Usafiri wa mwendokasi hauna tofauti na usafirishaji wa ng'ombe toka mikoani

lingamba lidodi

JF-Expert Member
Nov 15, 2018
964
1,137
Habari wana jf!
Adha wanayopata wasafiri jijini D'saalam kwakutumia usafiri wa mabasi ya mwando kasi,hauna tofauti sana na magari ya Ng'ombe toka mikoani.

Kama afya mgogoro utakaa sana kituoni,na ukibahatika kuingia utapumua kwa kazi kubwa kwaajili ya mbanano.

Kituoni unaweza subiri SAA nzima bila kupata Gari la kule unakoenda.

SERIKALI IRUHUSU BASI ZA ABIRIA BARABARA ZOTE ZINAZOTUMIKA NA MWENDO KASI

Kulikuwa hakuna haja ya kuzuwia usafiri wa awali kwa kutegemea mabasi ya mwendo kasi ambao haikujulikana kama utatosheleza mahitaji .

Rais magufuli, tunakuomba uliangalie tatizo hili la kuzuwia daladala za kwenda mjini kwa kutegemea hayo mabasi ambayo ni machache sana.

RUHUSU DALADALA KWA IDADI YA MAHITAJI ILI ADHA IONDOKE.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mi hata kama Niko ubungo naenda kimara,,nageuza na Gari ya gerezani,,ili nikae nipate siti😂😂😂😂
 
Yule tokomeza ziro anachojua ni kutafuta kiki ile ya tezi dume sijui imeishia wapi.Liquid konki fire atabakia kuwa juu
 
Bila Nguvu na ujanja hupati seat mwendokasi. Ni usafiri wa udhalilishaji maana wote wakubwa kwa wadogo kugombania.

Sent using Jamii Forums mobile app
Juzi nimepanda kutoka ferry mpaka ubungo badala yake dereva katupeleka hadi kimara akifika kituoni kabla watu hawajashuka anafunga mlango na hapo watu wanapumuliana kama nn sijui na watu wanasweat vibaya mno...
Kwakweli sijui kama nitakuja kuupanda tena na hapo ktuoni tulikuwa tumesubiri zaidi ya lisaa limoja
 
Nilitoa 10000 wakasema hawana chenji nisubiri zipatikane, nikasema hata kaoption ka lipa kwa mpesa wameshindwa kuongea na mitandao wawekewe, japo ni 650?!1. ubunifu hakuna ni huo usafiri ni kero sana.
 
Yaan ni kero kwakweli
 
Back
Top Bottom