Usafi wa Jiji bila vitendea kazi kwa kukosa "forex" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Usafi wa Jiji bila vitendea kazi kwa kukosa "forex"

Discussion in 'Jamii Photos' started by BAK, May 15, 2010.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  May 15, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,612
  Likes Received: 82,201
  Trophy Points: 280
  <TABLE border=0 cellSpacing=0 cellPadding=0 width="100%"><TBODY><TR><TD vAlign=top align=middle>[​IMG]</TD></TR><TR><TD class=kaziBody vAlign=top align=left>Baadhi ya Makampuni yanayokabidhiwa zabuni za kufanya safi katika barabara jijini Dar es Salaam hazina vitendea kazi kama alivyokutwa mfanyakazi huyu akizoa mchanga katika barabara ya Kilwa kwa kutumia kipande kidogo cha bati. (Picha na Yusuf Badi).</TD></TR></TBODY></TABLE>
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  May 15, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,612
  Likes Received: 82,201
  Trophy Points: 280
  Inakuwaje kampuni inapewa mkataba wa kusafisha jiji wakati haina vitendea kazi vya kufanyia usafi? Sasa huyo Mama hapo anasafisha kweli au anahangaika tu!? Hii mikataba inayotolewa kishkaji chini ya meza inaharibu sana Tanzania yetu. Si ajabu kampuni hizi zenye mikataba ya kusafisha jiji ni za wanene mbali mbali Serikalini. Wanatia ndani mabilioni kibao huku jiji likiendelea kunuka kwa uchafu uliokithiri.
   
 3. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #3
  May 15, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Kwa nini jiji lisiajiri wasafishaji wenyewe na kuwa na vifaa vyake yenyewe? Ujinga tuuuu kila kona.
   
 4. Injinia

  Injinia JF-Expert Member

  #4
  May 15, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Si ndio hapo sasa. Kwani hizo kampuni zinakitu gani cha ajabu ambacho Manispaa/ Jiji hazina?
  Tena wangeacha kununua magari ya milioni 100 wanunue Suzuki au Toyota ya kawaida (4 wheel drive ya nini mjini??) wanunue yale magari ya kufagia na kubebea taka.

  Kweli ujinga mtupu
   
 5. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #5
  May 15, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Injinia,

  Hayo ndio masharti Serikali iliopewa kwene haya ma-SEAP na madudu mengine, kwamba serikali isijishughulishe na utoaji huduma na badala yake kazi hiyo ifanywe na watu binafsi. Cha kusikitisha ni kwamba hakuna uboreshaji wowote wa maana ambao tunaeza kusema umepatikana na hizi sekta binafsi. Na kituko zaidi, kwenye kadhia kaa hizi anayefaidika ni mwenye kampuni. Utakuta yupo town anasukuma ndinga ya maana thanks to tenda ya halmashauri , ilhali hao wamama wafagizi(mind you, wengi wao ni wajane) wanalipwa pesa mbuzi ambayo huezi kuamini. The same stupidity in policy ndio unakutana na kadhia kaa ile ya akina Kingunge na kituo cha mabasi Ubungo. With this same spirit ndo unakuta mpaka ukarabati wa kawaida wa mabarabara ya vumbi huko mawilayani wanapewa hadi Wachina halafu eti tunakaa tunaulizana kwanini tu maskini? Are we for real?

  Lakini kinyume chake, serikali inge-take charge ya kusimamia shughuli hizi kwanza ingetoa ajira kwa watu wengi zaidi kwa sababu kusingakuwa na sababu ya kulipa zaidi kwa mwenye kampuni binafsi. Pili ingeweza kuwa kusimamia utekelezaji na ku-link na shughuli nyingine kama maboresho ya sehemu za madampo et etc..
   
Loading...