Usafiri wa Daladala ni mateso. Hakuna mamlaka ya kudhibiti ubovu wa Daladala, au mpaka Majanga yatokee ndiyo tutashituka?

Kurunzi

JF-Expert Member
Jul 31, 2009
9,277
9,912
Kigezo cha Gari kuwa Dadadala ni lazima liwe Bovu? Nenda stendi zote, Dar, Dodoma, Arusha, ukiacha zile zinazofanya ruti ndefu lakini zingine zote magari ni mabovu kiasi ambacho zingine ukiwa ndani unaona chini.

Lakini sioni mammlaka husika zikifanya kazi yake.

Zamani kwa mabasi yalikuwa yanafanya ruti zake kutoka makumbusho kwenda Posta zilikuwa zinasifika kwa ubora wake, siku hizi ni balaa tu gari ni mbovu, gari imepigwa rangi nje ukiingia ndani ni uozo mtupu.

Inafikirisha sana kuona usafiri wa Daladala ni kama mateso na dhamha ili hali kwa wenzetu waliostarabika ni usafiri rahisi wa jumuiya.
 
Huku Arusha Kuna daladala za Kilombero kwenda Kijenge juu na Moshono, nyingi ni majanga
 
Mkiambiwa biashara zimeporomoka muwe mnaelewa! Uwezo wa wananchi (wenye daladala) ku-replace magari ya zamani kwa mapya umepungua sana. Kinachofanyika ni mikangafu kuendelea kufanyiwa ukarabati hadi hapo itakapokufa rasmi.

Fanya utafiti utagundua hata idadi ya daladala kwenye miji yote imepungua sana badala yake zimekuwa replaced na bajaji na bodaboda; ndio uwezo wa matajiri kwa sasa! Hata wale matajiri wa mabasi ya mikoani ambao kila mwisho wa mwaka lazima waingize vifaa vipya barabarani wako wapi? Hali ni mbaya!

Mliambiwa wanatakiwa waishi kama mashetani kwa ujinga tukashangilia bila kujua wao wakiishi kama mashetani sisi makapuku tutaishi zaidi ya mashetani! Tukafurahia kuona watu wakiporwa mtaji yao; fedha zao zikikwapuliwa benki; bureau zao zikikwapuliwa fedha hadi vitendea kazi; tukasema haituhusu sisi "majizi" hayo! Tusilalamike!
 
Njia nzuri ya kuepuka hayo vuta kausafiri kako tu chap ,vuta HONDA FIT uepuke madhira hayo yote

sent from HUAWEI
 
Njia nzuri ya kuepuka hayo vuta kausafiri kako tu chap ,vuta HONDA FIT uepuke madhira hayo yote

sent from HUAWEI
Ni asilimia ngapi wenye uwezo wa kuvuta hiyo, kujaza mafuta daily na service bila kusahau bima. Nilichogundua usafiri wa daladala bado haujakidhi, mabasi ya mwendokasi wajitahidi sana kupunguza gap.
 
Back
Top Bottom