Usafi na Vivutio vya Dar es Salaam | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Usafi na Vivutio vya Dar es Salaam

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by ndeanasia, Feb 12, 2009.

 1. n

  ndeanasia Member

  #1
  Feb 12, 2009
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani,

  Naomba tuongelee maswala ya usafi na vivutio vya Dar es Salaam kama Jiji Kuu la Tanzania. Hivi taka kuzagaa kila mahali, mashimo kwenye barabara kuu za jiji, mitaro iliyojaa uchau na mimea, ofisi za serikali chafu na ambazo hazina vyoo vinavyofanya kazi wala kusafishwa, na kadhalika na kadhalika ina maana gani kwa jiji lenye biashara na majengo makubwa na madogo vyote hivi vikiwa ni vyanz vikubwa sana vya mapato na kodi kubwa asilimia 80 ya nchi nzima ikitokana na Dar es Salaam! Mameya watatu Regional Commissioner, Ma DC watatu zaidi ya watendaji kibao wa serikali kuu, serikali ya mitaa na wengineo wana fanya kazi gani hawa haswa? Na kwanini waendelee kuvumiwa hivi na huku tunalipa kodi zetu> Hvi kweli hawa waheshimiwa wanafikiri wao wanawajibika kwa nani haswa ni kwa Rais amabaye kutwa wakisimama kwenye majukwaa hawaishi kumaja kana kwamba waliwekwa hapo kumwimbia ngonjera tu! Hata pale anapowashushua bado hawpati somo? Hivi majuzi aliwauliza wanachokifanya kuboresha mazingira ya Jiji ndio kwanza mwingine akasimama kwenye jukwaa juzi anamuigiza Rais ka kurudia aliyosema badala ya kuweka mkakati na jinsi ya kutekelezwa na kuhakikisha anasimamia utekelezaji wake.
  Mimi nimechoshwa na uzembe huu na kwa kweli nahitaji ushirikiano kuwashinikiza hawa viongozi kututendea haki siye walipa kodi kwa kutuhudumia.

  Tuedeleze huu mjadala kwa mawazo na mikakati ili hatimaye tuyapeleke kwa wahusika wastahiki mameya na watendaji wao. Huu Uswahili ukome sasa!
  Fed up

  Ndeanasia
   
Loading...