Usafiri wa treni ya TAZARA ubora wake ukoje?

mpimamstaafu

JF-Expert Member
Jul 18, 2018
4,445
4,704
Watanzania wenzangu, naomba kufahamu ubora wa treni ya Tazara kwa waliosafiri nalo hivi karibuni.

Natarajia kusafiri kwenda Mbeya hivyo naomba kujulishwabdaraja gani nzuri kusafiria, usalama, nauli na muda unaotumika kwa safari.

Na kama kuna ziada naomba pia nifahamishwe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watanzania wenzangu ,naomba kufahamu ubora wa treni ya Tazara kwa waliosafiri nalo hivi karibuni.Natarajia kusafiri kwenda Mbeya hivyo naomba kujulishwa , daraja gani nzuri kusafiria, usalama,nauli na muda Unaotumika kwa sababu kwa safàri.Na kama kuna ziada naomba pia nifahamishwe

Sent using Jamii Forums mobile app

Unamchokoza Magu wewe, wenzako wanatamani watu waone ishu ya Treni ni mpya
 
Mtz one ,acha kukurupuka kujibu jaribu kuelewa nini kimeulizwa suala la kumchokoza Magu lina uhusiano gani na Tazara?Pia lugha ya matusi sio nzuri wala haikupi maksi zozote zaidi ya kukushusha.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sio kumshusha tuu nafikiria jf ianzishe ban ya maisha hawa watoto waliotoka kunyonya siku za karibuni wana shida sana ni life ban wakajipange. Hiki sio kijiwe au shule ya kufundishwa heshima.
 
Mtz one ,acha kukurupuka kujibu jaribu kuelewa nini kimeulizwa suala la kumchokoza Magu lina uhusiano gani na Tazara?Pia lugha ya matusi sio nzuri wala haikupi maksi zozote zaidi ya kukushusha.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu mwache.. kujibizana na mtu kama huyo ni kujishushia heshima yako.
Kukaa kimya ni jibu tosha.
 
Ili upate nafasi ya kusafiri wa tren kutoka Dar mpaka Mby kwa daraja la kwanza au la pili unatakiwa ufanye booking mapema ikiwezekana week 2 au 3 kabla ya safari kwani nafasi zinajaa mapema Sana kwa madaraja hayo.

Daraja la kwanza Chumba kinakuwa Cha watu 4 na daraja la 2 watu sita, vyoo vyao ni visafi na maji yapo muda wote. Kwa upande wa vyakula wahudumu wanapita kuchukua order kila chumba baada ya muda unaletewa au unaweza kwenda buffet unaweka order unasubiri uandaliwe hii pia ni sehemu nzuri kujipumzisha kwani kuna sehemu ya vinywaji pia. Kwa upande wa Nauli sikumbuki vzr Ila kwa daraja la kwanza nadhani ni Tsh. 75,000 au 780000 na sent kidogo kwa daraja la pili ni Tsh. 48,000 na sent kidogo pia na kuna daraja la pili la viti namaanisha ni behewa lina viti vya kukaa linchukua watu wengi tofaouti na kwenye vyumba ambako viti mnavyokalia ndo vitanda mtakavyolalia Kama zilivyo double decker. Kama hutaki usumbufu au Kama unasafiri na familia unalipia chumba nafasi za watu 4 kwa first na 6 kwa second unajiachia humo pasipo usumbufu.

NB: Kuhusu Nauli inawezekana zikawa zimepanda maana hizi nilizoandika hapa zilikuwa za mwaka Jana, haya no baadi ya ninayoyafahamu kuhusiana na usafiri wa tren la TAZARA.
 
Thanks Sana mkuu. Nadhan nimeshawishika ngoja nipate taarifa zaidi ili nifanye hivo.
 
Back
Top Bottom