Usafi wa madereva na makonda wa daladala ni jukumu la nani?

Jayfour_King

JF-Expert Member
Nov 15, 2009
1,135
128
Hi wana JF,
Imekuwa ni kawaida sasa hawa wahudumu wetu wa mabasi ya mjini (Town Buses) dala dala, vifodi chai maharage nk. tangu umeanzishwa huu utaratibu wa kuvaa uniform wamekuwa wachafu zaidi kuliko ilivyokuwa hapo kabla ambapo kila mtu alikukwa anavaa vazi alipendalo na zilikuwa nguo zao binafsi.

Tangu utaratibu huu umeanzishwa hali imekuwa mbaya zaidi kwa kuwa watumiaji wa mavazi haya yaani makonda na madereva wao, wamekuwa wanavaa kwa ajili ya kuwaonyesha traffic police kwamba wanazingatia agizo la kuvaa uniform.

Kilicho kibaya hapa ni kwamba nguo hizi mara nyingi ni chafu na hata uvaaji wake inaonyesha kabisa kwamba ni nguo zisizo thaminiwa na mvaaji wake. Kwani mbali yakuwa zimechafuka bado uvaaji wake ni ule wa Ka.. Ku.. ambao ni maarufu kwa vijana wasio na maadili mema.

Hapo utaona mapungufu yaliyopo kwa mtoa huduma muhimu kama muendesha daladala kuwa katika hali ambayo sio mfano bora kwa jamii. Kibaya zaidi ni pale ambapo hata traffic polisi wanapowakamata kuhusiana na matatizo mbalimbali yanayohusiana na gari hili huwa hawalichukulii kama ni tatizo.

Ushauri:
Kama jukumu hili halina msimamizi maalum kisheria, ni bora makonda na madereva wao wakaruhusiwa kuvaa nguo zao wazipendazo ambazo ni lazima zitakuwa safi kama ilivyo kuwa hapo awali. Kuliko kuvaa hivi wafanyavyo sasa ambapo inakuwa ndio kigezo cha uchafu, tunatoa picha gani kwa watoto wetu na wageni kwa uchafu wa nguo hizo na uvaaji usiozingatia maadili na pia zikiwa zimechanika sehemu ambazo mtu mwenye akili timamu hapaswi kuvaa mbele ya watu hata kama kuna nguo nyingine ndani.

Tanzania yenye makonda wasafi inawezekana, lipi lifanyike? Na jukumu hili ni la nani ki mamlaka?
 
Mi Nazani Ikifunguliwa Kampuni Itakayotoa Huduma Ya Usafi Kwa Hawa Watu Itakuwa Poa Zaidi Kuwe Na Wafanyakazi Warembo Wawasafishie Nguo Zao Hasa Za Ndani Na Vikwapa Vyao Loh! Wanakera Jamani!!
 
Unakuta konda kikwapa kinanuka kama choo box a hawafui mdomo unaharufu ya ugori' kiroba na sigara yani ni shidaa baadhi yao lakini siyo wote
 
Kuna mmoja juzi alikuwa mchafu na alikuwa amelewa, alikuwa na maneno mengi kama kasuku.
Ila alitunufaisha ambavyo hakuchukua nauli kwa abiria wote waliopandia relini hadi mawasilianoni.
Na abiria wasivyokuwa na nidhamu wakawa wanashuka tu bila kulipa walivyoona yeye ameshatangulia chini.
 
Ni jambo la kushangaza wakati Mamlaka zinazosimamia usafiri Wa daladala zipo lakini abiria tunateseka Na hali ya uchafu Wa makondata Na madereva Wa daladala kuwa mbaya Na mamlaka kukaa kimya bila kukemea.Unakuta kinda au Dereva kavaa suruali 2 zote in mregezo mpaka chupi inaonekana Na chupi yenye CHAFU.Miguuni kavaa kandambili nywele hajachana ili mraji tu akusanye nauli.Tunaiomba Sumatra iliangaikie hili mbona wakati Wa Mzee MWAIBULA liliwezekana?
 
Poleni na majukumu.

Daladala ndani ya jiji la Dsm n kiungo muhimu sana kwa ajili ya sisi wakazi wa Dsm kufanya kazi zetu vzr,mtaa kwa mtaa.

Inakuwaje madereva na makondakta hupenda kuvaa nguo chafu, oversize, zisizo na vifungo wala zipu za suluari? Ni utamaduni au tatizo vichwani mwao?
 
Sio Dar tu ni nchi nzima huwezi amini hata Marekani makonda wao wachafu sana naona ni code of conduct
 
Tatizo hata sijui ni nini. Kuna kipindi D. Mwaibula ililikomalia hili suala lakini nafikiri kwa sasa hamna anayehangaika nao.
 
kwa Dar hata abiria wennyewe wachafu- hasa wanaume vijana wengi asubuhi hunuka vikwapa hawaogi!!!!
 
Mkuu ingia Nairobi, wengi wa makondakta wako smart hasahasa wa "matatu" tena magari yapo standard mpaka konda ana kiti chake... WaKenya Wapo vizuri kwenye kusimamia Sheria, Tanzania tupo vizuri kwenye kuziburuza sheria
 
kwa atakayebisha basi wewe fanya utafiti mabasi yale ya alafajiri ambapo tunategemea mtu awe ameoga na mtanashati maaan hajapambana bado na kashkash za siku lakini still mtu ananuka kikwapa,
1. shati inavaliwa siku 2-4
2. suruali inavaliwa - siku 4- week
3. chupi week nzima
soksi week 1
 
Mkuu ingia Nairobi, wengi wa makondakta wako smart hasahasa wa "matatu" tena magari yapo standard mpaka konda ana kiti chake... WaKenya Wapo vizuri kwenye kusimamia Sheria, Tanzania tupo vizuri kwenye kuziburuza sheria
Yale yale ya kuamini cha nje ndo kizuri na cha kwenu kibaya, unaambiwa mpk marekani wachafu unaleta sifa za kenya.
 
Yale yale ya kuamini cha nje ndo kizuri na cha kwenu kibaya, unaambiwa mpk marekani wachafu unaleta sifa za kenya.
Mkuu.. Upo Marekani....?
Sasa hawa wa kwetu tutembee na ndoo za maji au? Tatizo serikali ipo down kwenye kusimamia Sheria inazoziweka
 
Back
Top Bottom