miaka yote anaenda kazini kwa usafiri, mhudumu wa ofisi ya serikali ambaye ofisi yao haina gari,
Mtoto aliyeanza kusoma shule ya msingi hadi chuo akiwa hapa, mfanyabiashara wa karume kwa miaka 5 haya ndo maisha yao ya kila siku.

Watumiaji wa usafiri huu ni wengi sana. Lakini inaonekana siyo serikali au wenyewe hawajali hii hali. Inawezekana watu wameamini hii ndio stahiki yao kusafiri kidhalili mkiwammebanana kama taka kwenye gunia.

Traffic police wa dar hili kwao si tatizo. Ukizidisha mzigo kwenye usafiri wako binafsi utakamatwa lakini si daladala.

Sumatra kwao hili si tatizo. Viongozi wa mji huu kutwa wanasemea barabara au matengenezo ya barabara au miundo mbinu ya kisasa ya barabara na si hali ya abiria.

Dar ina wabunge wengi na madiwani wakutosha lakini wao wanaongelea umiliki wa UDA na si hali ya wasafiri.

Mwendokasi ilihadithiwa kuwa itakuwa suluhisho, imeondoa foleni lakini udhalilishaji ule haujatoka.

Kama wakazi wa dar ambao wengi wamesoma hadi darasa la saba na vidato wanatendewa hivi seuze huko ambako hawapo.

Haihitaji PHD kujua kuwa hili si sawa. Na si kweli kuwa miji yote yenye watu wengi na kipato kama chetu hali ni hii.
Hapo Nairobi tu kuna unafuu na SA hali tofauti kabisa.

Nadhani ni wakati muafaka wakazi wa jiji hili kuongelea vipaumbele halisi kwenye siasa na kwa watendaji.
Kama kuna fedha za kutindua barabara kila mwaka, kama kuna tunakopa kwa ajili ya mwendokasi basi tunaweza kutatua na hili. Si sawa kuwa kuongoza kwenye rekodi za makusanyo ila maisha yenu ya kila siku yakawa hayaguswi kwa zaidi ya miaka 20 na tukaona tunaendelea.
Hadithi za uchumi kukua na maisha bora hazijayagusa maisha ya watu wa dar wasio na uwezo wa kununua gari.
Mimi nimeona niseme, msikie sio sawa. Kama ni kuwanyima kura nalo ni sawa.
 
Ujanja ujanja mwingi. Hata mambo serious bado yanafanywa kwa maelekezo kutoka juu. Fikiria mradi wa mabasi ya mwendo kasi ulivyoshindwa kuleta matokeo chanya, mabasi shida, kimara watu wanajazana mpaka unawaonea huruma
 
Back
Top Bottom