Zanzibar 2020 Usafiri wa anga: Tutatekeleza Zanzibar (2020-2025)

Sep 8, 2020
66
125
#USAFIRI WA ANGA.

CCM inatambua kuwa usafiri wa anga ni njia muhimu na ya haraka inayounganisha visiwa vya Zanzibar na sehemu nyingine duniani. Katika Ilani hii, Chama cha Mapinduzi kitaelekeza SMZ kuongeza uwezo na ufanisi wa viwanja vya ndege kwa kuzingatia viwango vya kimataifa ili kuendana na kasi ya ongezeko la abiria hususani watalii na kuvutia mashirika ya ndege mengi zaidi kufanya safari zake nchini.

Mambo yafuatayo yatatekelezwa kwa kipindi cha mwaka 2020-2025;

1. Kuendeleza ujenzi wa kiwanja cha ndege cha Pemba ikiwemo kuongeza urefu wa njia ya kurukia ndege (runway) kufikia mita 2,500, kujenga jengo jipya la abiria na kuimarisha huduma zote za mahitaji ya kiwanja hicho.

2. Kumalizia ujenzi wa uwanja mdogo wa ndege wa Kigunda na kujenga viwanja viwili vya kurukia na kutua helikopta, kimoja Unguja na kimoja Pemba.

3. Kuimarisha ubora wa vifaa na huduma kwenye uwanja wa ndege wa AAKIA.

Mambo haya pamoja na mengine mengi yatatekelezwa na SMZ ili kuendelea kuboresha Usafiri wa Anga Zanzibar.
Tunaomba KURA yako kwa CCM,
#ChaguaDr. Mwinyi,
#ChaguaDr. JohnMagufuli.
 
GHIBUU

JF-Expert Member
Jan 13, 2011
4,300
2,000
Mshafail tena vibaya

Act Wazalendo itafanya kila jitihada Zanzibar kuwa na mamlaka kamili ili iweze kunufaika na rasilimali zake ikiwemo anga na bahari

Zanzibar kuazisha jeshi la police lake zaidi ya ajira 3000, kuazisha jeshi la wananchi kwa wazanzibari wenyewe zaidi ya ajira 3000

Zanzibar kupata fursa kujiunga jumuiya za kimataifa kama FiFa ,CAF na OIC

Zanzibar kuweza kupata fedha kutoka kwa wahisani moja kwa moja pamoja Na scholarship

Zanzibar kupata ajira nyengine zaidi katika wizara ya uhamiaji zaidi ya ajira 2000

Ujenzi wa bandari ya mpiga duri na kuwa bandari huru.

Ujenzi wa uwanja wa ndege wa Pemba kuwa wa kimataifa pamoja na bandari ya were.

Haya yote yatafanyika chini ya serikali y umoja wa kitaifa, rais maalim seif sharif Hamad
 
mtanzania in exile

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
472
500
#USAFIRI WA ANGA.

CCM inatambua kuwa usafiri wa anga ni njia muhimu na ya haraka inayounganisha visiwa vya Zanzibar na sehemu nyingine duniani. Katika Ilani hii, Chama cha Mapinduzi kitaelekeza SMZ kuongeza uwezo na ufanisi wa viwanja vya ndege kwa kuzingatia viwango vya kimataifa ili kuendana na kasi ya ongezeko la abiria hususani watalii na kuvutia mashirika ya ndege mengi zaidi kufanya safari zake nchini.

Mambo yafuatayo yatatekelezwa kwa kipindi cha mwaka 2020-2025;

1. Kuendeleza ujenzi wa kiwanja cha ndege cha Pemba ikiwemo kuongeza urefu wa njia ya kurukia ndege (runway) kufikia mita 2,500, kujenga jengo jipya la abiria na kuimarisha huduma zote za mahitaji ya kiwanja hicho.

2. Kumalizia ujenzi wa uwanja mdogo wa ndege wa Kigunda na kujenga viwanja viwili vya kurukia na kutua helikopta, kimoja Unguja na kimoja Pemba.

3. Kuimarisha ubora wa vifaa na huduma kwenye uwanja wa ndege wa AAKIA.

Mambo haya pamoja na mengine mengi yatatekelezwa na SMZ ili kuendelea kuboresha Usafiri wa Anga Zanzibar.
Tunaomba KURA yako kwa CCM,
#ChaguaDr. Mwinyi,
#ChaguaDr. JohnMagufuli.

Hivi jamani mnapotaka kutudanganya mnafikiri sisi ni majuha sana au nyie ndio akili zenu finyu na hamkumbuki lolote? Hebu twambieni kwanza ujenzi wa kiwanja cha ndege kipya cha abeid amani karume ni miaka mingapi sasa kinajengwa na hakijakamilika? Ikiwa kiwanja kimoja tu kimechukua miaka tele na hadi leo bado hakifanyi kazi kiukamilifu, itachukua miaka mingapi kujenga viwanja hivyo mnavyotwambia leo?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom