Sami Omary Khamis
Member
- Sep 8, 2020
- 67
- 133
#USAFIRI WA ANGA.
CCM inatambua kuwa usafiri wa anga ni njia muhimu na ya haraka inayounganisha visiwa vya Zanzibar na sehemu nyingine duniani. Katika Ilani hii, Chama cha Mapinduzi kitaelekeza SMZ kuongeza uwezo na ufanisi wa viwanja vya ndege kwa kuzingatia viwango vya kimataifa ili kuendana na kasi ya ongezeko la abiria hususani watalii na kuvutia mashirika ya ndege mengi zaidi kufanya safari zake nchini.
Mambo yafuatayo yatatekelezwa kwa kipindi cha mwaka 2020-2025;
1. Kuendeleza ujenzi wa kiwanja cha ndege cha Pemba ikiwemo kuongeza urefu wa njia ya kurukia ndege (runway) kufikia mita 2,500, kujenga jengo jipya la abiria na kuimarisha huduma zote za mahitaji ya kiwanja hicho.
2. Kumalizia ujenzi wa uwanja mdogo wa ndege wa Kigunda na kujenga viwanja viwili vya kurukia na kutua helikopta, kimoja Unguja na kimoja Pemba.
3. Kuimarisha ubora wa vifaa na huduma kwenye uwanja wa ndege wa AAKIA.
Mambo haya pamoja na mengine mengi yatatekelezwa na SMZ ili kuendelea kuboresha Usafiri wa Anga Zanzibar.
Tunaomba KURA yako kwa CCM,
#ChaguaDr. Mwinyi,
#ChaguaDr. JohnMagufuli.