Wewe naona hujapanda magari ya Kigoma, Sumbawanga au Mpanda shukruni hata kwa hicho kidoogo wanachotoa. Hizo ruti utaambulia Mende na Kunguni Mkuuu.Hao jamaa wanajitahidi kwa huduma , kusini mikoa ya mtwara na Lindi bado kunahitaji ukombozi mkubwa sana kwa biashara ya abiria maana ni kama ndo wanaaanza ,
Abiria kule hana haki zake za msingi , kumbuka hawana hata Miaka 10 ya mabasi mazuri ,kwa sababu njia ilisumbua sana kule ,
Usishangae unapanda Basi halafu konda anakuomba pesa ya begi ulilobeba Kama mzigo mbali na nauli .