Usafi wa makonda jukumu la nani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Usafi wa makonda jukumu la nani?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Jayfour_King, Nov 26, 2010.

 1. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #1
  Nov 26, 2010
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Hi wana JF,
  Imekuwa ni kawaida sasa hawa wahudumu wetu wa mabasi ya mjini (Town Buses) dala dala, vifodi chai maharage nk. tangu umeanzishwa huu utaratibu wa kuvaa uniform wamekuwa wachafu zaidi kuliko ilivyokuwa hapo kabla ambapo kila mtu alikukwa anavaa vazi alipendalo na zilikuwa nguo zao binafsi.

  Tangu utaratibu huu umeanzishwa hali imekuwa mbaya zaidi kwa kuwa watumiaji wa mavazi haya yaani makonda na madereva wao, wamekuwa wanavaa kwa ajili ya kuwaonyesha traffic police kwamba wanazingatia agizo la kuvaa uniform.

  Kilicho kibaya hapa ni kwamba nguo hizi mara nyingi ni chafu na hata uvaaji wake inaonyesha kabisa kwamba ni nguo zisizo thaminiwa na mvaaji wake. Kwani mbali yakuwa zimechafuka bado uvaaji wake ni ule wa Ka.. Ku.. ambao ni maarufu kwa vijana wasio na maadili mema.

  Hapo utaona mapungufu yaliyopo kwa mtoa huduma muhimu kama muendesha daladala kuwa katika hali ambayo sio mfano bora kwa jamii. Kibaya zaidi ni pale ambapo hata traffic polisi wanapowakamata kuhusiana na matatizo mbalimbali yanayohusiana na gari hili huwa hawalichukulii kama ni tatizo.

  Ushauri:
  Kama jukumu hili halina msimamizi maalum kisheria, ni bora makonda na madereva wao wakaruhusiwa kuvaa nguo zao wazipendazo ambazo ni lazima zitakuwa safi kama ilivyo kuwa hapo awali. Kuliko kuvaa hivi wafanyavyo sasa ambapo inakuwa ndio kigezo cha uchafu, tunatoa picha gani kwa watoto wetu na wageni kwa uchafu wa nguo hizo na uvaaji usiozingatia maadili na pia zikiwa zimechanika sehemu ambazo mtu mwenye akili timamu hapaswi kuvaa mbele ya watu hata kama kuna nguo nyingine ndani.

  Tanzania yenye makonda wasafi inawezekana, lipi lifanyike? Na jukumu hili ni la nani ki mamlaka?
   
Loading...