Usafi wa mazingira na binafsi husaidia kupunguza magonjwa ya kitropiki

Jul 13, 2021
6
6
Mazingira safi ni dawa, mazingira safi ni tiba, hutufanya kuishi Kwa amani mbali na magonjwa. Ni jambo la kushangaza, ya kwamba mwanadamu ni mzalishaji wa taka lakini si mwepesi wa kuziondoa taka hizo.

Magonjwa mengi hutokana na hali duni ya usafi wa mazingira na wetu binafsi.

Kusafisha mazingira hapahitaji akili ya ziada zaidi ya kujidhatiti kuifanya kazi hii. Kusafisha vyanzo vya maji, na kila kinacho husika katika matumizi ya mwanadamu.

Magonjwa yaliyosahaulika ni magonjwa yanayosababishwa na bakteria ama vimilea ambukizi ambavyo hupatikana katika nchi 149 ambazo ziko kwenye ukanda wa kitropiki ni zile zenye joto kali ama la wastani.

Magonjwa haya yanaleta athari hatarishi mfano husababisha matatizo kama upofu au matatizo ya tumbo. Magonjwa ya kitropiki ni kama ugonjwa wa minyoo tumboni, kichocho, matende, upofu wa macho, trakoma.

Takwimu zinaeleza kuwa magonjwa haya huleta vifo zaidi ya laki moja na sabini elfukwa mwaka, na watu zaidi ya bilioni huhitaji matibabu. Magonjwa haya hufanya jamii kutumia gharama kubwa kutibu waathirika pale gonjwa linapokuwa kubwa.

Moja kati ya vichochezi vya magonjwa haya niukosefu wa usafi wa mazingira na upatikanaji wa maji safi, mazingira, chakula na makaazi. Wanawake na wasichsana ni waathirika wa kiwango kikubwa wa magonjwa ya kitropiki kwani wao ndio wadau wakubwa wa kuteka maji kwenye mito na visima.

Je, vyanzo hivi vikisafishwa tutaathirika?Mazingira yanamchango mkubwa katika afya zetu.

Wengi hutazama magonjwa haya na kuyachukulia kwa wepesi. Husemekana yamesahaulika kwani si rahisi mtu kufikiri juu ya kichocho na trakoma kwa sasa na kusahau ukimwi ama malaria.

Takwimu zinaonesha kuwa waathirika wa magonjwa haya kwa asilimia kubwa ni masikini, yaani watu wenye kipato cha chini zaidi.

Je, pesa ndio jibu la usafi wa mazingira na miili yetu? Hapana.Usafi wa mazingira hauhitaji pesa wala utajiri.

Magonjwa mengi ya kitropiki huambukizwa kutokana na kutokuwa na usafi wa mazingira na ule wa miili yetu. Mazingira yakitunzwa, yatatutunza pia.

Usafishaji wa mazingira huweka mbali vimelea viletavyo magonjwa haya.
 
Back
Top Bottom