Usafiri Dar Es Salaam kero tupu, Si Abiria, Si foleni, Si Trafiki, Si Viongozi(misafara) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Usafiri Dar Es Salaam kero tupu, Si Abiria, Si foleni, Si Trafiki, Si Viongozi(misafara)

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mansakankanmusa, Sep 8, 2012.

 1. mansakankanmusa

  mansakankanmusa JF-Expert Member

  #1
  Sep 8, 2012
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 4,092
  Likes Received: 603
  Trophy Points: 280
  Tanzania ya 1980 si hiiya leo, imebadirika sana. Kama wewe hujazaliwa jijini au hata kama umezaliwajijini inatosha kuona tofauti ya DSM ya miaka 32 iliyopita. Nikiwa mdogo sana,katikati ya mji watu, magari wakati mwingine hata nyumba na barabara nje ya mjizilikuwa chache sana, na sehemu nyingine zilikuwa ni za waenda kwa miguu footpath.ubungo kuelekea tabata  Maeneo ya mtaa wa samora unaweza ukadumu kwa dakika 20 ndipo utaonagari ama mtu akipita akikata mtaa. Hakika watu walikuwa wachache sana.


  Kwa sasa tumekuwa wengi sana, ten asana. Magari na raia/ abiriawamekuwa wengi pia. Wasomi wameongezeka, lakini unaweza ukahoji enzi zile eneokama ukonga palikuwa ni mashamba leo hii wameshindwaji kupangilia mji.  Dar es salaam imegeuka kero kero kero, tena inasababishwa na VIONGOZINA WASOMI.


  Utakaa chini ujiulize hivi mitaa iliyojengwa vibaya!Hawa planners hawapo??! Tunavyokosa barabara mitaani kumejaa nyumba huu niubinadamu gani.


  MAENDELEO
  : kama unatimamu huwezikuthubutu ukatamka kwamba DSM inamaendeleo, hakika DSM ni kero na sivinginevyo.


  Uwe umetoka nje ya Tanzania utaamini maneno yangu. NendaLilongwe acha Nairobi,Kenya. Utajiuliza maswali bila majibu.


  Kero
  : abiria wenyewe kwa wenyewe kerotupu. Kama gari imefika ubungo kwa nini ushushwe songas. Kama gari limejaa kwanini upande, kama unatoka gym Unajasho kwa nini ujigusishe na mtu kavaa zakevizuri, unakuta mtu kava singlend, kama unaongea na simu kwa nini sautidaladala zima, wakati simu yangu inaita hakika siwezi zungumza wakati weweunaongea. Achilia mbali milio inayokera.  Trafikipolisi, kama taa zipo kwa nini uongoze, kiongozi anajua kabisa kwamba yukoMbezi luis Gari zinazuiwa ubungo, kwa nini.


  Hawo wasomi waliohitimu wameshindwa wapi, kugundua kero na kuzitatua.


  DALADALA: waliondoa Hyace wameruhusu KOSTA ni jambojema, lakini, nani hajui kwamba mabasi marefu maref u ndio muafaka? Enzi za chai maharage ni sasa tofauti ikowapi? Ni huko kulaa na kuangalia mbele, city bus za mji muhimu kama dsm, jamanibado tuamini kuwa ni kosta au dcm? Hapana.


  Ingefika mahali tukate tiketi kwa mwezi na kampunizenye uzoefu kusafirsha abiria waendao makazini wasafirshe watu.


  Binafsi naombea sana mradi wa mabasi yaendayo kasiBRT rapid transport naamini itakuwa fundisho naahidi daladala byebye! Ndio tunafanyabishara za daladala lakini wengine makazini tunaharibikiwa  Madhara:
  labda kwa asiye jua, lakinitunafika makazini hauko vema, umechelewa na umevurugwa kwenye daladala..


  Huwezi ukawa na mpangilio mzuri wakati uligombea naumeminywa, umechafuka, nguo zimekunjikana, viatu ndio usiseme, ustaarabu ni upihapo. Ifike mahala unaweza ukafurahia safari ya kwenda na kurudi nyumbani. Kusomana kujisikilizia muziki na kurelax.  Ni mawazo/maoni yangu ww unasemaje,
   
 2. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #2
  Sep 8, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kinachonikera zaidi misafara ya viongozi wetu isiyokuwa na tija na nadhani kama na wao wangekuwa wakikaa kwenye foleni suluhisho lingekuwa lishapatikana na bora basi wanakowahi kungeonyesha matunda yake badala yake wanazidi kuboronga kwa kila kitu
   
 3. mansakankanmusa

  mansakankanmusa JF-Expert Member

  #3
  Sep 8, 2012
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 4,092
  Likes Received: 603
  Trophy Points: 280
  Mwingine anawahi mwanamke hotelini
   
 4. Mcharuko

  Mcharuko JF-Expert Member

  #4
  Sep 9, 2012
  Joined: Sep 25, 2011
  Messages: 201
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Ashakum si matusi, Jamaa mmoja alikuwa amebanwa na tumbo la kuhara,
  Tulisubiri msafara wa kiongozi gani sijui yaani hata simjui kwa masaa 2 mpaka
  jamaa akaharibikiwa kwenye gari. Yaani sijui tutembee na NEPI?!!!!!!
   
 5. Zamaulid

  Zamaulid JF-Expert Member

  #5
  Sep 9, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 16,355
  Likes Received: 6,699
  Trophy Points: 280
  nyie kina mama si huwa mnatembea na zile sijui mnaita pedi,hamkumstili mtoto wa mwanamke mwénzenu!
   
 6. mansakankanmusa

  mansakankanmusa JF-Expert Member

  #6
  Sep 9, 2012
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 4,092
  Likes Received: 603
  Trophy Points: 280
  na kuchimba dawa ni marufuku sasa, kazi ipo hapo. mkuu mwakyembe angeachana na kuchimba dawa angedili na matatizo mengine
   
Loading...