Usafiri dar es salaam wapata uvumbuzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Usafiri dar es salaam wapata uvumbuzi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mkombozi, Feb 1, 2011.

 1. M

  Mkombozi JF-Expert Member

  #1
  Feb 1, 2011
  Joined: Feb 19, 2008
  Messages: 626
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Nampa ushauri wa bure Waziri wa Ujenzi za kuondoa kero ya foleni Dar es Salaam. Kujenga barabara kila kona sio suluhisho la kudumu, kila siku watu wanaongezeka na kuingia Dar es Salaam. Kifuatacho kifanyike

  •Kujenga bandari kubwa ya nchi kavu maeneo ya kibaha au mkoa wa Pwani, then kujenga reli itakayotoka bandarini Dar moja kwa moja hadi kibaha kwaajili ya Treni ya Mizigo ya kuchukoa macontainer kutoka Dar hadi kibaha. Malori yote yaanzie Kibaha kwenda mikoani, Dar kubaki malori yanayobeba mizigo ya Dar tu. Pia Reli hii itatumika kupitia treni la abiria pia.
  •Pia wafufue usafiri wa treni Dar, Moja ianzie Posta, kupitia Kariakoo, Manzese, Ubungo, Kimara, Mbezi hadi kibamba. Nyingine Kariakoo hadi uwanja ndege, Tabata.Nyingine Posta, Mwenge, Mbezi beach, Tegeta, book bunju.
  •Kuanzisha usafiri wa Makampuni ili kuimarisha usafiri wa uma, vigari vidogo vyote kuondolewa.
  •Magari binafsi yapungue hasa sehemu zenye treni.

  Hizi mbinu ni za kudumu, ujenzi wa barabara sio suluhisho sana. Pia usafiri imara na wa uhakika itapunguza kasi ya watu kuagiza magari au kutumia magari yao kwenda mjini.
   
 2. George Maige Nhigula Jr.

  George Maige Nhigula Jr. Verified User

  #2
  Feb 1, 2011
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 470
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Naunga mkono, hoja Dawa ni kuimarisha public transport iwe bora na ya uhakika, jenga underground metro train, na mabasi makubwa ya abiria yawe kwa style ya kampuni , hakuna nchi yenye watu wengi kama china lakini wameweza ku control foleni kwa kuwa na reliable public transport, watu wengi wata opt kutumia public transport kwa sababu ni reliable and cheap kuliko kutumia private transport. huo mradi wao wa BRT umefia wapi?

  Dar es laam ni mji wa Bahari wanatakiwa kujenga a lot of piers ili watu wa kawe, mikocheni, mbweni, tegeta, mbezi, temeke waweze kutumia speed boat au ferries kuja mjini posta, tena hiyo ni rahisi kabisa ku implement, serikari ijenge hizo piers iwe inakusanya ushuru lakini uendeshaji wa hizo ferries wapatiwe makampuni binafsi kama mawili hivi au matatu na yawe regurated to keep the fare reasonable
   
 3. g

  geophysics JF-Expert Member

  #3
  Feb 1, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 904
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mawazo yako ni mazuri kabisa mzee... Ikitekelezeka folleni zitaisha mjini.
   
 4. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #4
  Feb 1, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,164
  Likes Received: 1,251
  Trophy Points: 280
  Seconded.
  Wasiwasi wangu hawa jamaa huwa hawafanyii kazi vitu vya msingi kama hivi ulowapa. Hili lingekuwa ni suluhisho la kudumu na si kwa usafiri tu hata makazi, watu wangeenda kujenga makazi bora huko nje ya mji na kuacha kuishi kwenye chumba kimoja Sinza, Tandale, Manzese
   
 5. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #5
  Feb 1, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,725
  Likes Received: 1,631
  Trophy Points: 280
  hihii sio Suluisho la sasa , kama ungeusisha Kuhama kwa Wizara kwenda Dodoma ua Taasisis za fedha kuamia Bagamoyo , barabara za ndani kama Mwananyamala kwenda kijitonyama kuunganisha na sinza, barabara zote za kijitonyama kupigwa lami ili ziweze kupitika kwa urahisi , surender Bridge kupanuliwa kuwa njia nne au kuweka bara bara ya juu kama ikiwezekana , sio kuwa dar kuna magari mengi bali mpangilio tu
   
Loading...